Padri Evaristitus Mushi

Padri Evaristitus Mushi wa KANISA la Katoliki,Parokia ya ST.Joseph,Shangani,Unguja ameuwawa leo mnamo saa moja asubuhi katika eneo la Beit-el-Ras karibu na kanisa la Katoliki.

Kwa mujibu wa taarifa iliotolewa na Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Mhe. Mohamed Aboud imeeleza kuwa kutokana na tukio hilo Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeliagiza Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi wa kina ili kuwatambua wale wote waliohusika na tukio hilo kwa ajili ya kuwachukulia hatua zinazofaa kwa mujibu wa sheria.

Mhe. Aboud amesema kuwa wakati uchunguzi huo unaendelra, Serikali inawaomba wananachi wote kuwa watulivu na kuliachia Jeshi hilo la Polisi kutekeleza wajibu wake.

Aidha Serikali imetoa mkono wa pole kwa familia na wanafamilia wa marehemu pamoja na waumini wa kanisa hilo kuwa wastahamilivu katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo.

IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Naomba kuuliza kwani nchi hii haina makachero? Serikali kila siku ni kuomba moyo ya subira na utulivu. Hao makachero wameajiriwa wanakula pesa za bure? Zanzibar ni nchi ndogo sana kweli hili lisijulikane kwa wiki hata wiki 4 basi???? hata kama si maswala ya ukristo na uislamu tuelezwe tusiachwe kigazani na kujenga mioyo ya chuki na hisia

    ReplyDelete
  2. R.I.P Mushi,
    Mungu tuepushe na haya majanga!

    ReplyDelete
  3. Serikali sasa inashindwa kazi. Haijifunzi kutokana na matukio yaliyotangulia kama yale ya yule Padri aliyepigwa risasi. Kila siku ni kuomba utulivu. Serikali lazima ielewe kuwa utulivu una mipaka yake pia. Watu watachoka kuwa watulivu mambo haya yakizidi kuendelea.

    ReplyDelete
  4. It's quite devastating, heartbreaking and intolerable. How long will Christians be reminded of our values & moral duty to remain ' humble, submissive & persevering'? Our Holy teachings say it so clear. However, states & governments are in our belief, God given authority (ies). They have a duty to ensure all it's citizens irrespective of their differences, more so religion to,peacefully enjoy this basic right of WORSHIP & FAITH! We need action before things gets to worse from this bad scenario. We are all human beings with two sides of our being, the good & the bad. Let us respect each other! Neighbor principle should prevail.

    ReplyDelete
  5. Mdau wa mwanzo suali lako kwa kiasi ni zuri lakini nadhani umeshau kuwa kila kukicha sio zanzibar tu bali tanzania nzima watu wanauliwa na serikali haifanyi lolote.

    Kifo hiki kimesikika tu kwa sababu ya wadhifa wake, lakini ndugu zetu tele wa albino kwa mfano wanauliwa kila leo na hata katika redio hairipotiwi seuze kwenye internet na kwengineko.

    watu wanauliwa kila siku na serilai haitoi kauli yeyote ile, mifano ipo tele hapa zanzibar na wala sikusudii mauaji ya kidini au siasa ni mauaji ya wizi na ugomvi wa mitaani tu.

    ReplyDelete
  6. Wauaji wanasahau kwamba Jehanamu ya milele inawangoja kama hawatatubu.Mungu si mtu aseme uongo;Wala si mwanadamu,ajute;Iwapo amesema hatalitenda?Iwapo amenena, hatalifikiliza?Hizi ni nyakati za mwisho.Chukua hatua

    ReplyDelete
  7. Jamari sasa too much!! Vita hii ipo wazi wazi Serikali isije kimya Lazima something must be done

    ReplyDelete
  8. Haya yote yasingetokea kama Watanzania tungeacha kushabikia udini!

    Kuna watu wanamchukia Rais tu kwasababu ya dini yake lkn.hakuna baya lililotokea ambalo ni kubwa na halijawahi kutokea hapa.

    Watu na magazeti hawataki kumpa ushirikiano badala yake wanabaki kumlaumu na kumchafua lakini na sisi tunasema lazma amalize mda wake!..nchi ni yetu sote hii!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...