Mv Victoria ikijitayarisha kwa ajiri ya kufanya safari yake usiku wa leo kuelekea mjini Bukoba mkoani Kagera mara baada ya kukaguliwa kufuatia kunusurika kuteketea mchana wa leo kupitia sakata la wachomeleaji walio sababisha moto uliozuka eneo la kuhifadhi mizigo.

Mv. Victoria ikipakia gari usiku huu hatimaye kuanza safari yake usiku huu.

Nao wasafiri walipanda kama ada licha ya baadhi yao kuonekana kuwa na wasiwasi na wengine kuahirisha kabisa safari.

Ndani ya meli abiria wakitathimini mazingira.

Saa 3 na dakika 10 meli ya Mv. Victoria inaondoka Mwanza.... kuelekea Bukoba mkoani Kagera. Picha na Mdau G Sengo 

Kwa picha za awali za tujio lenyewe BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Wahandisi watakuwa wameikagua na kuhiruhusu(May be).

    Ankal siku hizi ndiyo umeacha kutoa somo la upigaji picha hata mara moja kwa mwezi?.Picha ya chini kabisa unaweza kuona kama ina matone ya maji,hapa tunaweza kuhisi maji ya ziwa lakini picha za Usiku/giza kama ww si mtaalam zinatoka hivi hata kama hakuna maji yanayondondoka na mimi nina tatizo hilo hilo nikipiga picha kwenye giza/Usiku kwa kutumia flash.TATIZO nini?Karibu Ankal.

    David V

    ReplyDelete
  2. Hivi ni kwanini meli hii HAISIMAMISHWI AU MPAKA ILETE MAAFA MAKUBWA KAMA YALE YA MV. BUKOBA? Mwishoni mwa mwaka jana nikiwa maeneo ya Kamanga ferry, nilishuhudia kwa macho yangu meli hii ikiwa inatokea Bukoba ikiwa imelalia upande mmoja na humo ndani ilikuwa na malori kadhaa, mabasi makubwa, magari madogo na abiria wa kutosha. Niliendelea kuingalia tokea mbali mpaka ilipotia nanga ndipo niligundua kwa vile imeshaegemea upande hata haiendi speed. Jamani hivi nyie SUMATRA, Waziri mwenye mamlaka hamjaliona hili au mpaka VIFO vitokee? Meli haitakiwa kabisa kuendelea na safari.

    ReplyDelete
  3. Msijisumbue Abiria:

    Kulikuwa na sababu ya kuahirisha safari kama chombo kimesha fanyiwa ukaguzi na ikaonekana kitamudu?

    Kwa kuwa licha ya tahadhari kabla ya hatari kwa kuhakiki chombo hizo ni taratibu tu,

    Pamoja na kwamba uzembe upo, pana sehemu inafikia ukomo wa binaadamu unafikia mwisho, LA MUHIMU NI KUWA KIFO HUPANGWA NA MUNGU!

    ReplyDelete
  4. Ahsante Mdau wa Mwanza Mdau G.Sengo!

    Kwa mahesabu ya haraka haraka ni kuwa tikea hiyo saa 3:10 usiku itakuwa uwezekano chombo kimesha wasili Bukoba, je unazo umeshafanya nao mawasiliano kama walifika vyema?

    Tunaomba utujuze!

    ReplyDelete
  5. Mnaahirisha safari?

    Mnafikiri kifo kinakatiwa Denge?

    Kaeni mkielewa ya kuwa Mwenyezi Mungu anauwezo mkubwa sana, anayopanga daima hutimia!

    Unaweza kuahirisha safari ukafa (tena muda mchache baada ya kuahirisha safari yako) kwa kugongwa na pikipikiau au kabisaaa ukafa usingizini ukiwa umelala!

    ReplyDelete
  6. Israeli MTOA ROHO ZA WATU, alifika kwa jamaa mmoja. Akamwambia kuwa leo ndo siku yako iliyopangwa nikutoe duniani kwa kuwa katika list niliyo nayo jina lako ndo la kwanza. Yule jamaa kusikia hivyo akafanya ujanja, akamwambia ISRAELI kuwa yeye anapenda sana kula, na hivyo kabla hajamtoa duniani, anaomba ampe muda apike chakula ili ale kwa mara ya mwisho.

    ISRAELI alimkubalia. Yule jamaa alipika chakula, akapakuwa sahani mbili, ya kwake na ya ISRAELI. Katika sahani ya ISRAELI alimwekea DAWA YA USINGIZI. ISRAEL alikaribishwa chakula akakubali. Baada ya kula ISRAELI alipata usingizi mzito.

    Kutokana na usingizi wa ISRAELI, yule jamaa alipata fursa ya kumpokonya ISRAELI ile KARATASI yenye list ya ratiba ya WATU KUTOLEWA ROHO. Akakata kwa umaridadi kipande cha juu na kulitoa jina lake, kisha akachukua kalamu na kuliandika jina lake mwishoni.

    ISRAELI mara akatoka usingizini, akamtazama jamaa. Akamwambia, kwa kweli wewe ni mkarimu sana. Kutokana na ukarimu ulionifanyia, nimeamua kubadilisha mtizamo. Kwa leo nitamtoa ROHO mtu wa mwisho katika list yangu.

    Yule jamaa kusikia hivyo, akasema KWELI KIFO HAKIKIMBIWI.

    Hadithi hii inatufundisha kuwa KAMA SIKU YAKO IMESHAFIKA, hata uhairishe safari KITAKUPATA tu.

    ReplyDelete
  7. Mdau wa sita anony wa Sat Feb 09, 12:40:00 am 2013

    Hahahahaha!

    Unenichekesha saaana!,,,ili kumkwepa ISRAELI laiti jamaa angejua walau angeacha jina lake juu au angelitoa kabisa akaweka la mtu mwingine kabisaaa chini!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...