Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM-Bara),Ndg. Philip Mangula akiteremka kutoka kwenye ndege ya shirika la Tanzania (Air Tanzania) ,kwenye uwanja wa ndege wa Kigoma leo asubuhi.Ndg. Mangula yupo Mkoani Kigoma kwa Maadhimisho ya Miaka 36 ya CCM

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM-Bara),Ndg. Philip Mangula akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma,Mh. Issa Machibya wakati alipowasili kwenye kwenye uwanja wa ndege wa Kigoma leo asubuhi.Watatu kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Juimuiya ya Wazazi Taifa,Ndg. Dogo Iddy Mabrouk.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM-Bara),Ndg. Philip Mangula (kushoto) akisalimiana na Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha - Rose Migiro wakati alipowasili kwenye kwenye uwanja wa ndege wa Kigoma leo asubuhi.Katikati ni Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi wa CCM,Ndg. Nape Nnauye.

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM-Bara),Ndg. Philip Mangula akiwasalimia wananchi wa Mkoa wa Kigoma waliojitokeza kumpokea kwenye uwanja wa Ndege wa Kigoma leo.
Vijana wa Chipukizi wa Mkoa wa Kigoma wakimsalimia Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara,Ndg. Phillip Mangula (hayupo pichani).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...