A standing ovation as President Dr Jakaya Mrisho Kikwete arrives for the opening the African Conference on the Strategic Importance of Intellectual Property Policies to Foster Innovation, Value Creation and Competitiveness at the Hyatt Regency Kilimanjaro hotel in Dar es salaam today March 12, 2013.
opening the African Conference on the Strategic Importance of Intellectual Property Policies to Foster Innovation, Value Creation and Competitiveness at the Hyatt Regency Kilimanjaro hotel in Dar es salaam today March 12, 2013.
Dr. Francis Gurry, Director General of the World Intellectual Property Organization (WIPO), speaks at the opening of the African Conference on the Strategic Importance of Intellectual Property Policies to Foster Innovation, Value Creation and Competitiveness at the Hyatt Regency Kilimanjaro hotel in Dar es salaam today March 12, 2013.
Hon. Dr. Abdallah Kigoda, Minister for Industry and Trade, invites President Kikwete to address the gathering
President Dr Jakaya Mrisho Kikwete opens the African Conference on the Strategic Importance of Intellectual Property Policies to Foster Innovation, Value Creation and Competitiveness at the Hyatt Regency Kilimanjaro hotel in Dar es salaam today March 12, 2013.
A cross section of participants to the African Conference on the Strategic Importance of Intellectual Property Policies to Foster Innovation, Value Creation and Competitiveness at the Hyatt Regency Kilimanjaro hotel in Dar es salaam today March 12, 2013.For full story and more photos CLICK HERE

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Hongera Mhe. Raisi Dr. Jakaya M. Kikwete, Hongera Mhe. Waziri Dr.Abdallah O.Kigoda, Hongera Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!

    Kweli Tumethubutu, Tumeweza na Tumesonga mbele!!!

    Hatua hii sio mchezo hawa Wazito WIPO wa haki Miliki kuja kufanya Kikao hapa ina maana tumefanya vizuri.

    Maendeleo ya jamii yanachangiwa na umiliki wa haki miliki ktk Sekta ya Biashara, Uzalishaji na Rasilimali ambapo Tekinolojia ndio mwendshaji wa hayo yaani 'SCIENCE AND TECHNOLOGY TO BE DRIVING FORCE TO ACHIEVE SUSTAINABLE ECONOMIC DEVELOPMENT'

    Zipo nchi nyingi ktk Dunia ambapo WIPO wangekwenda kufanya Mkutanao licha ya kuwa sisi kama wanachama wa Shirikisho hilo tunayo haki, isipoikuwa pana kilicho wakuna hawa kuweka Kikao hapa Tanzania.

    Ina maana kazi, shughuli pevu imefanyika sio bure bure, kwa kuwa hawa jamaa WIPO hawafanyi Vikao vya Matumizi bila Tija.

    Ili kuwahakikishia kuwa tumeweza natoa mifano kwa nchi 2 za jirani yetu zilivyofanya vema licha ya nchi zingine za Duniani, na kwa nini WIPO wachague Tanzania?.

    1.Rwanda-imezengumzwa kuwa ni nchi iliyotumia Sayansi na Tekinolojia kuakisi maendeleo makubwa yaliyo patikana baada ya Vita na Mauaji ya Kimbari 1994 hadi kufikia mwaka 2010 wameweza kuongoza kwa ICT (Information and Computer Technology) ktk Afrika ya Mashariki na ktk dunia wapo nchi za juu zaidi zilizo fanya vizuri, Ripoti hii ipo ktk UNDP.

    2.Kenya-imekuwa juu kwa Mradi wao mkubwa wa Konza City au Silicon Savannah na pia wametumia Sayansi na Tekinolojia kuakisi maendeleo yao na kuwa nchi inayowika mfano Uvumbuzi wa M-PESA kwa Kampuni ya Safaricom, pia wamepiga hatua ktk Utafiti wa kilimo cha Kitekinolojia kwa miradi kama GMO (Genetically Modified Seeds) na pia Utafiti wa wanyama wa mifugo, hivyo kuongeza uzalishaji wa chakula kwa kuwa mazao ya GMO (i)yanastahimili Ukame,(ii) yanastahimili Magonjwa na (iii)yanaongeza Mavuno na sasa Kenya ina ardhi ndogo ya Kilimo lakini sasa haina njaa na mfumuko wa bei ya chakula umeshuka, Infation rate WORLDBANK report ni 3.9% kwa mwezi Dec 2012 hadi Jan 2103 kipindi kabla ya Uchaguzi.

    Mchango mkubwa kuifanikishia Kenya umetolewa na mwendeshaji Prof.Calestous Juma ambaye ni Mkenya wa Harvard University Marekani, Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Sayansi na Tekinolojia kwa nchi changa.

    3.BAO TULILOPIGA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA:
    Ili kuakisi maendeleo kwa kasi kupitia Sayansi na Tekinolojia kunatakiwa vitu kama TICTBB(Tanzania Information and Computer Technology Broadband Backbone)-as vehicle to achieve, hivyo Mkonga wa Mawasilino Tanzania utawezeisha Ufanisi na maendeleo ya ksai zaidi ktk sekta hizi:

    *e-Government
    *e-Administration, (kama CAG)
    *e-Business and Trade
    *e-Health
    *e-Education
    *e-Justice
    *e-Production
    *e-Finance
    *e-Politics
    *e-Communication
    *e-Society

    Hivyo Tanzania ni miongoni mwa nchi zitakazokuwa na kasi kubwa ya maendeleo ktk jamii yake kwa ujio na matumizi ya mkonga huo wa mawasiliano, kama tulivyoona sasa TTCL itamiliki hisa kwa 100% kuliko ilivyokuwa kabla na kiuutumia Mkonga kwa ufanisi zaidi, Makampuni ya Mitandao ya simu yamefungua Mfuko ili kuwa na uwezo wa kufikisha huduma za Mawasilinao hata sehemu zisizo na mvuto wa kiniashara, Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu ya Serikali imekuwa ya kwanza CAG kujiungana Mkonga wa Taifa(TICTBB).

    Hivyo kwa mifano hiyo miwili ya ufanisi wa wenzetu hapo juu, ilistahili WIPO wafanye Mkutano Nairobi-Kenya ama Kigali-Rwanda, lakini kwa kuwa sisi tumefunika KWA BAO LETU hapo juu imebidi wafanyie Dar-Tanzania.

    Mungu Ibariki Afrika, Mungu Ibariki Tanzania na watu wake!

    ReplyDelete
  2. Tumethubutu tumeweza na tukasonga mbele na Richmond! Watanzania hatujasahau.

    ReplyDelete
  3. Anony wa kwanza umechemsha sana. Inasikitisha kuona kuwa hujui hata madhara ya GMO hasa siku za usoni. Pole sana. Sijui nikwambie au nikuache tu. Ngoja nikuache tu.

    ReplyDelete
  4. Mbonagharama za simu na mtandao bado ziko juu?

    ReplyDelete
  5. Mdau wa 3 anony wa Wed Mar 13, 05:20:00 am 2013

    ...Anony wa kwanza umechemsha sana.Inasikitisha kuona hujui hata madhara ya GMO.

    ...SASA WEWE UNAFIKIRI IDADI YA WAKAZI WA DUNIA INAYOFIKIA 7 BILIONI HUKU IKIWA INAONGEZEKA KWA KASI YA AJABU WAKATI UZALISHAJI WA CHAKULA UKISHUKA DUNIANI ITALISHWA CHAKULA LA NANI?

    ...JE, WEWE UNAFIKIRI UTAISHI KARNE NGAPI?, HUTAKUFA?,

    ...JE, UNA UHAKIKA GANI KAMA MADAWA YA VIWANDANI UNAYOMEZA HAYANA MADHARA?, KWA NINI USITUMIE MITI SHAMBA KWA TAHADHARI?

    ...JE, HAPO ZAMANI KABLA ULISHAJUA YA KUWA DAWA YA ASPIRIN ULIYOKUWA UKIITEGEMEA MIAKA NENDA MIAKA RUDI ILIYOPIGWA MARUFUKU KWA MATUMIZI INA MADHARA?

    ...JE, HUJUI YA KUWA MAISHA NI LAZIMA KU-TAKE RISK NA KU-SUCRIFICE?

    HEBU ELEZA WEWE BINAFSI UNAFIKIRI DUNIA ITAWALISHA VIPI IDADI YA WAKAZI WA DUNIA INAYOKUWA KWA KASI HUKU UZALISHAJI WA CHAKULA DUNIANI UKIWA HUENDANI NA KASI YA ONGEKO LA IDADI YA WATU DUNIANI?

    +++++++++++++++++++++++++++++++++++===================================

    WEWE ANONY WA Wed Mar 13, 05:20:00 am 2013 ,WEWE NDIO ULIYECHEMSHA!!!

    ReplyDelete
  6. Anony wa Pili Tue Mar 12, 09:08:00 pm 2013

    ...Tumethubutu, tumeweza tunasonga mbele, na Richmond waTanzania hatusahau...

    Wewe umesoma?, akili unayo?

    Je kuna uhusiano gani kati ya Kashfa (Richamond) iliyopita na hatua iliyopigwa ktk (Sayansi na Tekinolojia-Kitu kama TICTBB)?

    ReplyDelete
  7. Mdau wa nne simu ziko bei juu, ni kuwa kinachofanyika hapo sasa ni wizi kwa kuwa Gharama wanazo zibeba Makampuni ya Mitandao kwa sasa ni chini sana!

    ReplyDelete
  8. Anony wa tatu 3 wa Wed Mar 13, 05:20:00 am 2013

    Wewe hujui ya kuwa Maendeleo hayakosi changamoto?

    Mfano kabla ya Matumizi ya simu za Mikononi kasi ya Uhalifu na mtindo wa Uhalifu vilikuwa chini saana, isipokuwa baada ya Maendeleo ya sekta ya Mawasiliano Uhalifu nao umepanda Daraja na kuwa wa Kiwango cha Maendeleo yaliyopo kwa kuwa nao Wahalifu wanatumia Tekinolojia ya Mawasiliano kuliko watu wa kawaida.

    Wamagharibi wanasema ''There is no development withought challenge''

    Hivyo usitegemee kuongeza Uzalishaji wa chakula kwa miujiza bila kutumia Tekinolojia ngalau yenye madhara ya upande wapili, hata kama itakuwa kiwango cha madhara kipo chini lakini huwezi kupiga hatua bila changamoto zozote.

    Kama suala ni GMO kuwa na madhara ya upande wa pili, itatumika michakato ya angalau ya kupunguza madhara hayo kwa kuboresha ugunduzi huo.

    Hivyo mtoa Maoni wa Kwanza hajachemsha bali wewe mwenye Mkosoaji ndio uliyechemsha!

    ReplyDelete
  9. Mdau wa Tatu hapa tunalinganisha ufanisi na hatulinganishi madhara yanayopatikana!

    Je, unataka kutuhakikishia ugali unaokula ukipitisha kiwango cha shibe huwezi kuvimbiwa?

    Je, ingawa kuvimbiwa kuna fanana na shibe nako sio madhara?


    Think twice !, be innovative !

    ReplyDelete
  10. Mtoa Maoni wa tatu (3) anony wa Wed Mar 13, 05:20:00 am 2013


    '''''Anony wa kwanza umechemsha sana. Inasikitisha kuona kuwa hujui hata madhara ya GMO hasa siku za usoni. Pole sana. Sijui nikwambie au nikuache tu. Ngoja nikuache tu.'''''

    HILI NDILO TATIZO LETU KUBWA WATANZANIA,

    SASA KAMA UNA MAWAZO YA FAIDA NA MAONI KWA NINI UMWACHE TU MTOA MAONI WA KWANZA?

    NA WEWE TOA MAONI ULIELEZE JAMVI LA WASOMAJI HUMU HAYO MADHARA !!!

    KWA KUWA HILI NI JAMVI LA JAMII LIBENEKE HAPA HAZUNGUMZWI MTU ILA YANAJADILIWA MAMBO KWA FAIDA YA WOTE!

    Unakuta mtu anadai Mtaala wa Elimu mbovu, ndio anakataliwa maoni yake mwanzoni, inatokea mambo kweli yanaharibika nchini (MATOKEO MABAYA MITIHANI KIDATO CHA NNE) anaitwa kushiriki kutatua tatizo yeye tena kushiriki anakataa!

    Mmeona Watanzania tulivyo?

    ReplyDelete
  11. Mtoa Maoni wa 3 elewa ya kuwa mnakwenda Mstari wa mbele Vitani mkiwa Kikosi Kamili labda Batalioni moja watu 1,000 Vita inapigwa mnamaliza mkiwa mmeshinda huku mkiwa Askari 100 tu !

    Hivyo mnapopigana na adui anayetisha kama 'njaa' (au upungufu wa chakula) usitegemee Kikosi chenu cha Kijeshi kitabaki kuwa na idadi kamili ya askari wengi watakufa vitani.

    Hivyo madhara ya hiyo GMO unatakiwa wewe ufanye Research kutatua tatizo hili, kwa kuwa unayafahamu, kwa kuwa wengine tayari wamesha fanya kazi ya kutatua tatizo la njaa.

    Lakini lengo ni kumshinda adui na kushinda vita, huku marekebosho mengine yakifanywa baadaya ushindi!

    Upo hapo?

    ReplyDelete
  12. Mdau wa 2 usilete Siasa za Chadema hapa ,

    ...ohhh Richmond , hatutasahau Tanzania.

    Kinacho jadiliwa jamvini humu ni maendeleo na ukuzaji na sio Siasa!

    ReplyDelete
  13. Mdau wa 3 wa GMO anony wa Wed Mar 13, 05:20:00 am 2013

    Kwa suala la hayo madhara ya GMO kama utamwacha Madu wa Kwanza humu jamvini ni vema ukawasiliana na Mwendeshaji wa Mipango hiyo ya Kilimo hicho cha Kitekinolojia huko kenya Prof.Calestous Juma.

    Hiyo hata huko kwao Kenya amesha pata upinzani mkubwa sana kwa Wana harakati mbali mbali huko huko Kenya kuhusiana na Miradi yake na uenezi wake Kitaaluma hasa kwenye suala hilo la GMO pamoja na kama wewe unaweza kuchangia hizo harakati za Wakenya kukosoa.

    http://www.hks.harvard.edu/about/faculty-staff-directory/calestous-juma

    e-mail:calestous_juma@harvard.edu

    Hivyo Mdau toa hoja zako za madhara ya hizo GMO halafu akikujibu tushukie Jamvini ili tufadikie sote kwa pamoja.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...