Na Freddy Macha

Waziri wa Nishati, Profesa Sospeter Muhongo (pichani) amewasili Uingereza leo jumapili tarehe 24.2.13 kwa ziara ya siku nne.
Waziri alipokewa na Balozi wetu mheshimiwa Peter Kallaghe na anatazamiwa kukutana na viongozi mbalimbali wa serikali ya Uingereza na wataalamu wanaohusiana na shughuli za madini, maendeleo ya kimataifa.
Miongoni mwa maofisa anaotazamiwa kukutana nao kesho Jumatatu  ni pamoja na Waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Kiafrika, Jumuiya ya Madola na nchi za Kigeni, Bwana Mark Simmonds;  Naibu Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa Uingereza, Bi Lynne Featherstone na Mbunge wa Stratford chama cha Conservative, Jeremy Leffroy  ambaye pia ni mwenyekiti wa kundi la Wabunge wa Uingereza wanaoshughulikia Tanzania (APPG).
Jumanne saa kumi na moja jioni Waziri ambaye pia ni Mbunge wa kuteuliwa amepanga kuongea na Watanzania wanaoishi Uingereza ukumbi wa Ubalozi wetu London. Ukumbi uko 3 Stratford Place, London W1C 1AS. Stratford Place iliyojishika na barabara kuu  ya Bond- ni sekunde chache tu mbele ya kituo cha magari moshi na mabasi cha Bond Street.
Waziri Muhongo anaongozana na Dk Athanas Macheyeki wa Ukaguzi wa Madini Tanzania, Seleman Hatibu Chombo wa idara ya Nishati katika Wizara ya Madini na Nishati na Bwana Sosthenes Masau Bigambo Massola, katibu wake muhtasi.
 Waziri Muhongo ni msomi aliyebobea ndani ya masuala ya kisayansi na taaluma ya mawe na madini. Mbali na kuwa profesa na mhariri wa jarida la  “Journal of African Journal Sciences” ni vile vile mwanachama wa  jumuiya mbalimbali za madini na sayansi za kimataifa. Jumuiya hizo ni “Geological Society of London,” “Geological Society of America,” “Chinese Academy of Geological Sciences” na “Tanzania Academy of Sciences.”
 Kiongozi huyu ni  Makamu Rais wa Tume ya Tume ya Ramani ya Madini duniani iliyoundwa 1881  Ufaransa. Lengo la tume hii ni kuendeleza masuala ya mazingira, madini na hali ya hewa ya ulimwengu  na Rais wake ni Philippe Rossi.
Mshindi wa tuzo kadhaa za kielimu na kisayansi, Profesa Muhongo alizaliwa Musoma mwaka 1954 akamaliza masomo yake vyuo vya Dar es Salaam na Ujerumani. Mwaka juzi alizawadiwa “Ordre des Palmes Academiques” ya serikali ya Ufaransa – inayotolewa kwa wataalamu waliochangia masuala ya kielimu na kitamaduni toka lipoanzishwa na Mfalme maarufu Napoelon karne ya 19.
 Mwaka 2007 kiongozi huyu alipewa tuzo la heshima (“Honours Award”) na Jumuiya ya Madini ya Afrika Kusini na 2004 akatunukiwa tuzo la “Robert Shackleton” la  Jumuiya ya Madini Afrika. Robert Shackleton aliyefariki 2001 ni Mwingereza aliyeendeleza uchimbaji madini Afrika Mashariki.
Nchini Tanzania Waziri Muhongo amepata zawadi ya Makamu wa chuo kikuu (1977), zawadi ya Gondwana (1979) na tuzo la kitaifa la utafiti wa kisayansi na teknolojia (NARST) linalotolewa na Tume ya Sayansi na Teknolojia Tanzania(2006).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Sound okay but all these qualification and award will be useful if at all the prof gears at reforming the madini sector and helping the wananchi in participating in the sector rather than the current situation where the owner (wananchi) wamebaki kuwa watazamaji tu.

    ReplyDelete
  2. Vyeti na tuzo lukuki zisaidie kuifaidisha Tanzania, wachimbaji wadogo na wakubwa wa madini ambao ni wazawa.

    Vyeti na tunzo kwa ajili ya nadharia viende mbali zaidi kukuza faida kwa vitendo na mali halisi kwa wengi.

    Mdau
    Mwalimu

    ReplyDelete

  3. Hii C.V ya professor ni nzuri sanaaa, yaani ipo solid kabisaa yaani ni GURU wa madini na miamba, LAKINI HII ELIMU ITAKUWA BURE KABISAAA HUYU JAMAAA AKIKUBALI KUTUMIWA NA MAKAMPUNI YA KIGENI AMBAYO YANAPORA MADINI YETU. Mwalimu Nyerere aliwahi sema Education is not a mere collection of certificates as legal tenders but how that education transform the lives of indigenous people in rural communities in Tanzania and Africa. Makampuni makubwa ya madini hayalipi kodi inavyotakiwa kwa sababu ndiyo watoaji wakubwa wa rushwa. Mpaka viongozi wa G8 waziri mkuu Cameroon alikiri hilo kwenye mkutano wa Davos World Economic Forum. Sasa huko Uingereza kama amearikwa na hao wageni yaani makampuni ya kibepari basi kuna mashaka. Ndugu michuzi usibane hii comment yangu ni kwa manufaaa ya watanzania wa vijijini. Kwa sasa hakuna ubishi Ulaya na Marekani wako hao kiuchumi na madeni makubwa. Hivyo sehemu ya hawa jamaa kutokea kama ilivyo historia yao ni kupora rasilimali za Africa. Tafadhali Watanzania wa Uingiereza muulize professor, je Tanzania sheria ya Madini imebadilishwa tunataka 50% kwa 50% share of ownership siyo 3% royality huu ni wizi na uporaji. Je wanalipa Kodi kuna kampuni tunajua zinadaiwa pesa nyingi ikiwemo Barrick Gold mine na nyingine ya Australia ambayo inadaiwa kuwa Bulyankulu Nzega je wamelipa? Je Barrick Gold Mine kwenye taarifa zake huko kwao na kwenye soko la dunia wanaonekana hawajawahi pata hasara mbona kuna vipindi vingi Tanzania hawa jamaa hawajalipa kodi kwa kisingizio cha kupata hasara? Fanya maamuzi magumu Professor kuhusu TANESCO safisha kama Dr.mwakyembe Bandari. umeme ni gharama kubwa Tanzania kwa nini?

    ReplyDelete

  4. Watanzania Uingereza Tafadhali muulize Professor maswali haya hapa

    1. Je amefanya nini kuanza kuhifadhi dhahabu Benki of Tanzania as part of national strategy for national reserve at the central bank, tengeneza sera kuwa 1% of madini lazima iwekwe central Bank. 2. Je amefanya nini kuanza kuprocess madini Tanzania kama vile Tanzania cutting and processing of minerals locally ili kuongeza ajira? Je amejiandaa vipi kukabiliana na nguvu za mabepari wa kimataifa katika kuwanyonya wazawa? Je yupo Tiyari kufanya maamuzi magumu kuanzisha kampuni Tanzu na TANESCO kwa umeme wa lipa ndogo vijijini kwa watu wengi wenye kimo cha chini cha mshahara?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...