Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akivuta waya kuashiria kufyatua mtego wa kuwasha moto wa kuteketeza Silaha haramu, wakati alipokuwa mgeni rasmi katika zoezi hilo la uteketezaji wa silaha haramu, Lililofanyika katika Kambi ya Magereza jijini Dar es Salaam, Jumamosi Feb 16, 2013. Kushoto kwake ni Kamishna msaidizi wa Jeshi la Polisi Tanzania, Simon Siro na wa pili kulia kwake ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Perera Ame Silima na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kmataifa, Benard Membe.
Sehemu ya Silaha hizo zikianza kuteketea kwa moto baada ya Makamu wa Rais, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, kufyatua waya maalumu wa kuwasha moto huo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi, baada ya kusimamia zaoezi la uteketezaji wa Silaha haramu, lililofanyika Ukonga jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi, Simon Siro, wakati wakipita kukagua sihala hizo haramu kabla ya kuanza kwa zoezi la uteketezaji wa silaha hizo haramu lililofanyika Ukonga jijini Dar es Salaam.
Silaha haramu zilizoteketezwa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati wa zoezi la uteketezaji wa Silaha Haramu, lililofanyika Ukonga Jijini Dar es Salaam.
Wimbo wa Taifa, kabla ya kuanza kwa zoezi hilo. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Hivi sio hasara kuteketeza silaha,hata kama ni haramu? Kwa nini zisirasimishwe zikaingizwa katika vyombo vyetu vya ulinzi na usalama? Naomba kuelimishwa

    ReplyDelete
  2. Je wanamazingira hapo wana kauli gani?

    ReplyDelete
  3. Mbona AK47 hawakuzileta hapo kuharibiwa?...zinauzwa tena mitaani...!

    ReplyDelete
  4. Hivi Majeshi yetu yana silaha za kutosha hadi tuteketeze hizi??

    ReplyDelete
  5. Ohhh marundo yote hayo?

    Tena inaonekana ni Migobore migobore hakuna mamashine ya maana kama Sub Machine guns.

    Ama kweli kazi tunayo kwa silaha haramu!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...