Rais Jakaya Mrisho Kikwete Jumamosi hii ya Februari 16, 2013 amekwenda kuhani na kufariji ndugu, jamaa na marafiki wa familia zilizoondokewa na watoto na wazazi kufuatia ajali ya barabarani maeneo ya kijiji cha Kibiki, Ubena Zomozi katika mkoa wa Pwani iliyotokea Februari 11, 2013 na kupoteza hapohapo maisha ya watu nane wakiwemo wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Chalinze baada ya gari dogo aina ya Toyota Mark II walilokuwa wamepanda kugongana uso kwa uso na roli la mizigo.

Familia alizokwenda kuhani na kuzifariji ni pamoja na za marehemu Hassan Erasto Kurunge (57), Maria Sadiki ((52) na mtoto wa mwaka mmoja Samweli Ismail wa kata ya Ubena.

Wengie ni marehemu Essau Enos Mwamgingo (16) , Stella Isaack Kazimoto (18), Bahati George Mbena (17) na Latifa Maneno (17).

Akiwa ameongozana na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe Mwantumu Mahiza na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Ahmed Kipozi, Rais Kikwete alieleza kusikitishwa kwake kwa ajali hiyo, na kuwataka madereva wawe makini katika kuzingatia sheria za usalama barabarani.

Rais Kikwete alisikitishwa zaidi kwa taarifa kwamba gari hilo dogo lilikuwa limebeba abiria wanane, na kuwa dereva wake ambaye pia alipoteza maisha, hakuwa makini katika kuzingatia sheria za usalama barabarani.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa mkono wa pole na kuwafariji ndugu, jamaa na marafiki wa familia zilizoondokewa na watoto na wazazi wao kufuatia ajali ya barabarani iliyotokea maeneo ya kijiji cha Kibiki, Ubena Zomozi katika mkoa wa Pwani Februari 11, 2013 iliyoua hapohapo watu tisa wakiwemo wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Chalinze baada ya gari dogo aina ya Toyota Mark II lililokuwa limebeba abiria wanane kugongana uso kwa uso na roli.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia moja ya picha za ajali hiyo alizopewa na wanafamilia walioondokewa na watoto na wazazi wao kufuatia ajali ya barabarani iliyotokea maeneo ya kijiji cha Kibiki, Ubena Zomozi katika mkoa wa Pwani Februari 11, 2013 iliyoua hapohapo watu wanane wakiwemo wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Chalinze baada ya gari dogo aina ya Toyota Mark II lililokuwa limebeba abiria wanane kugongana uso kwa uso na roli.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifariji ndugu, jamaa na marafiki wa familia zilizoondokewa na watoto na wazazi wao kufuatia ajali ya barabarani iliyotokea maeneo ya kijiji cha Kibiki, Ubena Zomozi katika mkoa wa Pwani Februari 11, 2013 iliyoua hapohapo watu wanane wakiwemo wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Chalinze baada ya gari dogo aina ya Toyota Mark II lililokuwa limebeba abiria wanane kugongana uso kwa uso na roli.
Haya ndio magari yaliyopata ajali hiyo na kupelekea vifo vya watu wanane wakiwemo wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Chalinze.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Jina la mmoja waliofariki rekebisha ni Essau Enos Mwamgiga ahsante.

    ReplyDelete

  2. Mwendo ulikuwa wa kasi sana, ni msiba mkubwa.

    ReplyDelete
  3. inasikitisha, na hilo gari dogo naona ilikuwa inaendeshwa kwa spare tire ndogo, ukiendesha na spare tire ndogo aina hiyo unashauriwa usiende zaidi ya km50/ saa....poleni sana

    ReplyDelete
  4. Ohhh poleni na Msiba!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...