Baadhi ya Vijana waliopata mafunzo ya jinsi ya kutengeneza mkaa mbadala wakionyesha
jinsi ya kutengeneza mkaa huo wakati wa ufungaji wa Mafunzo ya Ujasiriliamali
kwa vikundi vya Vijana kutoka Kata za Vingunguti na Buguruni jijini Dar Es
Salaam.Mafunzo hayo yaliendeshwa kwa Ufadhili wa Shirika la Kimataifa la Plan.
Mmoja wa wahitimu akipokea cheti kutoka kwa Mkuu wa
Wilaya ya Ilala Mh.Raymond Mushi wakati wa ufungaji wa Mafunzo ya
Ujasiriliamali kwa vikundi vya Vijana kutoka Kata za Vingunguti na Buguruni
jijini Dar Es Salaam.Mafunzo hayo yaliendeshwa kwa Ufadhili wa Shirika la
Kimataifa la Plan.Kushoto ni Meneja Miradi wa Plan Wilayani Ilala Bw.Daniel
Kalimbiya.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh.Raymond Mushi akimsikiliza
mmoja wa Vijana waliopata mafunzo ya
jinsi ya kutengeneza mkaa mbadala wakati wa ufungaji wa Mafunzo ya
Ujasiriliamali kwa vikundi vya Vijana kutoka Kata za Vingunguti na Buguruni jijini
Dar Es Salaam.Mafunzo hayo yaliendeshwa kwa Ufadhili wa Shirika la Kimataifa la
Plan
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh.Raymond Mushi akiangalia
mkaa mbadala wakati wa ufungaji wa Mafunzo ya Ujasiriliamali kwa vikundi vya
Vijana kutoka Kata za Vingunguti na Buguruni jijini Dar Es Salaam.Mafunzo hayo
yaliendeshwa kwa Ufadhili wa Shirika la Kimataifa la Plan.
Vijana waliopata
mafunzo ya jinsi ya kutengeneza mkaa
mbadala wakimsikiliza Mgeni Rasmi wakati wa ufungaji wa Mafunzo ya
Ujasiriliamali kwa vikundi vya Vijana kutoka Kata za Vingunguti na Buguruni
jijini Dar Es Salaam.Mafunzo hayo yaliendeshwa kwa Ufadhili wa Shirika la
Kimataifa la Plan.(Picha na Demetrius Njimbwi-Jeshi la Polisi).
=============== ========= ==============
Na Frank Geofray-Jeshi la Polisi
Vijana
nchini wameshauriwa kuacha kubweteka na kuonekana mzigo kwa familia na
badala yake wajikite katika ujasiriamali ili kupambana na hali ngumu ya
maisha hatua itakayo wasaidia kuongeza kipato na kuinua uchumi wao.
Wito
huo umetolewa mapema jana na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh. Raymond Mushi
wakati akifunga mafunzo ya siku tano ya ujasiriamali wa kutengeneza mkaa
unaotokana na mabaki ya takataka za majumbani na viwandani kwa Vikundi
vya Vijana kutoka Kata za Vingunguti na Buguruni yaliyofadhiliwa na
Shirika la Kimataifa la Plan na kuendeshwa na Wakufunzi kutoka Shirika
la Kuhudumia viwanda vidogo (SIDO).
Mh.
Mushi amesema kuwa, moja ya changamoto zinazowakabili vijana wengi ni
kutokupenda kujishughulisha na badala yake hutumia muda wao mwingi
katika kufanya mambo yasiyo na faida hali ambayo imekuwa ikichangia
kurudisha nyuma jitihada zao za kujiletea maendeleo.
Alisema
kuwa pamoja na mafunzo yaliyotolewa kwa vijana hao, bado wanajukumu la
kutambua maendeleo yanaletwa na wao wenyewe kwa kuutumia ipasavyo ujuzi
walioupata hatua itakayo saidia kufungua fursa ya ajira.
Aidha aliwataka vijana kuzingatia maadili ikiwa pamoja na kuthamini mafunzo waliyoyapata na kuwa na tabia ya kushirikiana katika mambo yatakayo wasaidia kuongeza ujuzi pamoja na kutanua wigo wa kibiashara.
Kwa upande wake Meneja Miradi wa Shirika Plan
Wilayani Ilala Bw. Daniel Kalimbiya amesema kuwa, bado wataendelea
kushirikiana na taasisi mbalimbali ili kuboresha maisha ya Watanzania
ikiwa pamoja na kuwataka vijana kutokujiingiza katika
vitendo viovu vya uhalifu ikiwemo kujiuza katika madanguro kwa
kisingizio cha kukosa ajira.
“Tumieni
fursa vyema mliyoipata hapa ili mjiletee maendeleo na sisi tutaendelea
kushirikiana na kuviwezesha vikundi vya Vijana ambavyo vimekuwa
vikifanya vizuri katika kujiletea maendeleo kwani malengo ya shirika
letu ni kutetea haki za Watoto na Vijana”Alisema Kalimbiya
Naye
Meneja wa SIDO Mkoa wa Dar Es Salaam Hamwel Meena aliahidi kuwapatia
vijana hao mikopo itakayowawezesha kununua mashine zitakazowawezesha
kufanya kazi ya kutengeneza Mkaa mbadala kwa ufanisi ili kuokoa
mazingira na kuufanya mji kuwa msafi kwakuwa mkaa huo unatengenezwa
kutokana na takataka.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...