Pichani juu na chini ni baadhi ya abiria wakiwa nje ya basi la Kilimanjaroo Express lenye namba za usajili T860 BVA walilokuwa wamepanda wakitokea jijini Dar kuelekea jijini Arusha mapema leo asubuhi.
Ajali hiyo imetokea eneo la Mombo ambapo chanzo chake kinaelezwa kuwa dereva wa basi hilo alikuwa akimkwepa mwendesha baiskeli, matokeo yake basi hilo likakosa mwelekeo na kupinduka. Katika jali hiyo inaelezwa kuwa watu kadhaa wamejeruhiwa lakini hakuna aliyepoteza maisha.

Nimekuwa nikiendesha katika hii barabara kwa miaka mingi sasa. Tatizo la watembea miguu na waendesha baiskeli ni kubwa na dereva inabidi uwe muangalifu sana usigonge mtu. Ninashauri katika ujenzi wa barabara uzingatie kujenga njia za pembeni. Jambo hili linawezwa kufanywa na mkandarasi au mamlaka inayohusika na sehemu hiyo.
ReplyDelete