Askari Polisi wakiwa wanashusha magunia ya bangi ambayo yalikuwa yanasafirishwa kutoka Arusha kuelekea Dar es salaam kwa gari aina ya Fuso lenye namba za usajili T 282 AAJ
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi Liberatus Sabas akiwaonyesha waandishi wa habari madawa ya kulevya aina ya bangi ambayo yalikamatwa na jeshi hilo tarehe 07/02/2013. Picha na mahmoud ahmad wa Globu ya Jamii, Arusha
Na Rashid Nchimbi wa
Jeshi la Polisi Arusha
Jeshi la Polisi
mkoani hapa limemkamata mtu mmoja akiwa na magunia 97 ya madawa ya kulevya aina
ya bangi ambayo yalikuwa yanasafirishwa toka mkoani hapa kuelekea Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi wa
Polisi Liberatus Sabas amesema kwamba, tukio hilo lilitokea muda wa saa 10:00
alfajiri eneo la Usa River wilayani Arumeru.
Alisema mafanikio
hayo yametokana na ushirikiano mzuri kati ya jeshi hilo na wananchi ambapo
taarifa za tukio hilo zilitolewa na raia wema ambapo askari wa jeshi hilo waliweka
mtego eneo hilo na kufanikiwa kulikamata gari aina ya Fuso lenye namba za
usajili T. 282 AAJ.
Kamanda Sabas
aliongeza kwa kusema kwamba, ndani ya bodi ya gari hilo kulikuwa na mboga aina
ya kabeji iliyosambazwa vizuri huku chini ya mboga hiyo kukiwa na madawa hayo
yaliyokuwa kwenye magunia huku yakivingirishwa kwenye mifuko ya “plastiki” kwa
ndani.
Alisema katika gari
hilo kulikuwa na watu watatu na mara baada ya askari hao kulisimamisha dereva
pamoja na msaidizi wake walifanikiwa kukimbia huku mtu mmoja aliyejulikana kwa
jina la Praygod Marick (22) Mkazi wa Dar esalaam akikamatwa.
Jeshi la polisi
Mkoani hapa linaendelea kumhoji mtuhumiwa huyo huku watuhumiwa wengine
wakiendelea kutafutwa. Kwa mara nyingine tena Kamanda huyo aliendelea
kuwashukuru wananchi wa Mkoa huu kutokana na ushirikiano wao mkubwa wanaoutoa
kwa jeshi hilo na kuendelea kuwasisitizia kuimarisha mahusiano na jeshi hilo.
Kwa muda wa kipindi cha
mwezi mmoja toka Januari 07, 2013 mpaka hivi leo jeshi hilo limeshakamata
madawa ya kulevya aina ya mirungi magunia 372 katika magari mawili tofauti na
pia limeshakamata jumla ya magunia 117 ya madawa ya kulevya aina ya bangi
ambapo mwanzoni mwa wiki hii jumla ya magunia 20 yalikamatwa yakiwa
yanasafirishwa kwa kutumia wanyama aina ya Punda maeneo ya Losoiti wilayani
Longido.
Mkuu Sabas, unaposhika mihadarati ushikage huku ukiwa umevaa "Gloves"
ReplyDeleteNi ushauri tu
hivi jamani hizo biashara zimeanza leo huko arusha? mbona miezi hii tu ndio habari za kukamatwa kwa bangi zimeshika moto au kuna afande katoswa ulaji?
ReplyDeletehapo lazima itakuwa kuna afande kakosa ulaji sasa kaamua kuwatia adabu hao wauza bangi kwa kukamata mizigo yao yote
bange ipo miaka nenda rudi sasa iweje ikamatwe hizi siku tu?
haya hongereni sana maafande arofonso.
Mdau wa kwanza ukiona hivyo ni kuwa huyo Bosi aliyepita alikuwa anakula nao hao watu ndio maana mambo hayakuwa yanaharibika!
ReplyDeleteSasa nadhani huyu Bwana Mkubwa Kamanda aliyeingia sasa, kama sio Mlokole atakuwa ni Kijukuu cha Nyerere,,,watapita wapi?
Haaaa,!
ReplyDeleteMagunia 97 si lori zima hilo?
Inakuwa kama ni mzigo wa mahindi au mchele wa chakula vile?
Ndio maana idadi ya machizi ni kubwa sasa nchini!
fereeeeee chezea arusha kwa bangi,
ReplyDelete
ReplyDeleteNakubaliana mia kwa mia na ANON wa kwanza,
KAMATENI MARUNDO KAMA HAYA YA COCAINE, HEROINE, SILAHA HARAMU, PASSPORT ZINAZOUZWA KWA WASIO RAIA, MAKONTENA YALIOJAA WAHABESHI HAPO TUTASEMA NDIO.
SIO MARUNDO YA MAJANI ETI MADAWA YA KULEVYA.