Na
Mwandishi wetu
KAMPUNI ya Compass Communications imewatahadharisha
warembo na wanamitindo wote nchini
kutorubuniwa na genge la watu wanaotumia jina la Flaviana Matata kujipatia
fedha kwa njia ya udanganyifu.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Compass Communications,
Maria Sarungi Tsehai amesema jana kuwa kuna genge la watu wanaotumia ukurasa wa
mtandao wa kijamii wa facebook ujulikano kwa jina la Flaviana Matata’s na kujipatika fedha kiasi cha sh. 200,000 kwa
jila anayejiunga kwa lengo la kutafutiwa kazi au nafasi ya kufanya shughuli za
wanamitindo nje ya nchi.
Maria alisema kuwa watu hao huwarubuni wasichana na
kuwaahidi kuwatafutia kazi nje ya nchi kwa mgongo wa Flaviana na mmoja wa
vijana hao amejitambulisha kama ‘kaka’ yake mwanamitindo huyo, jambo ambalo si
la kweli.
Alifafanua kuwa baada ya kukutana na wasichana
waliongia katika mtego huo, huwa wanaawalaghai kwa njia mablimbali na baadaye
kulipa kiasi hicho cha fedha. Alisema kuwa hali hiyo imewaletea usumbufu
wasichana wengi na kujikuta wakihaha kutafuta ukweli baada ya kutapeliwa.
“Compass Communications kama kampuni inayosimamia
shughuli za Flaviana Matata inatoa tahadhari kwa umma kuwa Flaviana Matata
hahusiki kwa njia yoyote na ukurasa huu au watu hawa. Pia tunawatahadharisha wananchi kuwa wawe
waangalifu kwani Flaviana Matata hayuko katika biashara ya kumtafutia mtu
yoyote kazi ya uanamitindo popote pake,”
alisema Maria.
Maria alisema kuwa ukurasa halisi ya Flaviana Matata
kwenye mtandaomwa Facebook ni “Flaviana Lavvy Matata” na kwa sasa wanendelea kushirikiana
na vyombo husika kwa kutoa taarifa kuhusu uhalifu huo.
Ugumu wa maisha kipimo cha akili!
ReplyDeleteAcheni tamaa mbaya ya kufikia mafanikio, kuweni na uchu stahiki ili kufikia mafanikio kwa njia zinazokubalika.
Wabongo acheni tabia ya kupenda mafanikio ya haraka haraka, fanyeni kazi kwa bidii na muwe na malengo na msiwe na tabia ya kuiga iga bila mpango.
Ni aibu kubwa mtu Mwanaume mzima kutumia taswira ya Msichana kama Flaviana kujipatia fedha.
Flaviana Matata alipofikia amefanya kazi ya ziada hakupata kiurahisi rahisi, hivyo msiote kupata mafanikio kwa migongo ya wengine.
Acheni kusafiria nyota za wenzenu!