Pichani katikati ni Mwenyekiti wa kamati ya Tuzo za wanawake wenye Mafanikio Tanzania bi. Sadaka Gandi akifafanua jambo mbele ya Wanahabari (hawapo pichani) kuhusiana na mchakato mzima wa tuzo hizo, kulia Raisi wa tuzo hizo bi. Irene Kiwia na kushoto ni bi. Esther Shayo mratibu.
Pichani kulia ni Raisi wa tuzo hizo Irene Kiwia akielezea jambo mbele ya Wanahabari (hawapo pichani),kuhusiana na tuzo hizo za Wanawake wenye Mafanikio Tanzania msimu wa 2013, zilizopangwa kufanyika katika siku ya wanawake duniani tarehe 8 Mwezi Machi mwaka huu.
Taasisi ya Tanzania Women of
Achievement (TWAA) leo imezindua Tuzo za Wanawake wenye Mafanikio Tanzania msimu
wa 2013 zilizopangwa kufanyika katika siku ya wanawake duniani tarehe 8 Mwezi Machi
mwaka huu. Tuzo hizi ambazo hufanyika kila
baada ya miaka miwili zilizinduliwa mwaka 2009 kwa heshima ya wanawake katika sekta
mbalimbali nchini kote ambao kupitia kazi zao wamechangia kwa kiasi kikubwa sana
kuleta maendeleo ya jamii zao kwa njia moja au nyingine.
"TWAA inataka kutambua wanawake,
waishio Tanzania ambao kupitia kazi zao wameweza kupata mafanikio makubwa si tu
kibinafsi bali wametumia nafasi zao kuleta maendeleo na mabadiliko ya kimsingi kwenye
jamii zinazowazunguka." Alisema Mkurugenzi mkuu wa TWA Bi. Irene Kiwia. "Tuzo
hizi mbazo sasa ziko katika msimu wake wa 3 zinatoa fursa nzuri ya kutambua na kupongeza
wanawake ambao wamechangia sana kwenye kubadilisha na kuboresha sura ya
Tanzania. Kwa wanawake wengi hii itakuwa mara ya kwanza mafanikio na michango yao imetunukiwa na hili ni jambo la
kufariji na kuridhisha sana.”
Vipengele vya tuzo za mwaka huu
ni Sanaa na Utamaduni, Biashara na Ujasiriamali, Habari na Mawasiliano,
Michezo, Professional (Kazi), Elimu, Afya, Ustawi wa Jamii, Sayansi naTeknolojia,
Sekta ya Umma, Kilimo na Mshiriko Mdogo.
Bi SadakaGandi, mwenyekiti wa
kamati ya TWAA alitoa wito kuwa "tunawasihi mashirika, vyama, wanawake na wanaume
kote Tanzania kuteuawa na wake wenye mafanikio katika makundi haya na kuonyesha
mchango wao katika uwezeshaji wa wanawake. Kuna maelfu ya wanawake wastahili watuzo
hizi huko nje ambao ni mawakala wamabadiliko katika jamii zao.
Tunataka kuimba mapambio ya mashujaa
hawa na kuhamasisha mamilioni ya wanawake wengine wa Tanzania kuiga mifano na kupata
msukumo wa kuleta mabadiliko. Kamati ilipokea fomu nyingi sana za washiriki miaka
ya nyuma na hivyo basi tunategemea ushiriki mzuri zaidi mwaka huu. "
Kamati ya TWAA inawajumuisha Bi
Mary Rusimbi – Mwanaharakati na Mwanzilishi wa Programu yaMtandao wa Jinsia
Tanzania, Jaji Joaquine De Mello – Kamishna waTume ya Hakiza Binadamu naUtawala
Bora, Dk Marcelina Chijoriga-Mkurugenzi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,
Bi.Ludovicka Tarimo–Mtaalamu wa Jinsia kutoka USAID, Bwana. Innocent Mungy-Mkurugenzi
wa Mawasiliano kutoka Mamlakaya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA), Sadaka
Gandi – Mwanasaikolojia na mfanyakazi za Jamii, Irene Kiwia – Mwanzilishi na Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni ya mahusiano ya jamii Frontline Porter Novelli.
Huko nyuma tuzo hizi zilidhaminiwana
Baileys, Delloite, NBC, Home Shopping Center, TCRA, Songas, WatuwaMarekani,
DTP, UN DPG Gender Group, UNFPA, UNESCO, TBL, Multichoice, African Life Assurance,
Barrick, Twiga Cement, Vodacom, Farm Equip, RBP, Clouds FM na Frontline Porter
Novelli.
Esther Shayo tumepotezana miaka mingi naomba contact zako please
ReplyDeleteNaomba sana mtunuku wanawake mashujaa ambao hawajatumia NGOs na wafanyakazi wake au pesa za wafadhili kujifadhili umaarufu.
ReplyDeleteHawa ndiyo wastahili. Na wapo ila hatuwafikii wala hatuwadhamini. Tuache kujitukuza kwa mgongo wa wengine.
Mshindi halali azingatiwe:
ReplyDeleteVIGEZO MDAU WA JUU ULIYVYOTOA NI MUHIMU:
1.UTENDAJI WA MUHUSIKA.
2.ATHARI YA UTENDAJI WAKE KWA MAENDELEO NA USTAWI WA NCHI.
3.UADILIFU KWA MATUMIZI YA FEDHA KAMA ALIPATA FEDHA ZA WAHISANI.
4.SIO LAZIMA AWEPO KWENYE ASASI KUBWA AU MAARUFU.
5.PAWEKWE MFUMO HURU UTAKAO HUSISHA MCHAKATO MPANA ZAIDI ILI KUMPATA MSHINDI KIHALALI NA BILA MIPANGO.