Pichani ni baadhi ya Wasanii watakao tumbuiza kwenye tafrija ya Montage Charity Ball itakayofanyika jioni ya leo ndani ya Serena Hotel,jijini Dar.Kutoka kushoto ni Peter Msechu,Kidumu kutoka Kenya,Barnaba pamoja na Deo Mwanambilimbi ambaye ni kiongozi wa Kulunde Band.
Pichani shoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Montage,Teddy Mapunda (katikati) akizungumza na Waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akielezea kufanyika kwa tafrija maalum ya harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia wanawake wenye matatizo ya afya hapa nchini kupitia mfuko wa Montage Charity Ball,itakayofanyika jioni ya leo, Februari 22 kwenye Hoteli ya Serena,jijini Dar es Salaam

Aidha Teddy ameeleza kuwa malengo hasa ni kukusanya kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 100 kwa ajili ya kusaidia matibabu ya Wanawake wenye matatizo mbali mbali.Mgeni rasmi katika Tafrija hiyo anatarajiwa kuwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA),Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.Kulia kwake ni baadhi ya Wasanii watakaotumbuiza kwenye tafrija hiyo ambao ni Kidumu kutoka Kenya,Barnaba pamoja na Deo Mwanambilimbi ambaye ni kiongozi wa Kulunde Band naPeter Msechu ambaye hayupo pichani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...