Habari na picha na Dixon Busagaga,
Globu ya Jamii Moshi 

 WANARIADHA kutoka mkoa wa Arusha wamefanya vizuri katika mashindano ya mbio za Taifa za Nyika zilizofanyika jana mjini Moshi kwa kupata ushindi wa jumla baada ya wanariadha wake kushika nafasi za kwanza na pili katika mbio za kiliometa 12 ,nane na sita . 
 Mashindano hayo ambayo awali yalikuwa yafanyike mkoani Morogoro yaliowakutanisha wanariadha zaidi ya 100 kutoka mikoa mbalimbali nchini na kufanyika katika viwanja vya klabu ya gofu ya mjini Moshi baada ya kusimama kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita. 
 Katika mbio za utangulizi za kilomita 6 wanawake , Anjeline Irene 21:19;57, Selina Amosi 21:31:86, Fadhila Salum wote kutoka Arusha mbio za km 8 wanawake Jaeldine Sakilu (JWTZ-Arusha) 27:00:34, Zakia Mrisho (Arusha) 27:24:58 na Catherine Lange (Manyara) 28:12:91. 
Katika upande wa wanaume km 8, Dotto Ikangaa 23:53:95 JWTZ-Arusha, Joseph Theophil Mbulu 23:56:41 na Mohammed Ally 24:13:54 JWTZ- Arusha huku mbio za km 12 wanaume akichukua Dickson Marwa 36:34:52 kutoka Holili-Kilimanjaro. 
 Awali akizungumza na waandishi wa habari mapema kabla ya kuanza kwa mbio hizo, Rais wa Shirikisho la Riadha Taifa, (RT), Anthony Mtaka amesema kuwa madhumuni ya mbio hizo, ni kuandaa kikosi kitakacholiwakilisha Taifa katika mbio za Nyika za dunia zitakazofanyika Machi 24, nchini Poland pamoja na kuibua vipaji vya riadha nchini. 
Mtaka amesema kuwa sababu za kuhamishia mbio hizo mkoani Kilimanjaro ni kutokana na mdhamini waliyempta hapo awali kujiondoa na hivyo kuwalazimisha kutafuta mdhamini mwengine ambapo alisema, Executive Solution walisaidia sana. 
Nao baadhi ya wanariadha walioshiriki mbio hizo, Jackline Juni, aliyeshinda mbio za km 8 wanawake na Dickson Marwa, aliyeshinda mbio za km 12 wanaume, walisema wako tayari kuiwakilisha nchi katika mbio za Poland lakini walisisitiza umuhimu wa kuwepo kwa maandalizi na ushirikiano kutoka kwa wadau wa Riadha. 
 Jumla ya wakimbiaji wapatao 100 kutoka katika mikoa ya Mwanza, Arusha, Manyara, Singida, Mara, Zanzibar, mbeya, Dar es salaam na kilimanjaro walichuana jana katika mbio za Nyika za taifa zilizofanyika katika uwanja wa gofu wa Moshi Club ulioko katika Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro ambapo mshindi wa kwanza alipokea zawadi ya Sh. 60,0000.
 Mwandishi wa habari wa shirika la utangaza TBC Sauda Shimbo akifyatua bastola kuanzisha mbio za kiliometa 8 kwa wananwake wakati wa mbio za nyika zilizo fanyika mjini Moshi .
 Wanariadha wa mbio za kilometa 12 wakianza mbio hizo .
 Mwanariadha Banuelia Bryton Mrashani wa klabu ya Holili mwenye nguo nyeusi akichuana na mwenzakeambaye jina lake halikufahamika mara moja wakati wa mbio za nyika zilizofanyika mjini Moshi.
 Rais wa shirikisho la riadha Tanzania ,Anthony Mtaka (Shoto )akiteta jambo na mgeni rasmi wa mbio za Nyika za taifa ambaye pia ni mkuu wa chuo cha polisi Moshi , Afande Matanga Mbushi.
 Washiriki wa mbio za kilimeta 8 kwa upande wa wanawake wakijiandaa ,kabla ya kuanza kwa mbio hizo za nyika zilizofanyika katika viwanja vya Gofu mjini Moshi.

 Rais wa shirikisho la soka Tanzania Anthon Mtaka akizungumza na wanahabari wakati wa mbio za nyika zilizofanyika mjini Moshi.
Mbio za nyika 
Mshindi wa mbio za kilometa 12 kwa wavulana Dixon Marwa wa klabu ya Holili akimaliza mbio hizo kwa nafasi ya kwanza baada ya kutumia dakika 36 na sekunde 34 huku akimuacha mbali mshindani wake Damiani Foka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Huyu Mtaka ni wa Shirikisho la Soka au la Riadha? Maana naona katambulishwa mara mbili mbili kwa vyeo vyote viwili.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...