KIASI cha Sh. Milioni 200 kitatumika kwa ajili  Tamasha la Pasaka mwaka huu, ambalo kwa mara ya kwanza litafanyika katika mikoa saba tofauti.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha hilo, Alex Msama alisema fedha hizo zitatumika kwa masuala mbalimbali ikiwemo kulipa wasanii, misaada katika masuala mbalimbali ya kijamii na gharama za kawaida mahali watakapofanya maonesho. “Kila mwaka Tamasha la Pasaka linafanyika katika mikoa miwili, kwa maana ya Dar es Salaam na mkoa mwingine tutakaouchagua, lakini mwaka huu kwa mara ya kwanza litafanyika katika mikoa saba.

“Kwa hiyo gharama zake kidogo zitaongezeka na tunakadiria kwa mikoa yote hiyo kiasi cha Sh. Milioni 200 kitatumika maana tutakuwa na wasanii zaidi ya 30, tunaamini wengi watajumuika nasi kulipa viingilio ili kuwezesha dhamira yetu ya kupeleka ujumbe kwa njia ya muziki ufike,” alisema Msama. Alisema tayari wamekubaliana Machi 31 mwaka huu ambayo ni siku ya Pasaka tamasha lifanyike Dar es Salaam, lakini baada ya hapo mikoa mingine itakayofuata wataitangaza.

Msama alisema dhamira yao safari hii kwenye tamasha hilo ni kuhamasisha umoja, amani na mshikamano miongoni mwa jamii ya kitanzania. “Kila mwaka huwa tuna jambo ambalo tunaliangazia, safari hii tumeamua kuwa tamasha letu litasisitiza amani na upendo,” alisema Msama.

Tamasha la mwaka jana baadhi ya waimbaji mahiri waliokuwepo ni Rose Muhando, Rebecca Malope, Christina Shusho, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Solomon Mukubwa, Atosha Kissava, Ephraim Sekeleti na kundi la Glorious Celebration.

Pia kwaya mahiri ya Kinondoni Revival, Mwinjilisti Faraja Ntaboba kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) zilikuwa miongoni mwa burudani zilizokuwepo siku hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...