MAMLAKA YA USIMAMIZI WA BANDARI TANZANIA

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) inapenda kuwatangazia Wateja na Watumiaji wote wa Bandari kwamba imeanzisha Kitengo Maalum cha Huduma kwa Wateja kitakachopokea malalamiko, kero, taarifa, maoni, ushauri juu ya huduma mbalimbali zinazotolewa na Mamlaka.

Kuanzishwa kwa Kitengo hiki ni moja kati ya Mikakati ya Mamlaka ya kuboresha huduma zake na kuondoa kero kwa Wateja na Watumiaji wa Bandari.
Kwa huduma ya haraka tafadhali piga namba zifuatazo;
0754 292998
0756 849868
0788 888801
0789 334398
Namba hizi pia zinapatikana kwenye mtandao wa TPA www.tanzaniaports.com
MENEJIMENTI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Mnabidi mbadilike siyo msubori Mwakyembe awaongoze kila kitu . TAtizo lililopo Tanzania n kuwa watu wanafanya kazi kwa mazoea ili mradi pesa imeingia siku imepita basi . Hawana motivation ya kuongeza tija

    ReplyDelete
  2. Huduma kwa Wateja! Kitengo muhimu kisichotiliwa maanani na bahati mbaya hata walionacho wengine ni hovyo kabisa. Kwa mfano makampuni mengi ya simu ukipiga simu ya huduma kwa mteja sio wote wanaotoa huduma hiyo wanaelekea kujua "bidhaa muhimu za kampuni yao" Nenda kwenye benki za walalahoi, utakuta unataka kuuliza kitu tu wahusika wanakungalia kama uchafu! YEYOTE ANAEFANYA KAZI KWENYE KITENGO CHA AINA HII TAFADHALI BADILIKENI, WAPYA ZINGATIENI TAALUMA ZENU.

    sesophy

    ReplyDelete
  3. Mbona namba za Zantel, Tigo na TTCL hakuna??

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...