Na Freddy Macha
Maonyesho maarufu ya mavazi ya kimataifa –London Fashion
Week- yatamega kitengo chake cha kimataifa kusaidia kutangaza kazi za washoni
wapya toka Tanzania ndani ya Ubalozi wetu leo Ijumaa mjini London.
Mada ya maonyesho haya yatakayoendelea kwa juma zima ni “Swahili Flavour” (Ladha ya Kiswahili). Yametayarishwa
kwa ushirikiano wa Ubalozi wa Tanzania London na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB)
kujenga vipaji na kazi za mavazi za washoni wasiofahamika duniani.
Kazi
zitakazooyeshwa ni za washoni watatu Christine Mhando (anayetumia jina la
ubunifu: “Chichia London”), Anna Lukindo ( “Anna Luks”) na Jacquleine
Kibacha (“Heart 365”).
![]() |
Mbunifu Christine Mhando |
Christine Mhando
alihitimu chuo cha Usanii cha Kent mwaka 2002 na huhimiza mtindo wa Kanga na
misemo na manen ya Kiswahili mathalan “Tongoza” na “Zungumza” kama wajihi wa
kazi zake. Anna Luks aliyesomea shahada
yake chuo cha Middlesex, London hutumia vitambaa vya Kitanzania, kushona kwa
mikono, kamba kamba, mavazi ya kike na dunia ya kisasa. Baada ya kujiuzulu toka kazi ya kuajiriwa (kupanga
sera) Jaquileine Kibacha aliamua kufuata
ndoto zake za kuwa msanii. Ubunifu wake unaochanganya desturi za kijadi na
kisasa kutumia shanga shanga, manyoya ya ndege na mapambo imesanifiwa kutokana
na safari aliyoifanya kuishi na Wamasai.
Kina dada
hawa wanasisitiza kwamba wana lengo la kukuuza sanaa na ubunifu, utamaduni
wa Kitanzania, kutangaza taswira za Kiswahili na sura mbalimbali za Afrika
Mashariki.
Kaimu Balozi wa Tanzania, Mheshimiwa Chabaka Kilumanga
alisema kwamba maonyesho haya ya kimataifa yatakua nafasi kubwa kwa Tanzania
kujenga jina na ni sehemu mahsusi ya
kujivunia utamadunina nchi yetu.
Tovuti: www.freddymacha.com
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...