Na Heka Paul na Shakila Galus_MAELEZO –Dar
Wakaguzi
wa Ndani wa Serikali wametakiwa kubadilika na kuacha kufanya kazi zao
za kila siku kwa kufuata mazoea ili kuongeza ufanisi katika kuwatumikia
wananchi.
Kauli
hiyo imetolewa leo na Msaidizi wa Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali
Amin Mcharo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya viwango vya kimataifa vya
ukaguzi wa ndani kanda ya mashariki.
Alisema
kuwa wengi hawapendi mabadiliko na kusema kuwa ni vema kwa watu wa aina
hiyo wakaangalia uwezekano wa kutafuta kazi au taalum nyingine ili
kutochafua kazi ya ukaguzi.
Mcharo
alisema kuwa Ukaguzi wa Ndani ni taalum inayohitaji kwenda na
mabadiliko kwa kuzingatia mabadiliko katika miongozo ya kimataifa na
inayozingatia uadilifu.
Aliongeza kuwa Tanzania haiwezi kubaki kama
kisiwa na hivyo ni vema wakaguzi wake wa ndani wakawa chachu ya
utekelezaji wa utendaji wa kazi unaozingatia viwango vya kimataifa vya
ukaguzi wa ndani.
Aidha
Mcharo alisema kuwa Ofisi ya Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali
imejipanga kufuatilia kwa karibu utendaji wa Wakaguzi wa Ndani ili
kubaini kama utendaji wao unaozingatia maadili ya kazi na ikibainika
wanakwenda kinyume na maadili haitasita kuishauri Mamlaka husika
kuwaondoa katika nafasi zao.
Itawezekana kweli, Tanzania hii kila mtu anataka kulipua kazi na kutafuta rushw ili akalewe ama kulisha nyumba ndogo.
ReplyDelete