Islamic Development Bank (IsDB) itaipa Mozambique dola za kimarekani zisizopungua 68.3 Million ktk kipindi cha mwaka 2011- 2013, ameeleza hayo waziri anaeshughulikia maswala ya maendeleo Mhe, Ajuba Cuereneia jijini Maputo. 
Kiasi hicho cha pesa kinategemewa kutumika ktk miradi mbalimbali ikiwemo uvuvi, huduma za afya, maji masafi, ujenzi wa barabara, ugavi wa nishati na mengineyo.
 Waziri huyo aliyasema hayo ktk kongamano la uchumi unaofuata sheria za ki-Islam ambapo ulihudhuriwa na wachumi kutoka asasi mbalimbali nchini humo. Kongamano hilo lililkuja mfulilizo wa mikutano 36 ambayo inanyika kila mwaka ktk nchi tofauti ambapo Mozambique nayo iliomba iwe mwenyeji wa mkutano huo kwa ajili ya kuwafahamisha wananchi wake uhalisia wa benki zinazofuta sheria za ki-Islam. 
Malengo hasa ya serikali ya nchi hiyo pamoja na mambo mengine ni kukuza fursa za kiuchumi kwa taasisi za serikali na zile za watu binafsi, kuimarisha miundombinu, kilimo, na maeneo mengine kwa ajili ya kuimarisha ukuaji endelevu wa uchumi wa nchi hiyo na kupunguza umaskini. Kwa maelezo zaidi kuhusu uchumi unaofuta sheria za ki-Islam tembelea www.ijuebankyakiislam.blogspot.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Hizi habari za Mozambique zina tunatusaidia nini
    Please wekeni habari important kwa watanzania na mkopo kwa Mozambique hautusaidii chochote bongo.

    ReplyDelete
  2. Mdau Mozambique ni eneo Muhimu Kiuchumi kwetu!

    Kama huufahamu Uchumi upo na tabia kama ya homa za maambukizi, ni kuwa athari za kiuchumi za nchi jirani mara zote zinaakisi mustakabali wa Kiuchumi wa nchi jirani.

    Vivyo hivyo, kuimarika kiuchumi kwa nchi hiyo ndio kuimarika kwa nchi ya jirani.

    -Ukosefu wa Ajira wa nchi moja, unachangia uhamiaji kwenye nchi ya jirani ambako kuna unafuu ktk ajira ama matumaini angalau.

    -Kuimarika kwa biashara kwa nchi moja jirani kunavuta mtiririko wa biashara kutoka nchi ingine.

    -Suala la Kibenki na Kifedha la Msumbiji litaigusa Tanzania kwa namna fulani hivi, kama unavyoona pana mtiririko wa watu baina ya Tanzania na Msumbiji ktk mambo mbali mbali.

    Hivyo linalojiri Msumbiji litaakisi Tanzania kwa namna yeyote ile.

    N.K.

    UPO HAPO?

    ReplyDelete
  3. Mdau wa Kwanza juu Hapo ni kuwa Benki za Kiislamu hazitozi Riba kwenye Mikopo.

    1.Msumbiji ni nchi yenye asilimia ndogo sana ya Waislamu lakini ipo ktk Nchi za Umoja wa OIC hivyo inanufaika na Mikopo hiyo.

    2.Tanzania inakosa nafasi hiyo kwa kutojiunga na OIC hivyo kuikosa fursa hiyo muhimu.

    3.Nchi za Umoja wa Ulaya ambako Ukristo huko ndio Makao Makuu zina Benki hizi za Kiislamu na zina shirikiana na Taasisi za Kifedha za Kiislamu ambazo zimethibitika na WORLD BANK na IMF ya kuwa zina ukuzaji mkubwa kiuchumi Duniani na upenyaji wa Kifedha (Rapid Economic growth and financial sector penetration)

    ReplyDelete
  4. Shukran mdau kwa maoni yako lakin ni muhimu kujua kinachoendelea ulimwenguni na ndio maana hata kwenye taarifa ya habari kuna habari za kimataifa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...