Michuano ya kuwania Kombe la Mataifa ya Afrika kwa upande wa soka(AFCON 2013) inaelekea ukingoni.
Usiku wa jana ulikuwa ni usiku wa michezo ya nusu fainali ambapo Nigeria walikuwa wanaumana na Mali na kisha Ghana wakavaana na Burkina Faso.
Katika mchezo wa kwanza Nigeria walifanikiwa kuingia katika fainali kwa kuichabanga vibaya timu ya Mali kwa jumla ya magoli 4-1 kabla ya baadae Ghana kutupwa nje ya mashindano ya mwaka huu kwa kuchapwa kwa mikwaju ya penati baada ya kwenda sare ya 1-1 katika dakika za kawaida na 30 za nyongeza.
Jijini Dar-es-salaam, mashabiki wa soka wameendelea kufurahia michuano ya AFCON 2013 sehemu mbalimbali kupitia SuperSport Channels ambazo zinapatikana Live na pia katika High Definition(HD) kupitia DStv. Mojawapo ya sehemu hizo ni viota vya Samaki Samaki jijini Dar-es-salaam.

Baadhi ya wafanyakazi wa kitengo cha mauzo DStv wakiongozwa na Meneja Mauzo, Salum Salum(mwenye t-shirt ya Blue) walikuwepo tayari kabisa kufurahi pamoja na wateja na mashabiki wa soka na pia kujibu maswali mbalimbali kutoka kwa wateja na mashabiki hao.
Ukimuuliza shabiki yeyote wa soka atakwambia kwamba soka ina raha yake unapotizama na marafiki. Lakini....soka ina raha ya kipekee unapoitazama kwenye kiwango cha High Definition(HD). Ni DStv pekee wanaokuwezesha kupata raha hiyo.
Cartoonist wa siku nyingi,Fred Halla alikuwa na mengi ya kuuliza lakini pia kusifia na kufurahia michuano ya AFCON 2013 kupitia DStv.
Soka, mijadala, kinywaji...AFCON 2013 ina mengi. Samaki Samaki-Mlimani City.
Baada ya kazi, ni AFCON 2013 kupitia DStv pekee!
Unapozungumzia michezo,unazungumzia SuperSport.Unapozungumzia SuperSport unazungumzia DStv.
Meneja Mauzo wa DStv,Salum Salum, amenidokeza kwamba Jumapili ijayo(tarehe 10 Feb) siku ya Fainali ya AFCON 2013 patakuwa na shughuli maalumu ya kumaliza msimu wa AFCON 2013 katika viota vya Samaki Samaki na sehemu zinginezo. Mashabiki watashinda zawadi mbalimbali na watapata kujua mengi zaidi kuhusu DStv ambao ni wakongwe wa digitali. Usikose kutizama fainali ambayo itakuwa kati ya Nigeria(Super Eagles) na Burkina Faso.
Ili kujua mengi zaidi yanayojiri kwenye luninga yako,Jiunge na ukurasa wa Facebook wa DStv Tanzania kwa kubonyeza hapa.
ReplyDeleteSAMAHANI, HII KIDOGO HAIHUSU HAPA:
DSTV PALE "ESSO" OYSTER-BAY, MMEREKEBISHA ILE MISTARI MIREFU SANA YA KULIPIA? MAANA KUSEMA KWELI KULIPIA HUWA NI UNYONGE MKUBWA, UKILALAMIKA UNAJIBIWA "SIYO LAZIMA UJE HAPA, LIPIA KWA SIMU AU NJIA MBADALA"
HILI SIO JIBU ZURI, UFUMBUZI NI YALE MADIRISHA MAWILI YALIYOPO KWA SASA, YOTE YAWE YANAFANYA KAZI, IKIWEZEKANA MUWEKE MADIRISHA ZAIDI ILI KUONDOA KERO HII.
HUWA KUNA MAZINGIRA YA UNYANYASAJI, JOTO, MSTARI MREFU, DIRISHA MOJA TU LINAFANYA KAZI.
MALIPO YA MWEZI YAKO JUU SANA SIO RAHISI KWA MTANZANIA WA KAWAIDA KUWEZA KULIPA
ReplyDeleteNi ukweli usiopingika Dstv ni king'amuzi pekee ambacho unaweza ukawaamini kidogo ukilinganisha na ving'amuzi vingine. Pls wengine igeni mfano kwa DSTV kwani mnatuzingua sana, mara inawezekana uliweka up side down au nini...mmeishia kuzuga zuga tu, ngoja tu mwisho wenu utajulikana tu msipobadilika na kuiga kwa Dstv. Hongereni....But you (DSTV) are giant compared to others...
ReplyDeleteHao oysterbay karibu ya kituo cha mafuta ni kero kubwa sana na yasiku nyingi,tafuteni ufumbuzi juu ya hili
ReplyDeleteNi wakati sasa muweke na local channels zingine zaidi ya TBC na Star Tv ili mtuvutie na sisi wengine... maana Tv moja ving'amuzi kibao, haipendezi...
ReplyDeleteMCHEZA KWAO, HUTUNZWA!!!!
Sio DStv pekee wanaonyesha... Al Jazeera tunaona game zote pia
ReplyDelete