Assalam akaykum
Nimeona nichukue nafasi hii nitoe mapendekezo maana sijaona mwananchi kuchangia mawazo kutokana na matatizo yaliyopita ya mitihani Tanzania sasa kwa upande wangu nina haya naomba sana tena sana niwekee japokuwa ni marefu kidogo lakini nahisi ni jambo muhimu:

Mfumo wa Elimu Ningependekeza ungekuwa hivi:

Kuwepo na Tuition Resources (iwepo Online au hata maktaba zetu) ambayo itakuwa na mgawanyiko wa mambo makuu matatu (3) nayo ni haya:
 
1.      1. Syllabuses (Silabas)
2.      2. Lecture Guides (Muongozo wa Kusoma na kusomesha)
3.   3.    (a) Specimen question papers. (Sampuli ya Maswali) (b) Past Question papers and Answers.(Maswali na Majibu ya Mitihani iliyopita)
Mambo ya Nyongeza :
·         Kama kutakuwa na mabadiliko yoyote kwa mtihani ujao uelezwe hapa.(MFANO Masuala mangapi yanatakiwa yajibiwe yameongezeka au kupungua)
·         Kama kutakuwa na Mabadiliko au nyongeza  ya Syllabus vile vile ioneshwe hapa.
·         Ripoti ya Mtihani ambayo ieleze wapi wanafunzi walifanya uzuri na wapi bidii iongezwe na wapi walifanya vibaya.
·         Vidokezo vya kusoma (Reading Tips)
·         Listi ya Vitabu au website za kutafuta material zaidi (Reading lists)
·         Kuwepo na Manual au Mkusanyiko wote wa masomo  ambayo kama kutakuwa na mabadiliko yaelezwe kama nilivoorodhesha hapo juu wapatiwe wanafunzi kwa either bure au pesa kidogo walipie
·         Kuwepo na reward kwa wanafunzi waliofanya vizuri na utambulisho mfano watolewe kwenye majarida maalum ya elimu ambayo yatasambazwa bure au hata kwa fee ndogo.

Ufafanuzi kidogo
 
1.       Sylubuses : Zioneshe mgawanyiko wa masomo ambao mwanafunzi akitoka atatoka na ujuzi mfano somo la Biologia
1.       Agriculture iwepo na core unit (masomo ya lazima) na optional zake asipandikizwe mwanafunzi mambo ya Anatomy au Biochemistry au biomechanics pamoja na masomo yanayohusu Agriculture, (information overload).
 
2.       Lecture guides: ambayo itagawika kwa:
(a) Learning outcomes (Mwanafunzi aelezwe umuhimu wa hicho unachomsomesha       
            kwanza kabla hata ya kwenda kwenye mada.
             (b)Indicative contents ( Ambazo zipo kwa number mfano  Somo la Human Resources  
             1.1Definition, 1.2.Work related stress ,1.3 Equality) Hii itamsaidia mtu kukumbuka   
              ambapo akijibu suala la mtihani kuwa topic hii ni topic ya 1.3. au 2.4.au hata  
             akitafuta material online yatamuonesha kuwa soma topic no.1.3 au 3.4 n.k
             (c)Examination tips (Muhimu sana unamueleza mwanafunzi atarajie swali la aina
                gani katika topic hii na jibu la aina gani ajibu)
 
3.        (a) Specimen Question papers ambazo zinakuwepo mwanzo wa mwaka kuonesha mwanafunzi atarajie masuala ya aina gani yatakuja katika mtihani sasa anajifanyia mara kwa mara kujibu maswali haya  kwa kutumia resources mbali mbali na pia zioneshe marks ambazo atapata kwa kila suala atakalojibu .
            (b)Maswali na majibu ya mtihani iliyopita,ni muhimu kwa kuwa unamjengea  
            mwanafunzi jinsi gani ya kujibu masuala au atarajie nini ,
 
Hitimisho
Wengi watasema mfumo wa maswali na majibu wanafunzi watakuwa hawasomi wata solve maswali tu,lakini sio kweli mfano yakiwepo maswali ya somo la Biologia tokea ya mwaka 2005 naamini kujibu mara kwa mara haya maswali yanakujengea confidence na ufahamu vile vile na mara nyingi elimu ni ile ile mambo madogo madogo tu yanaongezeka ambayo hata kwenye mitihani ya ulaya huwekwa kijiswali kidogo tu kimoja cha mark ndogo kutokana ni jambo jipya.
Mfumo huu pia unatumika U.K mfano maswali ya interview unatakiwa uyasome na sio uwende interview kichwa kichwa,
masuala ya driving lesson unakuwa na CD na vitabu ambayo kwenye mtihani wenyewe yanakuwa hayohayo
Masuala ya uraia unapewa kitabu unasomeshwa hivo hivo hata masuala ya shule .
Sasa tuchukue mfano wa Driving lesson unajiona unajibu tu maswali lakini utakapoanza kuendesha je halikujii swali ulosolve ukaona aha nilisolve hili swali kuwa round about nikae upande gani sasa je si ujuzi huu?
 
Haya ndio nionayo mimi ila kila mtu ana mawazo yake
Ahsanteni.

Dr.Abdul AE 
University of Huddersfield 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Mapendekezo mazuri sana mdau. Ni vizuri watanzania tufike mahali tuiokoe elimu yetu kwaajili ya vizazi vijavyo. Siyo kuwa kila pendekezo linafaa lakini ni vizuri watu wengi kutoa yaliyopo moyoni kwa njia ya kuboresha. Napenda kukuuliza swali; ulipoanza kwa kuandika kuwa hujaona mwananchi kuchangia ulikuwa na maana gani?

    ReplyDelete
  2. Great and well defined points

    ReplyDelete
  3. Tatizo ni kubwa na mabadiliko yanayotakiwa kufanyika ni makubwa. We need the whole education reform in Tanzania. Maoni yangu hii ndio barua niliyotuma kwenye kamati teule. open this link

    http://leadergennis.blogspot.com/

    ReplyDelete
  4. Usilinganishe elimu ya UK ni ya TZ. Watoto wote wanaofaulu wanapata nafasi za kuendelea mbele UK na kupata kazi, lakini TZ nafasi za secondari hazitoshi kwa kila mtu, pia nafasi za kazi hazitoshi kwa kila mtu. Pia kulinganisha driving lisence na elimu ya kweli ni tafauti. Pia UK raia wao ambao ni hodari wanasoma kwenye skuli maalum na wanahudhuria vyuo vikuu maalum kama vile Oxford, Cambridge, Empirial College, LSE, n.k. Wanapomaliza wanaazisha makampuni yao au wanafanyakazi kwenye makampuni makubwa sana ya UK.

    ReplyDelete
  5. walimu WENGI wanaofundisha ni 'makapi' sababu wenye uwezo hawaendi kwenye ualimu. Vile vile hawafundishi kwa moyo sababu kipato kigodo. Kwa hiyo kinachotakiwa kufanyika ni serikali kuwekeza kwenye elimu. Haya mambo ya kiufindi hayatafanikiwa kama serikali haikuwekeza kwenye elimu. Na ndio maana tunailamu serikali lakini zaidi si kwa kushidwa kuteleleza kutekeleza mambo ya kiufundi unayosema bali kushidwa kuwekeza kwenye elimu. Tukifika wakati mu anayeingia chuo kikuu akichagua 'education' badala ya 'public administration' au 'economics' then tutakuwa kwenye mwelekeo mzuri. Siku hizi waalimu wanaoonekana 'WAJANJA' ni wale walioweza kuacha ualimu na kujiunga na mashirika mengine...

    ReplyDelete
  6. Dr.Abdul ahsante sana kwa Mawazo,

    Ni vyema ukaandika Full Proposal na kuituma huku moja kwa moja kwenye Mamlaka ili mawazo hayo mazuri sana yafanyiwe kazi.

    1.Mfano umegusia suala la ICT, hilo ni wazi tuna mapungufu na vehicle hiyo mashuleni lakini kulingana na kasi ya maendeleo tunatakiwa tuweke msisitizo kwenye Educationn for ICT ili Wanafunzi waweze kusomea online.

    Ingawa hadi sasa, tunaweza kusema Walimu hawana stahili zao kimafao hawajatoshelezwa, ni vipi tutaweza kutimiza masomo ya wanafunzi kwa Mtandao huku Walimu mishahara na Maslahi yao yako ktk mwendo na hali ya sintofahamu?

    2.Jambo la wazi ni kuwa kuanguka kwa Elimu nchini mojawapo ya sababu ni kuwa

    ''Mfumo au aina ya Elimu tunayotoa Mashuleni hailingani na kasi ya maendeleo tuliyofikia hasa ktk ICT'',

    Mfano watoto wa sasa wanatumia muda wao mwingi ktk internet na chat (kwenye Simu zao na PC, Laps) wakati huko masomo yao hayawafikii ili wasome au hakuna vehicle inayowaunganisha na masomo, kitu ambacho zinatakiwa Education reforms kama hizo unazosema ili elimu iwafikie wasomaji huko waliko kwenye internet.

    Maana kama unavyoona Ngalawa inakwenda mrama ama inakaribia kuzama kabisa!

    ReplyDelete
  7. Mimi naomba kuchangia kidogo sana.Wanafunzi wanapomaliza mitihani waruhusisiwe kuondoka na karatasi za mitihani labda kama siku hizi wanajibu kwenye karatasi za Maswali ili PAST PAPERS zipatikane kihurahisi(si wanafunzi wanailipia?) au baada ya mitihani ya kidato cha nne(mfano) wanafunzi wote wa kidato cha tatu wapate nakala ya mtihani ya kila somo waangalie format.Mnarudisha mitihani kwenye baraza kufanya nini???

    David V

    ReplyDelete
  8. Pendekezo zuri sana ila bila ya kulifumua baraza la mitihani na kulifanyia reform mapendekezo yako yatakuwa ni kazi bure tu.

    ReplyDelete
  9. Mimi nimefurahia kitendo chako cha kutoa solutions badala ya kama karibu asilimia 99% ya wanainchi wenzetu kuishia kutoa lawama kwa serikali.
    jamani kuipigia serikali kelele sasa imetosha, kilichobaki tupige kelele za ufumbuzi ili tuweze kujinasua hapa zaidi ya hapo tutakua tunapoteza nguvu zetu nyingi sana.

    Mdau!

    ReplyDelete
  10. Mdau sat mar16,inaonesha unamawazo bado ya tulipotoka,watu wa kuogopa mabadiliko na pia watu wanaokata tamaa kwamba tusilinganishe ,tusifanye,hatutoweza,NA MAWAZO YAKO NI STATIC Umesahau kitu kinachoitwa Benchmarking,ikiwa hatutomia benchmarking (kulinganisha) je tutafanikiwa wapi? Wenzetu wanaendelea kwa kuwa wanalinganisha na wanaona wapi wamekosea ndio maana wanafanikiwa,usiwe na akili ati shule hazitoshi -kazi hakuna-ndio kazi hamna kwa sababu elimu unayosomeshwa sasa inahitaji mabadiliko makubwa ikiwa mwanafunzi atatoka na ujuzi basi anaweza kuwa Entrepreneur,au hata kuajiriwa sehemu tofauti.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...