Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba (kushoto) akiongea na aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Katiba ya Kenya Prof. Yash Pal Ghai katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam leo (Jumatatu, Feb. 25, 2013). Prof. Ghai amekutana na Wajumbe na kubadilishana nao uzoefu kuhusu uandishi wa Katiba Mpya.
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba (kulia) na Mjumbe wa Tume Bw. Simai Mohamed (katikati) wakiongea na aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Katiba ya Kenya Prof. Yash Pal Ghai katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam leo (Jumatatu, Feb. 25, 2013). Prof. Ghai amekutana na Wajumbe na kubadilishana nao uzoefu kuhusu uandishi wa Katiba Mpya.
Katibu wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Bw. Assaa Rashid (kushoto) akiongea na aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Katiba ya Kenya Prof. Yash Pal Ghai katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam leo (Jumatatu, Feb. 25, 2013). Prof. Ghai amekutana na Wajumbe na kubadilishana nao uzoefu kuhusu uandishi wa Katiba Mpya.
Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Prof. Palamagamba Kabudi (kushoto) akiongea na aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Katiba ya Kenya Prof. Yash Pal Ghai katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam leo (Jumatatu, Feb. 25, 2013). Prof. Ghai amekutana na Wajumbe na kubadilishana nao uzoefu kuhusu uandishi wa Katiba Mpya.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Katiba ya Kenya Prof. Yash Pal Ghai (kulia) akibadilishana mawazo na Naibu Katibu wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Bw. Casmir Kyuki (kushoto) na Mjumbe wa Sekretarieti ya Tume Bw. Joseph Ndunguru katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam leo (Feb. 25, 2013). Prof. Ghai amekutana na Wajumbe na kubadilishana nao uzoefu kuhusu uandishi wa Katiba Mpya.
Hili ni jambo la kupongezwa sana sana tena sana,iwapo tu ushauri wa huyu Msomi na Mtaalamu wa masuala ya Katiba,na aliyeonyesha kwa vitendo umahiri wake wakati akisimamia Uandikaji wa Katiba ya Kenya,iwapo ushauri wake utazingatiwa na Tume yetu bila ya ajizi kuja na Katiba inayofanana kwa kiasi kikubwa na Katiba ya Kenya!Mazingira ya Kenya na ya kwetu yanafanana sana.Kwahiyo, sioni tabu,iwapo hata Katiba zetu zitafanana pia.Ila pale tu,tutakapo weza kuifanya iwe Bora zaidi kuliko ile ya Kenya,lakini,sio kinyume chake!"Tutachekwa na kudharauliwa na Afrika yote na Duniani kote".Why?We had the opportunity to "create meaningful change,but,we did not use it wisely!".Thank you for your "listening" or was it for your "attention"?Hakuna Mtanzania ambaye ni muhimu zaidi kuliko Tanzania - tonny!
ReplyDeleteAnny Feb 25, 03:03:10:00pm 2013
ReplyDeleteNdugu yangu taabu sio kwamba Wasomi na Washauri hawapo si unaona Wamemwita Jaji Mkuu wa Kenya last week na leo huyu jamaa ambaye ni msomi mbobevu na mahiri katika masuala ya Katiba. Lakini wee nisikilizie, utaona hayo mapungufu hapo hiyo katika itakapokuwa tayari ndiyo utashangaa kuwa hawa wote waliitiwa nini na tume ya Katiba. Mpaka hivi sasa kuna kila aina ya mbinu ya kuichakachua hiyo katiba ili iwe na sura ya kuendelea kuibeba serikali iliyopo madarakani. Hivyo fujo na uhasama tunauanzisha wenyewe walau Kenya waliyaona wakaamua kufungua njia yenye mwanga na amani. Sisi bado hatujajitambua.
angalia watanzania walivyojikoki na masuti halafu walinganishe na huyo profesa uvaa wake.
ReplyDeleteILANI:
ReplyDeleteHao watakao ichakachua Katiba tunayoitarajia historia itawahukumu!
Wanaweza wakaihckachua lakini baadae ikawatokea hao hao puani, wakakuta inawabana wenyewe!
Hivi kuna mwenye uwezo wa Jini wa kutawala daima?
In Life,the only Konstant in change,is change itself!.Usibabadilika au Usipokubali kubadilika,basi Utabadilishwa na Mazingira ya Nyakati au Utalazimishwa Kubadilika na Mazingira ya Nyakati!Fumbo la kwanza Mwenyezi Mungu alompa Binadamu, ni la "Kuzaliwa,Kuzeeka na Kufa".Utazaliwa ukiwa huna kila kitu bali "utakatifu wako",kisha Utakua na kuongezeka ukubwa wa Maumbile na Uwezo wa Kufikiri na ukifanikiwa utapata elimudunia na utajiri wa mali,utazaa watoto,na baada ya hapo,polepole,utaanza kurudi nyuma ulikotoka,"Utotoni kwa mtazamo tofauti wa Uzeeni",utaanza kupoteza kimoja kimoja,kuanzia mvutowa maumbile,uwezo wa kufikiri,mali uliyochuma duniani,na HATIMAYE,"Kifo"!Hiyo ndiyo siri ya maisha.Haibagui,hata uwe nani hapa duniani,lazima upitie katika mchakato huo!"Kila utakalo tenda hapa duniani,ama litakujenga zaidi,au litakuporomosha au kukudhoofisha bila wewe mwenyewe kujitambua".Kila mtu hujichimbia Kaburi lake hapa duniani,wengine ni wasindikizaji tu!Tanzania Kwanza,Utanzania baadaye!Utaitwa Mtanzania kwasababu Tanzania ipo!Kwahiyo,tuitunze na kuilinda Tanzania yetu nzuri ili tuendelee kuwepo na kuitwa Watanzania!Katiba ni Ramani ya Kudumu au ya muda mrefu ya Kutuvusha salama watanzania wote katika safari ndefu iliyojaa majaribu na hatari za kila namna na kutufikisha katika Nchi ya Asali,nchi ya ahadi!Ubinafsi wa aina yoyote usipewe nafasi!Shetani hupenda sana kutumia udhaifu wa ubinafsi ili kumsambaratisha mkusudia!Tusimpe shetani wa ubinafsi nafasi!Bora tuchelewe lakini tufike salama,kuliko kulikoroga na tukasambaratika na kuwapa "Mwewe"faida!Nothing is Permanent in Life!
ReplyDelete