Mbunge wa kuteuliwa kwa tiketi ya Chama cha NCCR-Mageuzi, Bw. James Mbatia, aliwasilisha hoja binafsi bungeni mjini Dodoma iliyoainisha suala zima la udhaifu uliopo katika sekta ya elimu nchini. 

 Katika hoja hiyo, Bw. Mbatia alisema kukosekana kwa mitaala katika shule za msingi na sekondari, kunachangia wanafunzi kufanya vibaya. 

 Alisema hali hiyo inachangiwa na utendaji mbovu wa kitengo cha kuandaa mitaala hiyo ambacho kimeshindwa kufanya kazi zake ipasavyo na kusababisha usambazaji vitabu kunuka rushwa. 

 Hoja hiyo iliibua mvutano mkali kwa wabunge ambao baadhi yao walishauri iundwe Kamati Teule ya Bunge kuchukuza udhaifu huo na wengine wakitaka hoja hiyo ifanyiwe kazi na Serikali.
 Mbunge wa Kuteuliwa (NCCR- Mageuzi Mhe James Mbatia (kushoto) akiongea na waandishi wa habari  katika Ukumbi wa Msekwa mjini Dodoma baada ya kuambiwa aondoe hoja yake ambako alikataa.(Mwengine), ni  Mnadhimu Mkuu wa Upinzani Mhe Tundu Lissu

 Naibu Waziri wa Fedha Mhe Janet Mbene(kushoto) akisalimiana na Mbunge  Khalifa Suleiman Khalifa (Gando) kat[ka viwanja vya Bunge leo mjini Dodoma
 Wabunge wa Upinzani Mjini Dodoma leo walipokutana na waandishi wa habari na kutoa taarifa ya msimamo wao baada ya Mbunge wa Kuteuliwa (NCCR – Mageuzi) Joseph Mbatia kuambiwa aondoe hoja yake Bungeni  na kukataa
Naibu Spika wa Bunge Job Ndugai (kulia) akisalimiana na Mbunge wa Kuteuliwa (NCCR-Magaeuzi) James Mbatia katika viwanja vya Bunge leo mjini Dodoma. Picha zote na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO
Kwa habari kamili BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. kazi nzuri wapinzani kuwatetea wanyonge ila uchaguzi ujao muungane kama walivyofanya Kenya

    ReplyDelete
  2. sheikh khalifa huo mzuzu,baraghashia na kumpa mkono mama inakuaje?

    ReplyDelete
  3. We mdao hapo juu wacha zako! Imani ziko makanisani na msikitini! You gotta go practice there!

    ReplyDelete

  4. sidhani kama ni kweli Tanzania haina mitaala mimi nimemaliza form 6 tambaza nakumbuka kabisa mwalimu wangu wa tuition alinipa copy ya mitaala yoote biology, physics na chemistry

    hata nilipokua o level nilikua na copy za mitaala yoote na leo hii na kiri kwamba ni elimu hyo hyo imenipa nafasi ya kusoma ivy league schools sasa nashanga wanaposema hakuna mitaala i dnt see any point hapo

    ReplyDelete
  5. Ulitaka ampe nini?

    ReplyDelete
  6. Wewe unayesema umesoma Tambaza hujui unachokiongea. Tunapoongelea mitaala ya elimu tunazungumzia the entire education system in Tanzania. Siyo tu kuanzia ngazi ya sekondari au high school bali kutokea darasa la kwanza mpaka chuo kikuu. Wala si kwa baadhi ya affluent institutions tu (kama hiyo Tambaza ambayo inatukuka kwa kuchukua watoto wa wakubwa na wa 'mafisadi' na pia wizi wa mitihani), bali kwa ajili ya shule zote katika nchi zima hadi vijijini.

    Si kila mtoto wa Kitanzania anapitia Tambaza, na wala si kila mtoto anaweza akaafford tuition fees kama wewe ulivyoafford. In order to understand and critically analyse this whole subject, you have to think in broad terms. Think in terms of the majority. Kwa mfano, hivi wewe unafikiri kila mtoto Tanzania anaweza akawa na access ya tuition kama uliyopata na hatimaye kuingia Ivy League?? Tatizo watu kama nyinyi huwa mnabahatika kwenda nchi za watu halafu mnabweteka na kuingiwa na ulimbukeni kiasi cha kusahau nchi yenu ilivyo na kutotambua 'reality on the ground' ilivyo kiasi kwamba mnashindwa hata kutoa upembuzi wenye mantiki, hence usomi wenu wote unakuwa hauna maana yoyote kwa jamii ya Kitanzania.

    Ukweli ni kwamba our education system is broken, na hapo Mbatia anachojaribu kufanya ni kupiga vita mafisadi wa elimu na kuwapigania wanyonge ambao ndio majority. He is a hero and he ought to be commended! I mean, endapo kama imefikia hatua watoto wanamaliza darasa la saba bado wakiwa hawawezi kujieleza, hawajui kusoma, na wala hawajui kuandika bado unafikiri hiyo ni curriculum ya kutetea?? Na hapo unadai umeenda 'Ivy League', Ivy League gani hiyo uliyoenda kama unashindwa hata kutoa uchambuzi ulio na tija kwa taifa lako katika sensitive issue kama hii??

    Na wewe michuzi usibanie hii comment please, tumechoka na hawa watu wanaojifanya 'wa ughaibuni' ilhali wanatetea ufisadi kila kukicha!

    Mdau - Bucks.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...