Ndugu zangu,
Kwenye vyombo vya habari juma hili, moja ya habari kubwa iliyochagizwa sana ni kitendo ch viongozi wa Chadema kutoa kwa wananchi, pale viwanja vya Mwembe Yanga, namba za simu ya mkononi ya Spika Anne Makinda na Naibu wake, Job Ndugai.
Kimsingi, viongozi wa Chadema waliofanya kitendo kile walikosea. Yawezekana kabisa kuwa madai ya Chadema kuwa Spika na Naibu wake wanaisiginya demokrasia ndani ya Bunge ni madai ya msingi, lakini, namna waliyochagua ya kufikisha madai hayo kwa wananchi haikuwa sahihi.
Ni kawaida, kwa baadhi ya viongozi wawapo majukwaani kusukumwa na jazba wanapoongea, lakini, hutokea pia, kauli za viongozi hao wawapo majukwaani zinapokosa umakini, kupelekea madhara makubwa.
Katika kazi yangu ya uandishi, nimeshawahi kutofautiana na Spika Makinda, si mara moja, mara ya mwisho ni kwenye hoja yake kuwa wabunge wawapo Dodoma wana maisha magumu, hivyo, kuhalalisha ongezeko la posho zao.
Lakini bado naamini, Spika Makinda ni binadamu kama wengine. Naye ni mzazi na mwenye familia yake inayomzunguka. Kitendo cha viongozi wa Chadema kutoa hadharani namba za Spika Makinda , za simu ya mkononi, kwenye umati wa watu wenye kero mbali mbali , na unaoambiwa kuwa watumie namba hizo kumpigia na kutuma ujumbe mfupi kwa Spika Makinda, bila shaka, kwa akili ya kawaida tu, kitapelekea Spika Makinda na mwenzake Ndugai kuwa na wakati mgumu. Maana, watu wale watakuwa wamechochewa.
Ikumbukwe, kijinsia Anne Makinda anaweza kuwa mhanga zaidi wa kupigiwa na kutumiwa jumbe za simu zenye hata kumdhalilisha kijinsia. Katika dunia hii kuna baadhi ya wanaume wenye maradhi ya kisaikolojia yenye kuhusihanisha masuala ya ngono.
Kwamba kuna wanaume ambao hutafuta namba za simu za wanawake tu. Ikifika usiku, hupiga bila kuongea, wanachosubiri ni kusikia sauti ya mwananmke ikijibu na kisha kumaliza haja zao. Hao ni wagonjwa.
Hivyo, unapotoa hadharani namba ya simu ya mkononi ya mwanamke, basi, unaweza pia kumuingiza katika hatari ya kupokea simu za ajabu ajabu kutoka kwa baadhi ya wanaume. Wako wapi wanaharakati wa haki za kibinadamu na kijinsia wa kumtetea Anne Makinda?
Tunajifunza nini?
Viongozi wa kisiasa wawe makini wawapo majukwaani. Mambo mengine wanaweza kuyafanya na hata kuyaongea majukwaani wakidhani kuwa wameyafanya kwa dhamira njema, lakini, matokeo yake yaweza kuwa na madhara makubwa.
Ingewezekana kabisa kwa viongozi wale wa Chadema kutoa hadharani namba maalum ya simu ya mkononi, ili watu wapige na watume jumbe fupi kwenye simu hiyo. Kisha, viongozi hao wangeweza kurekodi sauti zenye maoni ya watu yasiyo na matusi wala namna yoyote ya kudhalilisha. Wangekusanya pia jumbe hizo fupi kwa kuhariri zile zenye matusi na zenye kudhalilisha. Baadae zingewakilishwa kwa Spika Makinda na Naibu wake.
Ingewezekana pia kukusanya saini kutoka kwa wananchi zenye kuonyesha kuwa wanawapinga Spika na Naibu wake, na kwamba wanawashinikiza wang'oke. Hizi zote ni njia za kistaarabu kabisa za kuwasilisha malalamiko.
Tukishindwa kuonyesha mfano sasa, wa kufuata taratibu za kistaarabu, hatari yake tunaizoesha jamii kutumia njia za ovyo na nyingine zenye maovu katika kuwasilisha malalamiko yao. Na kesho huenda Spika wa Bunge atatoka Chadema.
Itakuwaje basi, pale kesho viongozi wa CCM nao watasimama Mwembe Yanga mbele ya wananchi wenye kero zao, na kutaja namba za simu ya mkononi za Spika wa Bunge linaloongozwa na Chadema?!
Hapana, hivi tunavyoenenda sivyo inavyopaswa twende. Na hakuna aliyekamilika. Tujisahihishe.a
Maggid Mjengwa,
Mjengwa una busara sana, KUDOS
ReplyDeleteWkt mwingine tuweke mapenzi yetu kisiasa na vyama vyetu kando tutumie kichwa kufikiria. Siku 1 wataweka namba ya mama Salma, ya Waziri mkuu au makamu, rais na wengine tunaopashwa kuwaheshimu watukanwe na wavutabangi na wahuni. Taifa la Nyerere linaenda wapi jamani? Taifa ambalo watu wake wana heshima zaidi huku ughaibuni kulinganishwa na mataifa yote ya Afrika, naam, tujisahihishe, hatujachelewa. Waandishi mna wajibu mkubwa ktk hili.
Chadema wakumbuke hata wao wakiongoza nchi wanayoyafundisha sasa yanaweza kuwageuka
Mjengwa, mie sina chama na huwa nakuaminia sana lakini naona kwa ili umekosea. Mhe. Spika na Naibu ni viongozi wa Umma,yaani maisha yako machoni kwa watu. Kwanza namba zao zinatakiwa ziwe wazi kwa sababu kazi zao ni za watu. Na kama wametukanwa wangechukulia kama changamoto, mbona Kiongozi wetu Kikwete na viongozi wengine wanatukanwa kila mala?!! Na hamna kelele. Unapoamua kufanya kazi fulani, mfano kiongozi wa watu basi uwe tayari kusikiliza kelele zao.
ReplyDeleteTaarifa zisizo rasmi zinasema wamepokea jumbe nyingi sana za matusi ya nguoni na kupigiwa simu nyingi za vitisho... yetu macho.
ReplyDeleteMaggid, hapa ni jino kwa jino. Hapa ni mambo ya siasa tu. Wewe hapo unatetea, lakini unaweza kukuta kesho chadema na makinda wako kwenye pozi la nguvu.
ReplyDeleteWewe tuwekee tu sisi maoni yetu kwenye blog yako, hao achana nao
Nimekupenda Mjengwa huo ndio uungwana! Kusema ukweli. Kwa hili ukweli viongozi wetu hamkutenda sawa.
ReplyDeleteKwa muungwana anapokosea huomba radhi kwa Umma kwani Makinda ni spika wa Bunge la Tanzania hivyo Watanzania hawakutendewa haki kabisa.
kwa maoni yangu mie sioni kama kuna tatizo lolote tatizo la spika wetu hana msimamo anaendeshwa na wabunge wa ccm hiyo hipo wazi.Mie nashindwa kuelewa yeye ni mtu wa mwisho kutoa maamuzi lakini nashindwa kwanini anakuwa anapelekwa sana na viongozi wa ccm.Inaonekana wazi kabisa huwa anapendelea ningependa kushauri kwenye uchaguzi ujao kuwepo na viti sawa kwa kila chama.Hii italeta changamoto bungeni.Tukifanya hivyo bac maendeleo yatakuja
ReplyDeleteKAKA MJENGWA, NAUNGANA NA WEWE KWAMBA KWA KWELI KUTOA NAMBA YA MTU YA SIMU HASA MOBILE HADHARANI SI VIZURI KWASABABU KAMA ULIZOZITAJA.
ReplyDeleteILA WAO CHADEMA WALIKUWA NA NIA NZURI KWAMBA WAMPIGIE ANNE MAKINDA NA NDUGAI NAKUWASHAWISHI WAJIUZULU YEYE NA NAIBU WAKE. LAKINI SASA DISADVANTAGE INAKUJA KWA WATU AMBAO WANASHIDA KI SAIKOLOGJIA KAMA ULIVOSEMA KWAMBA WATAMPIGIA BILA KUWA NA SABABU YA KIMSINGI WALIOITAKA CHADEMA.
ILA KWELI ANNE MAKINDA NA NDUGAI NAO WALIFANYA JAMBO BAYA BUNGENI KUKATALIA ISSUES ZA MSINGI TENA ZINAZOHUSU WANANCHI WA TANZANIA ZA WABUNGE KWA KUIPENDELEA CCM
KWAHIYO MIMI NASEMA CHADEMA NIA YAO ILKUWA NZURI KWAMBA WAMSHAWISHI AJIUZULU NA NAIBU WAKE LAKINI KWAVILE BINADAMU WAPO WENYE BUSARA NA WASIO NA BUSARA HAPO NDIPO AMBAPO WASIO NA BUSARA WANAWEZA KUTUMIA NAMBA HIYO VIBAYA LAKINI WENYE BUSARA WATAPIGA NA KUMWAMBIA ALIVYOFANYA SI VYEMA NA AJIUZULU.
UNAJUWA KAKA UKISEMA ANNE NAYE NI BINADAMU HAPO UNAKOSEA, ANNE AMECHAGULIWA NA JK KWA MAKUSUDI ATETEEE CCM NA NDIO MAANA ALITOLEWA MZEE WETU ALIYEKUWA SPIKA SASA UKISEMA NAYE NI BINADAMU UNAKOSEA YEYE YUPO PALE KWA NIABA YA CCM SI VINGINEVYO
USIMTETEE KWAMBA ANAFANYA KAMA BINADAMU ANAFANYA KAMA ALIVYOTUMWA NA JK NA CCM
ASANTE ILA USHAURI WAKO UNA ASILIMIA KAMA 40 NI SAWA.
CHADEMA WALIKUWA NA NIA NZURI KWAMBA APIGIWE KUAMBIWA UKWELI SI MATUSI NA SMS ZA KIJINGA
Bongo tutakuwa wajinga mpaka lini. Wabunge wote hizo simu zao zinalipwa na walipa kodi. Huku marekani namba za simu za congress members na senators ziko wazi kwa watu na ni wajibu wa watu kuwapigia na kutoa maoini yao licha ya kuwa kuna uwezekano wa kutofautiana katika hoja. Ndugu yangu Mjengwa nilitaraji kuwa wewe ni moja ya waandishi/mwanahabari stadi lakini umeonyesha ufinyu wa wako wa katika taxation without representation. Vilevile cha kushangaza bongo ni kwamba kama mtu kakutukana mpeleke mahakamani na mfungulie kesi ya madai. Kitendo cha polisi kushikia kidedea hii issue kama vile ni kosa la jinai ni upumbafu mtupu. Nakubaliana kama ni vitisho kw aspika na naibu wake lakini kama ni ujumbe wa kutokubaliana na uamuzi wao hilo sio tatizo na hizo simu ni mali za walipa kodi na lazime zitumike kuwakosoa na kutoa maoni yao. Kitendo vilevile cha naibu spika kupiga marufuku live coverage ya vikao vya bunge hapo tunarudi palepale invasion of freedom of information. Hivi lini bongo tutaelimika na kuacha mabo ya kila mtu kuwa mahakimu na kupiga marufuku kila kitu.
ReplyDeleteMaggid nini tena?Makala zako huwa ni nzuri sana lakini hii kama vile umeiandika kwa jazba/haraka sana .Kuna sehemu umetoka kwenye mistari.
ReplyDeleteDavid V
Weka maoni ya watu Michuzi kuliko kuendeleza ajenda za CCM. watu wana haki ya kuwapigia simu wawakilishi nwao bungeni kwanza simu zenyewe sio zao binafsi zinalipiwa na bunge na hiyo ni fedha ya walipa kodi. Kama mtu katukanwa polisi haina kazi ya kumshitaki hilo ni jukumu la alietukanwa kwenda mahakamani na kufungulia kesi ya madai. Kumuongezea spika ulinzi hiyo ni kuongeza matumizi ya walipa kodi tayari ana ulinzi tosha.
ReplyDeleteNadhani Maggid we ndiye unayekosea. Unapokuwa Spika au waziri Unakuwa ni Mtu wa wananchi. Lazima address yako na Simu yako ijulikane kwa wananchi maana unafanya kazi kwa niaba ya wananchi na si kwa niaba yako binafsi au kwa niaba ya marafiki zako wanaokukingia kifua! Sasa spika asipotoa namba Yale kwa wananchi atapataje maoni Yao? Au huyu spika hajali maoni ya wananchi? Kama hayajali basi kazi imemshinda!
ReplyDeletehajaonewa chochote.....chadema wako right
ReplyDeleteWewe majidi mjengwa,,tunashukuru kwamba umeandika sawa asante!! sasa wewe unasema watu wamemutukana anayetukanwa si anakuwa kakosea? au wewe unakubaliana na alichokifanya sipika na mwenzake naibu? kumbe hata wewe unakubaliana na wizi unaofanywa na viongozi hao!! hicho ndio wanachokitarajia kwa matendo yao mkuu wanastahili kutukanwa zaidi hadi kipigo kabisa kwani hawawajibiki vilivyo.watu wanapiga vita ufisadi ww unakubaliana nao tu.
ReplyDeleteSiungani na wewe kwa hili hata chembe... kwenye demokrasia ya ukweli hakuna kuficha mawasiliano kati ya viongozi na Raia... kama kweli Spika amekasirishwa na namba yake kuanikwa ni kwa nini asichukue hatua za kisheria kwa Chadema? Kwa nchi tajiri zilizoendelea Viongozi wanatukanwa na wananchi kila siku.Obama aliitwa muongo wakati akihutibia bunge tena na mmbunge.. Tanzania ni nnchi masikini duniani, Panapo umasikini na utawala mmbovu ni wazi kuwa wananchi hawawezi kufurahishwa na viongozi wa serikali. Hebu tufikirie ni nini kimepelekea Chadema kumshtaki Makinda kwa umma? Huyu mama analivuruga bunge letu tukufu kwa kuliendesha kibabe na upendeleo.. Inakuaje hoja binafsi za upinzani zitupwe lakini za CCM zipite? Halafu rufani zote za hoja binafsi amezikalia kwa miaka... WaTanzania wanaona na kusikia kinachoendelea bungeni.. hivi tunafikiri yanayotokea Uarabuni hayawezi tokea Tanzania? Watu wakichoka ndiyo matokeo yake ni haya.. Matusi ni udhaifu tunakoelekea ni kuondoa udhalimu wa CCM kwa nguvu ya umma.Huwezi kutawala watu kwa vitisho na ukandamizaji!! Sasa nauliza ni kwa nini asitukanwe kwa anayoyafanya bungeni? Suala ni haki siyo CCM au Chadema.. yeyote atakaendesha bunge kibabe asivumiliwe.
ReplyDeletebasi na watwekee namba za sim za mbowe na salaa maana nasi tuna kero nao hivyo hivyo. Mimi sina chama lakini nikiwasikia hawa wanaongea sipendi wanaongea kigomvigomvi hivi. Na Tundu Lissu anahitaji kwenda shule ya diplomasia kabla ya kupewa uwaziri wa sheria 215.
ReplyDelete