![]() |
Mzee Alex Kombe Enzi ya Uhai Wake |
Familia ingependa kumshukuru kila mtu binafsi lakini haitaweza kufanya hivyo bali shukrani kwa wote, na hasa asante zetu kwa padre Evod Shao wa Kanisa Katoliki la St. Edwards, Baltimore; Padre Callist Nyambo wa Kanisa Katoliki la All Saints, Florida, na Wachungaji wote wa The Way of the Cross Gospel Ministries, College Park, Maryland kwa kumuhudumia kiroho marehemu akiwa mgonjwa na baada ya kufariki. Shukrani maalumu ziende kwa wahudumu wote wa Kanisa Katoliki la St. Camillus, Silver Spring, Maryland; kwa Rais wa Jumuia ya Watanzania DMV bwana Iddi Sandaly kwa msaada wake usio na kifani wa kuwezesha marehemu kusafirishwa hadi Tanzania. Shukrani pia kwa Balozi na maafisa wote wa Ubalozi wa Tanzania Marekani kwa misaada yao. Bila ya kuwasahau woote wale ambao walisaidia upande wa vyakula, vinywaji na wale waliosaidia kumhudumia wakati wa matibabu.
Mimi na familia nzima tungependa kuwakaribisha wote katika sala ya kumuombea na kumkumbuka ndugu yetu Alex ambayo itafuatiwa na chakula cha mchana saa 7 mchana (1:00 pm sharp) Jumapili Februari 17 katika kanisa la:
The Way of the Cross Gospel Ministries, 3621 Campus Drive, University of Maryland College Park, Maryland 20740.
Asante na karibuni sana,
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...