ASKARI MMOJA WA USALAMA BARABARANI AMBAYE AMETAMBULIKA WA JINA MOJA LA WP 2492 CPL ELIKIZA,AMEGONGWA NA GARI AINA YA LAND ROVER DISCOVERY YA RANGI NYEUSI MCHANA WA LEO MAENEO YA BAMAGA,KIJITONYAMA JIJINI DAR ES SALAAM NA KUPELEKEA KUPOTEZA MAISHA PAPO HAPO,BAADA YA GARI HILO AMBALO LILICHOMEKEA KWA NYUMA MSAFARA WA RAIS.

GARI HILO LILITOKOMEA BAADA YA KUSABABISHA AJALI HIYO,NA DEREVA WAKE ANASAKWA.

GLOBU YA JAMII INAENDELEA KUFUATILIA TUKIO HILO NA TUTAENDELEA KUJULISHANA HAPO BAADAE.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. RIP PC Ezekile,kweli na foleni zote za dar huyo mtuhumiwa anawezaje kutokomea kirahisi hivyo?hapo sasa serikali inapaswa kuwa na data base ya magari yote sio TRA tu,wanatakiwa kuwa na link toka TRA kwenda polisi na taasisi nyingine husika lakini sisi wepesi wa kuiga kuvaa na simu na ipad mambo muhimu ya maisha yetu hakuna kitu,sasa wahusika macho na akili zitumike.

    ReplyDelete
  2. rip polisi, ila kwa kweli hii hali ya kusimamisha gari ambalo lipo speed 200 haiingii akilini, polisi mkiona hivyo ni bora mpigie radio call ili polisi aliyeko mbele alifkuzie na pikipiki. nafikiri kwa speed kali namna hiyo kufunga break ghafla kungeweza kumsababishia dereva ajali maana saa nyingine polisi mmekuwa mkisababisha ajali za namna hii, mnavizia magari yapo kwenye speed halafu mnasimamisha ghafla haya ndiyo matokeo yake,wafe abiria au liwalo na liwe.

    ReplyDelete
  3. RIP PW, na pole nyingi kwa wafiwa na polisi wote Tanzania. Ila ikumbukwe kuwa polisi nyie pia ni binadamu na hivyo msijisahau kuwa ni binadamu na gari ni chombo kilichotengenezwa na binadamu, gari ipo speed kali eti kwa kuwa wewe ni polisi bila kutumia hesabu za haraka haraka kugundua speed ya ile gari na uwezekano wa usimamaji wake wewe unataka yule binadamu na sio chombo kisimame utakavyo wewe. Mimi pia iliwahi kunitokea mataa ya kamata polisi mmoja alinisimamisha ghafla nikiwa kwenye speed wakati green lights inatumika ila kwa kweli mpaka polisi mwenzake alimkosoa alimwambia umekosea kusimamisha hili gari lingeweza kusababisha madhara makubwa ni vema kupima speed ya gari kabla ya kusimamisha ghafla.

    Lakini nawapa hongera polisi wengine wapo makini sana katika uongozaji wa magari hawa nahakika form four walipata A,B u C ya hesabu.

    ReplyDelete
  4. Tukio hili la kusikitisha limekwisha tokea na tunaomba Mungu amlaze marehemu mahali pema na awape nguvu na faraja wapendwa wake wote.

    Ila napenda kusisitiza suala la nini kifanyike ili madereva watii sheria za barabarani katika miji mikuu. Hili tatizo limekuwa sugu sana. Madereva wanakiuka sheria sana. Wale wa daladala ndio kabisa wako juu ya sheria. Msongamano wa magari barabarani ni tatizo ila pia linazidishwa na wale wanaotanua. Naomba mijadala ifanyike kwa kutumia vyombo vya habari kama vile kipindi cha malumbano ya hoja ITV, watu watoe maoni yao. Pili, jopo la jeshi la polisi na wanasheria waketi pamoja ili kutunga sheria kali ya adhabu kwa wale wanaokiuka sheria za barabarani. Narudia sheria kali.

    Mapendekezo yangu ni kwanza jeshi la FFU lihusishwe kikamilifu, pili adhabu ya viboko on the spot kwa yule anayevunja sheria, tatu kwa wale wanaotanua, akishapewa kiboko anawekwa pembeni; asubiri for a minimum of 3 hours kabla ya kurusiwa kuondoka. Askari wawe wanapangiwa zamu za guard za kuwalinda madereva waliosimamishwa. Kwa mfano mtu akikamatwa anatanua saa moja usiku, anawekwa pembeni hadi saa nne usiku ndio anaruhusiwa kuondoka na ameshapata kiboko. Tafadhali Bwana Issa naomba uwasilishe pendekezo langu hilo. Pia katika mijadala, wananchi wata highlight ni barabara zipi zinakabiliwa na tatizo hili sugu.

    Matatizo haya yasingekuwepo, Masikini Elikiza tungekuwa naye bado. Fikiria ni maumivu gani familia yake inapata muda huu, kuondokewa na mpendwa wao, mtu waliyemtegemea, ni uchungu wa kifo chenyewe. RIP Afande Elikiza

    ReplyDelete
  5. Watanzania tumepinda. Naona wachangiaji wanajaribu kumlaumu marehemu ambaye alikuwa natimiza wajibu wake wa kuzuia gari kufuata msafara. Tuna tabia ya kufuata msafara ili kuepuka foleni na tumekwishaweka akilini mwetu kuwa ni sawa tu. Si sawa. Kwa mawazo haya wataendelea kugongwa traffic wengi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...