WAZIRI MKUU Mhe. Mizengo Pinda ameunda Tume maalum itakayofanya uchunguzi wa matokeo ya mtihani wa kidato cha nne ambayo yalitangazwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa Februari 18, mwaka huu.
Katika matokeo hayo yaliyotangazwa Jumatatu wiki hii, asilimia 60 ya wanafunzi waliofanya mtihani wa kidato cha nne Oktoba, 2012 walifeli.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Peniel Lyimo amesema Tume hiyo ambayo inatarajiwa kuanza kazi wakati wowote wiki ijayo inajumuisha wadau kutoka Chama cha Wamiliki wa Shule na Vyuo Binafsi (Tanzania Association of Managers and Owners of Non-Government Schools/Colleges (TAMONGSCO), Taasisi za Dini zinazotoa huduma ya elimu, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Asasi zisizo za Kiserikali (NGOs) zinazoshughulikia masuala ya elimu.
Wadau wengine watatoka Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii na Umoja wa Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania (TAHOSSA).
Amesema Serikali inawaomba wadau wa elimu, wazazi, walezi na wananchi wote kwa ujumla watoe ushirikiano kwa Tume ili iweze kufanya kazi yake kwa ufanisi.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 3021,
DAR ES SALAAM.
JUMAMOSI, FEBRUARI 23, 2013.
Naamini tume hiyo itakuwa na wadau muhimu kama vile Hakielimu na TENMET! Wamefanya tafiti nyinyi ktk sekta ya elimu na watakuwa na mchango mkubwa kwenye hili.
ReplyDeleteNa Mh. Mbatia naye pia yumo?
ReplyDeleteMheshimiwa Mfumo wa Elimu tumeuvuruga wenyewe halafu tunajiundia tume wenyewe,tunachekesha kweli.Zamani Shule zetu zilikuwa zinatoa vijana wenye bongo zinazochemka kweli kweli .Kuna mtu humu kwenye blog yetu hii aliandika pointi muhimu sana jana;kwamba Tanzania Kiongozi anaweza akaamka akasema tufanye hivi(hata kama ni kitu kibaya),hakuna anayehoji.Matokeo yake ndo haya.
ReplyDeleteMajuzi Mh.Mbatia katoa hoja ya muhimu sana kwa Taifa kuhusu Elimu,kilichotokea bungeni sote tulishuhudia.Kuna masuala hayahitaji kuchanganywa na siasa kama hili la elimu.
David V
Kaaazi ipo hapo
ReplyDeleteWazo la Lowassa limesikilizwa. Good. HAKI ELIMU WASIKOSEKANE
ReplyDelete