Waziri wa Habari. Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara (pichani) ameliamuru Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuitisha mkuu wa marekebisho ya katiba na kuingiza marekebisho yote kuanzia ya mwaka 2007 hadi 2010 kwa kuwa katiba iliyopo kwa Wizarani ni ile ya mwaka 2006.
Hivyo Dk. Mukangara ameipa TFF siku 40 toka leo watekeleze hilo la mkutano wa marekebisho ya katiba na kwamba kabla ya Aprili 15, mwaka huu hayo yawe yameshafanyika.
Chanzo cha habari cha uhakika kimeiambia Globu ya Jamii jioni hii kwamba mchakato wa uchaguzi mkuu uliojaa mizengwe kabla ya kuahirishwa sasa unaanza upya.
"Wameambiwa waitishe mkutano mkuu wa marekebisho ya katiba na kuingiza marekebisho yote kuanzia ya mwaka 2007 hadi 2010 kwa kuwa katiba iliyopo kwa Waziri ni ile ya mwaka 2006 na wamepewa siku 40 toka sasa watekeleze hilo la mkutano wa marekebisho ya katiba kabla ya Aprili 15 yawe yameshafanyika.
"Pia wamepewa siku 40 nyingine kwa hiyo jumla ni siku 80 baada ya marekebisho ya katiba uanzie mchakato wa uchaguzi na hadi Mei 25 uchaguzi mkuu uwe umeshafanyika na pia TFF wametakiwa ndani ya siku tano kuanzia leo (jana) hadi Marchi 11 Jumatatu kuhakikisha wameshatoa msimamo wa kutekeleza agizo la Serikali" kimedatisha chanzo hicho.
Chanzo hicho pia kimesema kuwa katika mkutano wa marekebisho ya katiba, maazimio yatapitishwa kwa njia ya kupiga kura za uwazi kwa kunyoosha mkono ndio au hapana na pia kufuatia agizo hilo la Serikali kamati ya rufaa chini ya Idd Mtiginjola itakuwa imekufa kibudu huku ile ya Profesa Mgongo Fimbo ndio itakayopewa jukumu la kuendelea na zoezi la Kamati ya rufaa.
Akizungumzia suala hilo Katibu mkuu wa TFF, Angetile Osiah alisema "Nimewaoneni mmeingia Wizarani, wambieni wawape taarifa huko mimi siwezi kuzungumza chochote sijapata barua yoyote kutoka Wizarani."
Hata hivyo kwa upande wa Wizara walisema kuwa tayari wameshawapelekea TFF barua na kwamba TFF ndio yenye jukumu la kutangaza yale yaliyozungumzwa kwenye kikao chao na Waziri.
Kabla ya hapo, Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara alikataa kupangiwa siku ya kuonana na viongozi wa TFF na badala yake aliwataka jana kufika ofisini kwake kwa ajili ya kikao walichoomba. Na wasingekutana naye ngoma ingesimama kwa muda kwani Waziri alitarajiwa kusafiri jana usiku kwa muda wa siku 10.
Juzi TFF kupitia kwa Katibu mkuu wake Angetile Osiah alisema wamewasilisha barua kwa Waziri Mukangara kutaka kukutana naye siku ya Alhamisi, na kama ikishindikana wakutane baada ya March 13 na kwamba wanamtaka Naibu Waziri Amos Makala akae kando katika suala lao kwa vile ameshaonyesha ana upande anaoupendelea.
Upekuzi wa Globu ya Jamii unaweza kuthibitisha kwamba barua iliyokwenda Wizarani ambayo ilisaniwa na katibu huyo wa TFF yenye Kumb:Na: TFF/ADM/MIYCS.13/03 ya March 4 imeomba kukutana na Waziri bila ya kuweka angalizo la kumtaka Naibu Waziri Amos Makalla kukaa kando tofauti na alivyotangazia vyombo vya habari.
Hakuna mtu au kikundi cha watu kilicho juu ya serikali..hawa TFF wanachekesha kweli..waziri yyt kateuliwa na rais ..hivyo basi hio ni serikali..swali la msingi hivi huko TFF kuna nn??maana hata akina Ndolanga/Rage walikuwa hivihivi hawataki kuondoka duuh c mchezo.
ReplyDeleteHivi hao wakina Tenga kweli wako na hekima na busara sasa ona mambo yanavyo wakumba na kuwahaibisha ,kisa wanaweka urafiki mbele,miaka kadhaa iliyopita Rais Goodluck aliingilia chama cha mpira cha Nigeria na FiFa waliwafungia lakini ilikuwa fundisho kwani walijipanga na sasa ni mabingwa Africa na hakuna ujinga kama hawa wetu wenye vichwa panzi.Mkono wa serikali ukiingia uwezi chezea,sijui katibu au rais wa TFF wewe huko chini ya nchi sasa unawezaje kusema usiingiliwe?haya sasa kama ulitaka uonekane ni super hero tumewajua nyie ni wakina nani.
ReplyDeleteNaona waziri ameshindwa kuelewa sheria na kanunu za FIFA.
ReplyDeleteFIFA inatamka wazi kuwa mashirikisho yake yanaendeshwa nje ya serikali i.e serikali haina nguvu ndani ya vyama vya mpira, serikali ikiingilia kati katika uendeshaji wa chama cha mpira, FIFA huifungia nchi husika kuwa mwanachama wa FIFA. rlane
Bora tufungiwe na kukaa nje ya FIFA kama hakuna faida yoyote na chama cha mpira kiwe na utaratibu mzuri kuliko kuwa na wahujumu wachache wenye kuleta vurugu,anasema awawezi itisha mkutano mkuu kisa gharama za millioni 135...pambano moja la yanga na simba linaingiza millioni 200-300 iweke kwa mkwa au miaka miwili usiweze kufanya mkutano mkuu?unashindwaje kuandaa mechi za kirafiki ili uweze pata pesa ya mkutano?huyu tenga anaondoka kwa kujichafulia jina na pesa yote ndio inawakimbiza na kuwafanya hawajui majukumu yao.
ReplyDeleteSerikali ni serikali - hasa hizo za 3rd world, hazitaki kukosolewa. Tenga should know better about this. Hawa watu wote walikuwa UDSM, hapa wanaonyeshana ubabe tu ni wazi huyo mama akiwa Minister atashinda. The best thing for Tenga is to resign. Osiah you are on contract, when the knew executive comes in they will have the power to terminiate your employement, Tenga will not be there to cover you. Wewe ni mtumishi, kaa kimya. Acha Tenga na Waziri walishughulikie swala helo, morevoer hao wote wawili ni Yanga raizoni so all things will be sorted out at the end of the day.
ReplyDeleteHuyu waziri mambo haya hayamhusu.
ReplyDeleteMara nyingi sana serikali inapoingilia mambo ya michezo lazima mambo yataharibika, Serikali wafanye mambo yao huku wakitoa mwongozo tuu na wala sio kushinikiza cha kufanya.
Kama serikali inataka kuongoza kwenye michezo watoe pesa kuendeleza mpira wa mguu na mkono,riadha na michezo mingineyo inayoweza kuiletea nchi sifa, haya mambo mengine ni kuwa waziri amekosa la kufanya.
WAZIRI TIMIZA WAJIBU WAKO.TFF WAMEZOEA MARUMBANO
ReplyDeleteNdani ya miezi sita baada ya Tenga kuondoka tutaanza kumkumbuka kwa mema,acha upepo huu wa wanasiasa upite.kwanini mtu anataka kuongoza tff kwa hali na mali?yuko tayari hata kugharamia mkutano huo kama TFF itakuwa haina fedha ili mradi awe kiongozi kuna nini tff?na yuko tayari nchi ifungiwe na fifa ili mradi yeye awe rais wa tff kwa nini?vyombo vya habari vyote viko upande wake kuna nini?hivi huyu mtu anamfikia Tenga kwa uwezo wa uongozi,hekima,visioni?.Namshauri Tenga awaachie hawa wachezaji wa gofu,mapromota wa ngumi na viongozi wa kriketi ili waongoze soka letu na ndani ya miezi sita tutajuta,hawa wana ajenda zao kupitia soka
ReplyDelete