Jaji Mkuu wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Mahakama, Mhe. Mohamed Chande Othman akisaini kitabu cha wageni  alipotembelea ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Mwanza asubuhi hii. Kushoto  ni Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania ambaye pia ni Mjumbe wa Tume, Mhe. Fakih Jundu. Mhe. Jaji Mkuu pamoja na ujumbe alioambatana nao wapo mkoani humo kwa ajili ya kuongea na wajumbe wa Kamati ya Maadili ya Mkoa huo lengo likiwa ni Kujenga mahusiano mazuri ya kiutendaji na Kamati Hilo. 
  Katibu wa Tume ya Utumishi  wa Mahakama, Bw. Hussein Kattanga akiongea na wajumbe wa Kamati ya Maadili ya Mkoa wa Mwanza katika mkutano unaofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu mkoani Mwanza hivi sasa. Mbali na kuwa Katibu wa Tume, Bw. Kattanga pia ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Maadili ya mkoa wa Mwanza wakiwa Katika mkutano na Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Mahakama Picha na mdau Mary Gwera, Mahakama ya Tanzania

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...