Habari mkubwa,
naomba msaada wako,Leo nimepoteza wallet yangu majira ya saa tano na nusu asubuhi.
Sina hakika sana ni wapi lakini mara ya mwisho nimeishihika wakati nikiweka mafuta kwenye gari pale Total Petrol Station ya Mlimani City. Niliweka mafuta kisha nikalipa pesa. Nilipowaomba risiti yule muhudumu akaniomba nisogee mbele kidogo ningoje ili waniletee risiti maana kulikua na magari mengi kidogo yanangoja huduma , hivyo nilisogeza mbele kidogo kisha nikapaki na ili kuokoa muda, nilishuka kumfuata aliyekua ananiletea risiti ili kuichukua.
Sasa ninahisi nilipotoa pesa sikurudisha wallet mfukoni bali niliiweka juu ya mapaja na hivyo niliposhuka huenda niliingausha chini na sikugundua. Nimekuja kugundua tayari niko Ukonga nilipokuwa nakwenda. Nimejaribu kufuatilia sijaipata hadi sasa hivi. Ndani ya wallet kulikua na pesa, vitambulisho, mastercards za bank tatu, leseni yangu ya udereva, kadi ya bima ya afya (green card), kitambulisho cha kazi na vitu vingine nisivyovikumbuka kwa haraka.
Business cards zilikua zimeniishia hivyo sina uhakika kama kuna kitu kilichokua na mawasiliano ya namna ya kunipata kama vile namba za simu. Kitambulisho changu cha kazi kinaonesha kuwa ni mwajirwa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Mlimani.
Kwa atakayekuwa ameikota ninaomba na ninatanguliza shukurani zangu kwa kunisaidia kunipa vilivyomo.
Namba zangu za simu kwa ajili ya mawasiliano ni: 0782 581941 au 0 713 581941 au 0756 581941
ASATENI.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...