Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akimshika kwa furaha mtoto aliyezaliwa tarehe 5.7.2013 katika hospitali ya Mkoa wa Lindi, Sokoine huku mama wa mtoto huyo Muksim Issa ,19, anayetoka katika kijiji cha Mumbu kilichoko katika wilaya ya Lindi vijijini aliyelala kitandani akitabasamu. Mtoto huyo alizaliwa akiwa na uzito wa kilo 3.9 Mama Salma alitembelea hospitalini hapo kukabidhi vifaa vya hospitali tarehe 6.2.2013. Aliyesimama kulia kwa Mama Salma ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Lindi Dr. Nasoro Hamid.
Kikundi cha utamaduni kikiwatumbuiza waalikwa kwa ngoma ya Tambiko inayochezwa na watu wa kabila la Wamakonde wakati wa sherehe ya kukabidhi vifaa vya tiba kwenye hospitali kuu ya mkoa wa Lindi, Sokoine, tarehe 6.2.2013.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwahutubia viongozi na wafanyakazi wa hospitali ya mkoa wa Lindi, Sokoine,na wananchi waliohudhuria sherehe ya kukabidhi rasmi vifaa vya tiba kwenye hospitali hiyo tarehe 6.2.2013 huko Lindi Mjini. Waliokaa kushoto kwa Mama Salma ni Kaimu Mganga Mfawidhi wa hospitali Dr. Nicolaus Munni, Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ambaye pia ni Meya wa Lindi Mjini Ndugu Frank Magali na wa mwisho ni Mwakilishi wa Project C.U.R.E. nchin Tanzania Bwana Makembe Kimario.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akikata utepe kuashiria kukabidhi rasmi kwa vifaa vya hospitali ya mkoa wa Lindi,Sokoine, vilivyotolewa na Taasisi ya WAMA kwa kushirikiana na Shirika la Project C.U.R.E. la nchini Marekani. Vifaa hivyo vina thamani ya zaidi ya shilingi milioni mia saba. Kulia kwa Mama Salma ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Lindi ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Lindi Dr. Nasoro Hamidi akifuatiwa na Katibu wa CCM WA Mkoa huo Ndugu Adelina Gefi na kushoto ni Kaimu Mganga Mfawidhi wa hospitali Dr. Nicolaus Munni. Sherehe hiyo ilifanyika tarehe 6.2.2013.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Mtoto amezaliwa tarehe 5/7/2103?

    Mjomba mbona unaziharakisha siku?,,,Inshallah, tukijaaliwa tufikie muda huo.

    ReplyDelete
  2. Nguo za mama Salma pamoja na utepe vimependezesha sana picha hii, ila kitambaa cha meza kimeharibu!!!

    ReplyDelete
  3. Kweli Watanzania wengine, sisi vitu tunavyo angalia; vinaturudisha maendeleo nyuma. Unachokizingatia kinadhihirisha ukweli wa upeo wako! Hata maamuzi sahihi yanatupa shida, kutokana na fikra zetu finyu.

    Mama aksante kwa vifaa. Vitaokoa maisha ya wengi hasa kina mama na watoto. Naomba juhudi hizi ziwe kwa nchi nzima. Siya nyumbani tuu!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...