Wakati maandalizi ya Fainali za Taifa za kumpata Miss Utalii Tanzania 2012/13 yakiwa yanaendelea kwa kasi kubwa, Bodi ya Utalii Tanzania itaendesha Semina Maalum ya Mafunzo ya Utalii kwa washiriki wote walioko kambini Ikondolo Lodge Kibamba wakijiandaa na Fainali za Taifa zitakazo fanyika Mwishoni mwa wiki ijayo Jijini Dae es salaam. 

Akithibitisha taarifa hizo kwa waandishi wa Habari Raisi wa Kamati ya Mashindano hayo Erasto G. Chipungahelo alisema kuwa Semina hiyo maalum itakayo endeshwa na Bodi yaUtalii Tanzania itafanyika katika Ukumbi wa Bodi ya Utalii uliyopo katika ofisi za Bodi ya Utalii jengo la IPS Dar es salaam siku ya Alhamisi Tarehe 7.03.2013 kuanzia saa Tatu asubuhi na kuwashirikisha zaidi ya Warembo 40 wakiwakirisha Mikoa yote ya Tanzania Bara , Kanda maalum za Vyuo vikuu na Zanzibar. 

 Watoa mada wakuu katika semina hiyo, itakuwa ni wataalam walio bobea katika secta ya utalii na masoko ya utalii kutoka Bodi ya Taifa ya Utalii(Tanzania Tourist Board). Kwa niaba na kamati ya Miss Utalii Tanzania, Ninatoa shukurani za pekee kwa Serikali na Bodi nzima ya Utalii kwa kuendesha semina hii muhimu kwa washiriki wa Fainali za Taifa za Miss Utalii Tanzania ambapo washindi wa kwanza mpaka wa Tano watawakirisha Tanzania katika mashindano mbalimbali ya utalii ya Dunia. Yakiwemo ya Miss Tourism World, International Miss Tourism World, Miss Tourism United Nation World , Miss Tourism university World na Miss Heritage World yatakayo fanyika katika nchi mbalimbali kuanzia mwezi wa nne mwaka huu. 

 Hii ni fursa  pekee kwa washiriki na washindi watakaopatikana katika fainali za Taifa kuweza kujua na kujifunza juu ya utalii Tanzania, mbinu na mikakati ya kutangaza vivutio vya kitalii kitaifa na kimataifa, hivyo kutusaidia kutimiza ndoto na malengo yetu ya miaka mitano ya kutwaa Mataji matatu ya Dunia mwaka 2013. 

 Maandalizi katika kambi ya warembo yanaendelea vizuri , ushindani ni mkubwa ari na dhamira ya kila Mrembo kulinda hadhi na Heshima ya Mkoa wake kwa kutwaa taji la Taifa ni kubwa.

Chipungahelo aliongeza kwamba, ili kuthibitisha hayo, anaomba watanzania wote wakazi wa Dar es salaam na Mikoa ya Jirani, wajitokeze kwa wingi siku ya ya Jumamosi Tar 9.03.2013 usiku katika ukumbi wa Dar Live Mbagala kushuhudia warembo hawa wakipanda jukwaani kuwania Tuzo mbalimbali za Vipaji na Utamaduni. 

Mbali na kupita jukwaani na mavazi mbalimbali washiriki wote pia watashindana kucheza na kuimba nyimbo za Asili za Mikoa wanayo wakilisha. Na hili litakuwa ni tukio la kihistoria la Utalii, Urembo na Utamaduni kuwahi kufanyika hapa Tanzania kabla na Baada ya Uhuru. 

 Fainali za Taifa za Miss Utalii Tanzania mwaka huu Zimedhamiwa na: Mtwana Catering Services, Ikondolelo Lodge, Zizou Fashion, Coca Cola Kwanza, VAM General Suppries Limited,Global Publishers, TANAPA, Ngorongoro Crater, Lakeland Africa, Clouds Media Group, Star Tv, Vailey Spring,Dotinata Decoration,Tone Multimedia Group, Baraza la sanaa la Taifa (BASATA ) 
www.misstourismorganisation.blogspot.com 

Washiriki wa Miss Utalii Tanzania 201213 wakitoa Burudani ya Nguvu katika Jukwaa la Sanaa (BASATA
Washiriki wa Miss Utalii Tanzania 2012-13 wakiwa katika mazoezi ya Nguvu ndani ya ukumbi wa Dar Live
Washiriki wa Miss Utalii Tanzania 2012-13 wakiwa katika picha ya pamoja na Mmiliki wa Mtwana Catering Service ambaye ndiye anaye walisha Warembo hao.
Washiriki wa Miss Utalii Tanzania wakiwa Katika Picha ya Pamoja Baada ya kumaliza Mazoezi yao Katika Ukumbi wa Dar Live

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Hongera sana Mkurugenzi wa Mtwana Catering Services!

    Urembo ni lishe kwa vile mwili haujengwi kwa matofali, kwa uwezeshaji wako kwa suala la lishe kwa hawa mabinti bibie Mkurugenzi unastahili pongezi!

    ReplyDelete
  2. Duhhh ama kweli Walimbwende tunao!

    Wasichana muwe kigezo chema, baada ya mashindano na sio muwakilishe ndivyo sivyo.

    ReplyDelete
  3. Ama kweli Mkuregenzi wa Mtwana Catering kazi umeifanya!

    Tatizo kubwa tunashindwa kujua chakula bora ni kipi, na ni namna gani tuandae, wengi tunafikiri chakula bora ni kama Chips Mayai na vitu vya kiulafi ulafi tu kumbe sivyo.

    Heee watoto wanaonekana wakali visichana wanang'ara kumbe dishi la mpangilio di dawa kamili, sio mchezo mwana wane?

    ReplyDelete
  4. Wasichana nawapeni Darasa lingine fupi la PERSONAL MANAGEMENT:

    Ili muwe Warembo mfuate mwenendo huu:

    1.Msiendekeze hulka mabaya ya Ulevi, imethibitika kuwa ulevi unazorotesha afya, unaleta msongo wa mawazo na sio kupunguza (kwa mnao onja angalieni Hang over baada ya ulevi siku iliyopita) ulevi pia una zeesha watu kwa kasi ya ajabu,,,tazameni watu walevi unakuta kijana wa miaka 19 anaonekana kama kikongwe wa miaka 91 hivi!

    2.Starehe ikizidi, inaleta msongo wa mawazo pia, hasa zile starehe za kukesha usiku kucha kwenye Kumbi zinazomalizika mida ya Majogoo(kukosa usingizi wa kutosha au kulala muda mfupi).

    3.Mzingatie mwenendo wa ulaji mzuri, muwe mnakula ikiwezekana vyakula asilia kwa wingi na matunda, na kunywa maji ya kutosha.

    4.Mapumziko ya kutosha na kutulia kimwenendo (kuacha mwenendo mbaya wa mikwaruzano na mifarakano) vinajenga kimwili na kisaikolojia.

    5.Muutumie muda kwa kupanga mambo yenye tija kimaisha, na sio kupoteza muda kwa mambo yasiyo na tija, mfano kutumia muda mwingi kwa maongezi yasiyo na faida badala ya shughuli zenye tija kama kazi za mikono.

    ReplyDelete
  5. TTB na Wizara ya Utalii nyinyi mnacheza na marketing kwenye utalii,wenzetu wangukuwa na nusu ya vivutio vyetu wangekuwa mbali sana ila ulimbukeni na kuto kuwa wawazi ili kushirikisha wadau ktk sekta hiyo,ili kutangaza utalii lazima kuwepo na programe za utalii wa ndani na wa nje na lazima kuwepo na kipaumbele kwa kutangaza nje sana ili tuwe na wageni wengi lakini TTB na wizara wanasubiri kushiriki matamasha ya utalii peke yake hiyo haitoshi,wenzetu wana kitu kinaitwa road show,haya ni maonyesho madogo yenye kutargetwatalii wanaotaka kuja Tanzania,lakini tatizo Tanapa,wana plan zao,NCCA,TTB na wizara kila mmoja ana lwake kweli tutafika?tunatakiwa kuw ana kitu kimoja tu na all those key player wanakuwa behindi the forces kuliko hii vurugu ya sasa.nawakalisha.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...