Kama jibu kwa taarifa za kupotosha za hivi karibuni
kutoka kwa vyombo vya habari, Bodi ya fastjet ingependa kuchukua fursa hii
kutoa ufafanuzi kuhusu taarifa zisizo za kweli na za kuchafua zilizotolewa na
Don Smith wa fly540 Kenya.
Kampuni, kwa msisitizo mkubwa, inakataa madai yaliyotolewa na Don Smith
kuhusu wazo la ununuzi wa hisa ndani ya
Fly540 Kenya pamoja na madai mengine mengi yaliyofanywa kupitia vyombo vya
habari katika majuma ya hivi karibuni.
Akitoa kauli kuhusu madai ya hivi karibuni, mweyekiti wa fastjet David
Lenigas alisema:
“fastjet imenuia kufanya
biashara zake katika hali ya uwazi, isiyofichika na ya kihalali kwa ujumla wake,
kupitia itifaki zinazotakiwa. Kampuni hii haina nia ya kuendelea kukanusha
madai ya uongo kupitia vyombo vya habari lakini itachukua hatua za kisheria
kuhusu madai mengine zaidi kama hayo.”
“fastjet imemlipa Don Smith na wenzake zaidi ya Dola za Kimarekani
milioni 6 kwa ajili ya hisa zake kwenye
Fly540 na nembo nyingine za kibiashara zinazohusiana na hiyo, na sasa
kwa ari kubwa itachukua hatua kuhakikisha kuwa mikataba yake imetekelezwa.”
“Kampuni haitavumilia mikakati yoyote ya ulaghai na isiyo ya wazi. Masuala
yaliyotungwa na Don Smith nchini Kenya hayatadhuru mpango wa jumla wa fastjet
wa kuwa kampuni ya kwanza ya safari za ndege kwa Afrika nzima yenye gharama za
chini”
“Nafasi ya kampuni nchini Kenya,
ambayo ni sehemu ndogo tu ya upanuaji
wetu, imeshawekwa salama kupitia mkataba wa makubaliano na Jetlink uliotangazwa
wiki iliyopita. Tunahisi kuwa Jetlink, ambayo tayari ina ithibati ya IOSA, ni mshirika mzuri zaidi wa fastjet
ukizingatia viwango vyetu vya usalama na uaminikaji. Baada ya kufanya mapitio
ya kina, tulitambua kuwa Jetlink itaweza kuipa fastjet msingi wa kudumu wa
kuanzia kwa sababu ya uwezo wake mkubwa wa miundombinu na ithibati yake ya
kiwango cha kutoa huduma na kusimamia ndege nyingi kubwa za kisasa”
“Afrika ina karibu asilimia 4% ya abiria wa safari za anga duniani
lakini kwa bahati mbaya kwa sasa ndiyo yenye asilimia 25% ya ajali za ndege
duniani. Dhima yetu ya kuleta usafiri salama kwa watu wa Afrika inahitaji
viwango vya juu na uzingatiaji wa kila mara kuhakikisha kuwa haya
yanatekelezwa.”
Mkurugenzi mkuu wa fastjet Ed Winter aliongeza:
“Pale ambapo madeni ya
kihistoria yaliyoendelea kuongezwa na Don Smith na Fly540 yamekuja kuwa wazi
baada ya umiliki, fastjet inafanya kazi kwa karibu na wadai wake ili kufikia
muafaka unaoridhisha kwa pande zote zinazohusika. Hatukubaliani na viwango vya
gharama ambavyo vimekuwa vikitamkwa katika vyombo vya habari hivi karibuni, na
pale viwango vinavyodaiwa vinapotambulika, msivichukulie kwa umakini kuhusiana
na biashara kwa ujumla. Masuala haya yaliyojitenga hayadhuru utendaji wa siku
hadi siku wa fastjet au utendaji wowote wetu katika Angola au Ghana ambao
wanasafirisha chini ya nembo nyingine ya Afrika ya Fly540”
“fastjet itachukua hatua
kurejesha madeni haya ambayo hayawekwi wazi na mengine yoyote yaliyomo chini ya
waranti zilizotolewa na Don Smith na wenzake katika makubaliano yao ya kuuza
hisa zao ndani ya Fly 540 Kenya na kuiuzia fastjet mwezi Juni mwaka jana”
Timu ya menejimenti ya fastjet inabaki kuwa ya wanaharakati wakubwa wa
maendeleo ya kampuni, kujenga mafanikio yake Tanzania na ukuaji kuelekea kuweka
demokrasia katika usafiri wa anga wa Afrika na kuwa shirika la kwanza la usafiri wa anga barani Africa lenye
gharama za chini
“Kwa sasa, tunaendelea kufanya
kazi na mamlaka zinazohusika katika mataifa mengine Afrika kupanua mtandao wa
fastjet”
Dona Smith anatumiwa!
ReplyDeleteKwa kuwa Fastjet ni Mwekezaji wa Sekta ya usafiri anayezingatia kujikita kwenye maeneo ambayo Ukuzaji wa Kiuchumi umepatikana (Economic Growth) kutokana na kuonekana kwa mali hasa madini ya Nishati kama Gas,Oil and Uranium, WANAOMTUMIA huyo Don Smith ni zile nchi zilizokataa FASTJEST WASIJIKITE kuogopa Ushindani au kukwepa kuzidiwa Kibiashara!
-ANGOLA, wana OIL and Uranium
-GHANA, wana Oil and Gas
-TANZANIA, tuna Gas ,Uranium pia huenda na Oil.
WENYEWE WADAU MTAJUA NI NCHI GANI HIZO AMBAZO ZINAYO MASHIRIKA YAKE AMBAYO WANATAKA YAWE VINARA KATIKA ENEO LETU NA AFRIKA KWA UJUMLA.
-Kama mnavyoona ujio wa hawa jamaa FASTJET wa gharama za chini, huwezi kuamini umewaondoa wakongwe waliodumu nchini kwa miaka 82 BRITISH AIRWAYS!
BAHATI MBAYA NI KUWA NDEGE AMESHARUKA UKIMKAMATA UTAMPUNYUA MANYOYA YA MKIA,,,HUKU UKIMWONA YULEEEE MAEONDOKA!
MABILIONI YA GAS AND OIL YAKIMIMINIKA UTAZUIA WIPI UWEKEZAJI HUO?
Jamaa hapo juu umechemsha ndg yangu.Kwani FastJ ni mpinzani wa BA hata kama BA wameacha kuja nchini ni kabla ya ujio wa Fj.Kama BA awe mshindani wa FJ jee KLM,AEROFLOT,KQ watakuwa washindani wa nani kwanza FJ inaoperate locally hawana safari za nje kwa taarifa yako!Hao FJ hata kwa PW hawaenei
ReplyDeleteMdau wa pili anony wa Mon Feb 11, 01:50:00 pm 2013
ReplyDeleteINAONYESHA HUFUATILII VYOMBO VYA HABARI NA TAARIFA ZA DUNIA!
...Wewe unafikiri Fastjet wamekuja kubakia watoa huduma za ndani na nchi ya Tanzania pekee?
...Kwa taarifa yako Kenya Fastjest wamebaniwa na Kenya Airways ilikuwa waendeshe hadi huko hadi sasa bado wanapigania kuingia ktk soko hilo ingawa bado wanakwamishwa.
...Nia ya Fastjet ni kupanua wigo wa biashara hadi INTERNATIONAL ROUTES NA KUONGEZA IDADI YA NDEGE NA UKUBWA WA NDEGE KULINGANA NA UPANUKAJI!!!
UPO HAPO?