Makamu Mwenyekiti wa Kamati Maadili ya Utangazaji nchini, Walter Bgoya (katikati) akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam ukumbi wa habari Maelezo.
Na Thehabari.com
KAMATI ya Maadili ya Utangazaji nchini imevifungia vituo viwili vya radio pamoja na kukipiga faini kituo cha Clouds FM kutokana na kukiuka maadili ya utangazaji.
Vituo hivyo vya redio ambavyo vyote kwa pamoja vimefungiwa kutorusha matangazo yake kuanzia leo kwa miezi sita ni pamoja na Imani FM cha Dar es Salaam na Kwa-Neema FM kilichopo mkoani Mwanza.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Walter Bgoya alisema Kituo cha Clouds FM kimetakiwa kufuta kipindi
chake cha Jicho la Ng'ombe mara moja pamoja na kulipa faini ya sh. milioni 5.
Akifafanua zaidi Makamu Mwenyekiti huyo alisema vituo vya Imani FM na Kwa-Neema vimefungiwa kwa kosa la kufanya kazi zao kwa uchochezi jambo ambalo ni kinyume cha maadili ya tasnia ya utangazaji. Kituo cha Clouds FM kimetakiwa kutoanzisha kipindi kingine kinacho fanana na Jicho la Ng'ombe.
Kituo cha Imani FM kinadaiwa kufanya uchochezi kwa wananchi juu ya suala la sensa ya watu na makazi huku kile cha Kwa-Neema kufanya uchochezi juu ya mgogoro wa
uchinjaji wanyama kwa Waislamu na Wakristu mkoani Geita.
Hata hivyo Kamati ya Maadili imeweka mlango wazi kwa vituo hivyo kukata rufaa endapo havikuridhika na adhabu vilivyo pewa kutokana na makosa vinao daiwa
kufanya.
Kamati Imevitaka vyombo vyote vya habari kufanya kazi kwa kuzingatia Kanuni Sheria na maadili ya tasnia hiyo ili kuepuka kuzua migogoro kwa wananchi ambao wamekuwa
wakiviamini vituo hivyo.
Hata hivyo mara baada ya ujumbe wa kamati hiyo kumaliza kusoma adhabu hizo kwa waandishi wa habari haukuruhusu maswali kwa waandishi wa habari, hivyo waandishi kubaki wameduwaa.
Hii habari ni ya ajabu kidogo! Nilidhani kama kituo cha Radio/TV kikikiuka sheria na taratibu za leseni husika adhabu yake ni kunyangwanywa leseni na sio kufungiwa miezi 6 kama wachezaji wa mpira wa miguu. Inatia shaka jinsi hizi kanuni, sheria na taratibu zinavyotungwa. Nadahani umefika wakati wa kuwa na Kamati huru (isiyo chini ya mamlaka ya serikali) ili isimamie udhibiti na ufuatajwi wa sheria na kanuni zinanazosimamia vyombo vya habari!
ReplyDeletepengine wangeweka wazi pia sheria ipi inatumika,hii ingesaidia pia kujua adhabu zinatolewa vipi kwa makosa gani na pia ni muda gani unatolewa tangu kosa lifanywe mpaka adhabu,ama labda kama kuna uchunguzi nk.Mfano hivi vituo vimeadhibiwa kwa pamoja wakati suala la sensa ni la toka mwaka jana,na hili la geita ni la juzi tu,au kilikuwa kinasubiriwa kituo kingine kifanye makosa ili vifungiwa pamoja ili kujiridhisha kwamba adhabu ni halali?
ReplyDeleteWasiishie kufunga tu vituo, watafute na wachochozi wengine mitaani kama wale watu wanaoweka mikutano ya hadhara ya dini. Mikutano hii badala ya kuelezea dini yao huwa inaelezea taofauti ya dini nyingine na kuendelea kukashfu imani nyingine. Pia wasifunge tu wafanya utafiti wajue kwa nini wanafanya hivyo inawezekana kukawa na sababu nyuma ya pazia. Kufunga tu haitasaidia. Watu hawa watatafuta njia nyingine ya uchochezi
ReplyDeletekutangaza dini na mikutano ya dini ni hiyari ya mtu kusikiliza au kuacha, kwani imani ya dini fulani huwa inakufuru sana na hata kukaribia mbingu kupasuka na kuanguka, lakini watanzania tunavumiliana, anayeshawushika na dini ya mwenzake ni ruhsa kujiunga. hivyo kufungiwa tv fulani isiwe wao na watu jamii yao ni wabaya laa! ni Mtihai tu wa Muumba wa nchi. tujitadi na SUBIRA NA KUSHUKURU NEEMA YA AMANI YETU
ReplyDeleteTANZANIA NI YETU SOTE AU YUPO MWENYE HATI MILIKI YA NCHI HII, HAYUPO BALI NI SERIKALI TULIOIWEKA MADARAKANI. SO ISHU ZA SERIKALI HAZIWEZI KUBINAFSISHWA NGUDUZANGUNI TUWE WAELEWA. TUKUBALI KUWA MAAMUZI YA SERIKALI NI MAAMUZI YETU WATANZANIA SOTE
ReplyDeleteMI NAMPONGEZA SANA KWA HATUA HII. TENA WAKIRUDIA INAPASWA WAFUTWE KABISA KWENYE MAMBO YA UTANGAZAJI
ReplyDeleteJICHO LA NGOMBE KIMEFUNGWA KWA SABABU GANI??????????
ReplyDeletePOLENI MLIO FUNGIWA ILA MJIFUNZE, WATANGAZAJI WENGI HUWA WANAJISAHAU SANA, HASA KATIKA KIPINDI HIKI CHA MICHAKATO YA KISIASA, CLOUND NA JICHO LA NG'OMBE, WATANGAZAJI WAMEKUWA MHAKIMU WA WATENDAJI WA SERIKALI, HUWA SIWAPENDI KABISA, WAMEKUWA WAKISHUSHA HATA NYADHIFA ZA WATU, HAWANA HESHMA HATA KIDOGO, NADHANI WAMENUNULIWA NA WANASIASA FULNI, HAWAFAI KUWA WATANGAZAJI, REDIO INASIKIKA ENEO KUBWA LAKINI WANAITUMIA VIBAYA SANA. KAZI YAO NI KUCHOKOZA MADA NA KUPOKEA MAONI YA WASIKILIZAJI SI KUCHANGIA MADA, WANGIKUWA WANATOKA NJE YA STUDIO KISHA WAPIGE SIMU ILI WACHANGIE KAMA WASIKILIZAJI WENGINE. UONGOZI NADHANI UTALIFANYIA KAZI HILI, NA AJUE WATANGAZAJI WATAKUWA WAMENUNULIWA ILI KUICHAFUA SERIKALI.
ReplyDelete