Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limesema matokeo ya kidato cha nne bado hayajakamilika na kuwa habari zilizozagaa wiki hii kuwa yapo tayari si za kweli.
Hata hivyo Baraza hilo limebainisha kuwa licha ya kutokamilika, matokeo hayo yanakaribia kutoka kwa mujibu wa ratiba za baraza hilo ambapo hutakiwa kutoa matokeo hayo mwezi Februari.
Ofisa Habari na Mawasiliano wa NECTA, John Nchimbi amesema uvumi wa kwamba matokeo hayo yako tayari ulitokana na kuzushwa kupitia mtandao wa kijamii (Facebook).
Alifafanua kwamba habari kuwa matokeo hayo yameanza kutoka kisirisiri kabla hayajatangazwa rasmi na kwamba hatua hiyo inalenga kuyachakachua, siyo taarifa sahihi.
Aliwataka wananchi kuwa makini na uvumi huo kwa vile endapo matokeo hayo yatakuwa tayari yatatangazwa na Katibu Mtendaji wa Baraza hilo na pia kuwekwa kwenye tovuti ya Baraza pamoja na wananchi kuweza kuyapata kupitia simu zao za mkononi.
Hongereni sana kwa kufafanua jambo hili. Kuchakachua si jambo geni.
ReplyDeleteIngefaa NECTA iweke tarehe maalumu ya February ambayo itakuwa ndiyo tarehe na siku maalumu ya kutoa matokeo ya Kidato cha Nne. Tarehe maalumu kwa kutoa matokeo ya Kidato cha Sita n.k. Kusema tu yanatoka February. Mwezi ni mrefu kwa hamasa inavyokuwa!
NAWAPONGEZA JOPO LA MICHUZI BLOG, NA HII IWE FUNDISHO KWA BLOG UCHWARA ZINAZOJIFANYA NI MANAIBU MAKATIBU WA NECTA/ WIZARA NA KUSAMBAZA HABARI ZA UONGO IKIWEMO KUWEKA TOP TEN YA WALIOFAULU. AIBU KWAO KWANI WANARUDISHA MAENDELEO NYUMA
ReplyDeletemi naishauri necta ituweke wanafunzi katika hali itayotufanya tujijue tulipotoka na tunapokwenda tena kwa wakati yaani iwe inatoa tarehe maalum ya kutoa matokeo
ReplyDeleteVizuri wamesema wenyewe maana kila mtu alikuwa na tetesi zake
ReplyDeletematokeoo yanatoka lini tena brotherr
ReplyDeletekikubwa wekeni tarehe maalumu ya kutangaza
ReplyDelete