Marehemu Mzee George F. Mbowe
Ilikuwa tarehe 28 february 2012 ulipotutoka
ikawa dakika, masaa, masiku, hadi sasa ni mwaka mmoja na kwenda kupumzika kwa
Bwana! Kweli hatukujua kwamba usiku ule Mungu alikuwa anaenda kuita jina lako.
Katika maisha sisi tulikupenda sana, na tutaendelea kukupenda hata katika kifo
Tumevunjika mioyo kwa kuondokewa na wewe lakini haukwenda mwenyewe, umeondoka
na sehemu ya mioyo yetu uliporudi nyumbani kwa Baba!
Amani na upendo
uliyotuachia ni mwongozo kwetu. Hata kama hatukuoni lakini upo pamoja nasi.
Maisha yetu yamebadilika bila wewe lakini hata sisi Mungu atatuita mmoja mmoja
ili tuonane tena! Tuonane paradise! Tuonane mtoni!
“Nimevipiga
vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda; 2 Timotheo 4:7”
Familia ya Marehemu George F. Mbowe watakuwa na misa ya wafu huko Dodoma katika kanisa
la Mviringo Anglican, siku ya jumamosi 2nd March, 2013 saa nne asubuhi.
Karibuni sana kushirikiana nasi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...