Na Mroki Mroki-Father Kidevu Blog-DSM
Wawakilishi wa Tanzania katika Kombe la Shirikisho Afrika, AZAM FC, wamerejea jijini Dar es Salaam leo asubuhi na kupokelewa kwa shangwe na mashabiki na wapenzi wa timu hiyo katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere.
Azam waliwasili kwa mafungu kwa ndege ya Kenya Airways ambapo baadhi ya wachezaji wakiwapo wanaoichezea Taifa Stars kubaki Naorobi ispokuwa Mcha.
Azam ambao msimu huu wapo nafasi ya pili katika Ligi Kuu ya Tanzania bara walikuwa Nchini Liberia kuchuana na timu ya Barrack Young Controllers (BYC) ambapo Azam walishinda 2-1 katika mchezo huo wa kwanza wa Raundi ya Pili ya michuano hiyo uliofanyika kwenye Uwanja wa Antonette Tubman Monrovia, Liberia.
Azam sasa itahitaji hata sare tu ili kusonga mbele, raundi ya Tatu na ya mwisho ya mchujo kabla ya hatua ya makundi.
Pichani ni baadhi ya wachezaji hao walipowasili uwanjani hapo.
Baadhi ya mashabiki na wapenzi wa timu ya Azam FC wakicheza ngoma kwa furaha wakati wa mapokezi ya timu hiyo leo asubuhi.
SIMBA, YANGA ZILILIPENDWA... hivi ndivyo shabiki huyu wa Azam FC alivyoandika jezi yake na akitoa salamu kwa Watani hao wa jadi katika soka nchini.
Wachezaji wa Azam FC wakipanda basi lao
karibuni sana azam
ReplyDeletejamani narudia kusema kwa msisitizo nawewe ankali usibane hii
hiyo milango ya airport haipendezi kugeuzwa matangazo ya biashara jamani ni aibu kubwa
uwanja wa ndege tokea lini milango ukajazwa matangazo kwenye jengo husika la uwanja ?
matangazo yatafutie sehemu zake lakini sio milango ya kutokea au kuingilia
mnatuaibisha sana watanzania tunaoishi huku ughaibuni kuona kuwa uwanja wa ndege wa kimataifa una matangazo ya voda mpaka kwenye milango
ankali chonde chonde nimekoma naomba unihurumie japo hii moja maana unanibania mwaka mzima
very true, yanga simba zilipendwa.. na ndio zinazofanya soka ya tanzania inazidi kutokuwa na mvuto, tunataka kuona soka ya tz inarudi kama enzi zile za miaka ya themanini mpaka early ninety's.. hongereni azam.
ReplyDelete