Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Rais Mwai Kibaki wa Kenya wakiongozwa na Meya wa Kinondoni Mstahiki Yusuph Mwenda kutembea hatua chache kabla ya kuzindua rasmi jina la Barabara ya Mwai Kibaki linalochukua nafasi ya jiba la barabara ya Old Bagamoyo leo kwenye makutano ya barabara ya Bagamoyo na Rashid Kawawa na iliyokuwa Old Bagamoyo leo Februari 21, 2013. Barabara hiyo, yenye urefu wa kilomita 10.1 inaanzia makutano ya barabara za Rashid Kawawa na Bagamoyo hadi njia panda ya kwenda Africana karibu na uwanja wa kulenga shabaha wa JWTZ Mbezi Beach
Rais Mwai Kibaki wa Kenya akifunua pazia, akishuhudiwa na mwenyeji wake Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli na Meya wa Kinondoni Mstahiki Yusuph Mwenda akizindua rasmi jina la Barabara ya Mwai Kibaki linalochukua nafasi ya jiba la barabara ya Old Bagamoyo leo kwenye makutano ya barabara ya Bagamoyo na Rashid Kawawa na iliyokuwa Old Bagamoyo leo Februari 21, 2013.
![]() |
Vifijo na nderemo baada ya uzinduzi huo. |
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mgeni wake Rais Mwai Kibaki wa Kenya muda mfupi kabla ya kufanya mazungumzo rasmi(official talks)Ikulu jijini Dar es Salaam jana jioni.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwatambulisha kwa rais Mwai Kibaki baadhi ya Mawaziri waliohudhuria dhifa ya kitaifa ikulu jinni Dar es Salaam
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akigonga glasi na mgeni wake Rais Mwai Kibaki wa Kenya wakati wa dhifa ya kitaifa aliyoiandaa Ikulu kwa heshima ya Rais Kibaki aliyeko nchini kwa ziara yaka ya mwisho ya kiserikali.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwatambulisha kwa rais Mwai Kibaki baadhi ya Mawaziri waliohudhuria dhifa ya kitaifa ikulu jinni Dar es Salaam
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akigonga glasi na mgeni wake Rais Mwai Kibaki wa Kenya wakati wa dhifa ya kitaifa aliyoiandaa Ikulu kwa heshima ya Rais Kibaki aliyeko nchini kwa ziara yaka ya mwisho ya kiserikali.
tafuteni na barabara nyingine ipewe jina la michuzi road au mjomba kipanga road kwa tanzania kila kitu kinawezekana.
ReplyDeleteHawa waliyotajwa hapo juu, wanastahili kabisaaa. wamewezesha mabadiliko ndani ya jamii yetu kwa kiasi kikubwa sanaaaa. Ila ila ila huwa tunadhani viongozi ni wale waliyoshika nyadhfa za juu tuuuuu!
ReplyDeleteBARABARA NYINGINE MDAU HAPA JUU NADHANI ITAITWA SADAM HUSSEN ROAD.BONGO HILI LAWEZEKANA.
ReplyDeleteSerikali acheni kiburi tuambieni basi kwanini hiyo barabara imepewa jina la Mwai Kibaki.Lazima kuna sababu za msingi.Wananchi tunahitaji kufahamu.Usiri wa nini???
ReplyDeleteDavid V
MMEANZA KUUZA NCHI KITARATIBU EEH
ReplyDeleteWatanzania lazima tubadilike. Huku kusifia watu wakati ni wajibu wao ulishapitwa na wakati. Huyo jamaa anasema barabara ziitwe Mchuzi au Kipanga!! Je anashangaa nini barabara kuitwa Kibaki? Au ulitaka umfurahishe Mchuzi ili aweke comments zako? Huku kujipendekeza ndo kumeifanya nchi hii ikafika hapa ilipo. Nchi haiwezi kuendelea kama tunakuwa na mambo yale yale ya kizamani. Hao uliowataja wameifanyia nini nchi yetu? Tena hawa ndo wa kwanza kujipendekeza. TUTAFIKA????????
ReplyDeleteMasuala ya uhusiano wa kimataifa ni fani yenye wajuzi na wasomi waliobobea. Nadhani wanaohoji wajiulize kwanza kuna utaratibu ambao hutumika kuwatunuku kumbukumbu baadhi ya watu. Mtaa wa samora uliitwa independence, wakati marehemu samora machel alipofanya ziara rasmi katika Jiji la Dar alipewa uraia wa jiji na kuibadilisha jina barabra ya independence kuwa samora avenue kwa heshima ya Rais huyo. Lakini barabara kuweka kumbukumbu za kihistoria hapa duniani si jambo jipya, hapa Dar kuna sekou toure ilipatiwa jina kufuatia ziara ya rais toure. Kuna Kenyatta, Haile Selasie, Kaunda, Sokoine, Bibi Titi, Rajab Diwani, Max Mbwana, etc. Utaratibu huu upo srhemu nyingi dunianiza kuhifadhi historia kwa njia hii.
ReplyDeletemh hakuna mwanamke hata mmoja hapo
ReplyDeleteHapana hiyo barabara ilipewa jina la mbunge mmoja aliyekuwa wa kinondoni aliitwa Bryceson (Derek Noel Bryceson) aliwahi pia kuwa waziri wa kilimo enzi za mwalimu, semeni tu kama mmeamua kumchinjia baharini maana cc tulioishi Dar kitambo hayo tunayakumbuka.
ReplyDeleteWanao ishi kwa vitendo, tunawafahamu hata mkawa kejeli. Wanao jitukuza bila stahili kwa sababu wameshika mpini tunawafahamu. Sasa hilo libaki ktk uchambuzi wa kila mmoja wetu na kutafakari uhalali huu wa kienziana!
ReplyDeleteMimi nadhani huu uamuzi wa kuiita hii Barabara Mwai Kibaki si wa busara. Kwanza huwezi kukuta Nairobi au Kenya nzima jina la Nyerere rd, Kikwete rd au Kawawa rd. Pili, hili jina la Bagamoyo lina utaifa zaidi na historia,tena Old Bagamoyo rd hata kizazi kijacho kitakuja kufahamu kumbe kulikuwa na barabara ya zamani ya Bagamoyo na iko nyingine ya sasa new Bagamoyo rd, kihistoria ina mafunzo mengi. Tatu, inapendeza zaidi kwa ufahamu wa uelekeo kama barabara itabeba jina la kule inakoelekea hasa kwa mtu mgeni, mf. Pugu rd inaelekea Pugu, Kilwa rd inaelekea Kilwa, Morogoro rd inaelekea Morogoro n.k sasa kufuta majina kama haya ni kupoteza maana na kutowarahisishia uelewa wa uelekeo wasafiri hususan wageni. Mambo ya TZ mtu akiamka asubuhi anaamua tu vile alivyoota au kufikiria na hakuna mtu wa kumsahihisha na ndio inakuwa imetoka hivyo. Ninachosema hapa ni kwamba hakukuwa na haja ya kufuta jina la Old Bagamoyo rd na kuipa jina la Mwai Kibaki. Kuna maeneo mengi ya kuyabdili na kuyapa majina ya watu mfano majengo n.k
ReplyDeleteHII INAONYESHA KWAMBA TANZANIA HAKUNA DEMOKRASI,KWA SABABU MTU UNAAMUA MWENYEWE NITAFANYA JAMBO FULANI.KWANINI WANANCHI TUSIPEWE NAFASI YA KUPIGA KURA KUONA NI WANGAPI WANAPENDA BARABARA KUITWA MWAI KIBAKI?HIVI WATU KWA NINI WASITOE HICHO KIBAO USIKU?MDAU DALSTON.
ReplyDeleteWewe Anony wa Fri Feb 22, 01:14:00 pm 2013,umeandika comment yenye hisia kali.Imenitouch,sikufiria kitu kama hicho
ReplyDeleteMdau wa Fri Feb 22, 01:14 00 pm 2013, Mdau wa Fri Feb 22, 07:32:00 pm 2013
ReplyDelete...Kwa Mentality ya Wakenya muulizeni Mdau John Mashaka anawaelewa vizuri sana, hawa jamaa zetu majirani zetu wanatudharau sana ! na ndio maana huwezi kukuta Kikwete Road au Nyerere Rd huko kwao!
Ingawa ile dharau yao si lolote si chochote kwa kuwa mambo mengi sana tunawafunika, mfano shida yao na Machafuko na Kuunda Serikali yako sisi ndio Raisi wetu alifanya kazi ya ziada mpaka wakapatana.
Angalieni walikuwepo Mhe.Raisi Mstaafu Ben Mkapa, Mhe. Raisi JK ndani ya nyumba Koffi Annan, na Mzee Desmond Tutu ndio mambo yaka wa mambo Kenya baadabya machafuko ikapata Serikali!
Sawa baada ya yeye kupewa Barabara jina lake hapa TZ na sisi tunasubiri akifika kwao atoe jina barabara moja kuiita JK Road ili na sisi tumpe heshima zake!
ReplyDeleteJamani Ustaarabu una Chuo?
ReplyDeleteHawa Wakenya hawana Daraja ya ustaarabu kama huo wa kutoa majina ya wengine kwao!
Wajameni mkumbuke ya kuwa Uungwana ni vitendo!
ReplyDeleteUnapoona mtu anampa Heshima mwingine yule mtoaji heshima ni mtu muungwana sana.
Yeye tumempa heshima hapa TZ na sisi hata akitupa au asitiupe si lazima.
Huwezi kufanya uungwana kwa kujikakamua.