Kaka Michuzi Salaam Aleuikum,

Baada ya salaam, napenda kulizungmzia ili swala au kero linalowasumbua watanzania wengi. Kwa kweli, kwenda kupumzika au kula Sea-Cleaf ni tatizo ambalo uongozi wa jiji au serikali inabidi iingilie kati kwani tunakoelekea ni kubaya zaidi, kwani itafika hatua kila mtu atajichukulia hatua ya kufanya kila atakalo kwa manufaa yake Kwa muda mrefu nimekuwa mteja wa eneo la Sea-Cliff hasa sehemu ya Karambezi restaurant. 

Napenda sana kwenda pale na familia yangu. Kwa bahati mbaya kwenda pale sasa hivi na gari ni tatizo. Chakula ni ghali kuliko sehmu ya kula ulaya. Mbaya zaidi, wanachaji kupaki gari. Yaani licha ya kwamba chakula ni ghali mno, bado unalazimishwa kulipia kupaki vinginevyo hautoki Majuzi nilipoenda pale, nililalamika sana kuhusiana na hii tabia. Nikamwambia mkuu mmoja mwenye asilia ya Ki-Asia kwamba huu ni unyang’anyi. 

Yeye badala ya kunielewesha, aliniporomoshoea tusi la nguoni.Sikuwa na la kujibu. Tunaiomba serikali iingilie kati kuisaidia umma wa kitanzania. Vinginevyo tutawaomba wanchi waanze kuisusia hii sehemu kutokana na mwendelezo wa hii tabia. Serena, Kilimanjaro hata na Double tree ambazo ni za daraja za juu kupaki ni bure, lakini Se-Cleaf wanachaji kupaki. Uongozi wa Sea-Cleaf tunaomba muingilie kati hili tatizo la kuwachaji wateja wenu kupaki gari ili kuja kula. 

Nawakilisha 
Mdau

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Kwani hakuna sehemu nyengine ya kula na kupumzika mpaka iwe hapo Sea Cliff?

    Fedha ulipe wewe, matusi upate wewe na bado unalalamika!

    ReplyDelete
  2. ndugu yangu shida ipo wapi? tafuta sehemu nyingine utakapo pata huduma bila usumbufu, si lazima uende hapo

    ReplyDelete
  3. True nimeona mambo kama hayo south beach hata sunrise. unapoingia pale unalipia takriban elfu ishirini mtu mzima.
    Kinachoudhi mimi ni kuon maji ya tshs 500/= yanauzwa takriban elfu tatu!!! Najua ni free market lakini kama mtu umemcharge such hi, why umkamue such way tena?
    But najifunza kwamba haya yote ni kwakuwa wabongo hatujifunzi kuanzisha service kubwa kama hizi na tukarahisisha watu wachovu kuburudika,, badala yake tunajipeleka kwa hawa wenzetu!!

    pole sana mzee
    G7

    ReplyDelete
  4. Watanzania wenzangu mbona mnatia aibu! kama huwezi kumudu gharama za chakula na za kupaki gari kwanini UNAENDA hapo seaclif? si UZIRE to usiende,kiherehere cha nini? eti serikali iingilie kati, ACHA kwenda nenda uswahilini ukale mchemsho safiii, ukitaka kutanue lazima uwenazo, siyo zakubania bania halafu halafu unaleta MIROROSO hapa, SERIKALI ina mambo mengine ya maana ya kufuatilia,ie: Kufuta ujinga, kupunguza maternal and child mortality rates, kuboresha huduma za afya kwa wote, maji safi ya kunywa kwa wote, eradication of malaria,nakadhalika, don`t be so selfish mate. JUST DON`T GO THERE, END OF!.

    ReplyDelete
  5. Kwani kwenda huko ni lazima mkuu?

    ReplyDelete
  6. Kwa wale waliosafinri watakubaliana namimi huko tunakoendelea hawa jamaa wenye asili ya kiasia watakuwa na matatizo makubwa. Wamekuwa na dharau sana sehemu nyingi za dunia hasa kwa waafrika na ni wabaguzi. Serikali iingilie kati mapema manake wao ni minority sasa kama wanajijengea utabaka itakula kwao.

    ReplyDelete
  7. MIE SIONI TATIZO KULIPIZA MAEGESHO YA MAGARI HIYO SEHEMU KAMA WATAKUWA NAO WANALIPIA USHURU, TaTIZO LIPO KWENYE MTU AKISHAJIONA MKUBWA WA MALI ANAANZA MATUSI YANGUO, WW SIKILIZA MLALAMIKAJI KWA MAKINI ALAFU MFAHAMISHE KAMA UKUBALIANI NAYE KWA BUSARA. M

    ReplyDelete
  8. hiyo parking ni sh ngapi?
    ila kama unapesa za kula bei ghali mmh unalalamika nini, pale ukienda paki bure na wizi uliojaa maeneo yale unadhani utamlaumu nani ukitoka ukakuta gari halipo?
    walinzi inabidi walipwe, kama unajua basi masaki kuna wizi sana wa mabegi, magari etc sasa pale palivyo wazi unadhani watafanyaje wasipolinda magari ya wateja wao.

    wengi tunajua hata tukienda rose garden, break point ukitoka lazima kumpa mlinzi achenji ka chai maana ukijifanya hutoi basi labda hautarudi pale, ila ukitoa wanafurahia na ku note gari lako na siku ingine wataangalia tu wakijua ukitoka wanapata kitu.

    mie nadhani ukipaki kwa kiingilio. ukaingia kula unakula vizuri na kwa raha ukijua usalama nje upo.

    Pia hapo wengi walitumiaga parking yao na kwenda kwingine hivyo wateja wao wanakosa pa kupaki pia.

    Sasa usipotaka kutoa basi si una pesa nenda kwingine.

    Serikali haiingilii biashara za watu, kwa kweli umenisikitisha kuomba serikali iingilie suala hili. nilipoanza kusoma nilidhani unataka kuongelea wizi wa maeneo hayo ya masaki kumbe kulipia parking mmmmmmhhhhh.

    maana hata mikoba sie wanawake tunaibana kuogopa gari linalopits mtu anaweza kulivuta etc

    ReplyDelete
  9. Mdau kwa kweli hata Ughaibuni kuna sehemu sio kila mtu anamudu kwenda. Kuna sehemu zimewekwa kwa watu wenye pesa zao kutumia bila ya kusumbuliwa. Hakuna ubaguzi dunia ya sasa bali pesa yako. Kupata pesa inabidi uwe na kipaji.

    ReplyDelete
  10. Acheni ujinga na umbumbumbu waTanzania! Jamaa anaomba mamlaka husika ziingilie kati ili kuwasaidia waTanzania sasa nyie mnasema kwani amelazimishwa kula Sea Cliff? Ebo? Ndiyo maana hatuendelei kwa ujinga uliotujaa.. hivi mnafikiri uhuru wa biashara hauna mipaka? Tembeeni muone!!! Ukienda Stears pale Samora Ave unalipa parking kwa mgambo wa City.. sasa hivi kwani Stears siwanalipa sales tax kwa city!! sasa ukiwacharge watu kupaki kwenye eneo la stears maana yake ni nini? Kama siyo wizi? Unatoaje leseni ya biashara bila kuruhusu parking kwa wateja? Ni uwizi unaobarikiwa na ushamba wa Wenzetu wachache bongo..: ( Mteja ni mfalme cha msingi hapa ni mamlaka husika kuingilia kati tatizo la parking na bei za vyakula zisizoendana na gharama halisia...Nchi haiwezi kuendeshwa kiujanjaujanja namna hii.. Historia inatuonyesha ni jinsi gani hawa Wageni walitajirika kwa kurudufu bei! Mteja lazima alindwe na mamlaka husika.. mwenzetu ametukanwa tena na mgeni halafu tunapuuza na kusema asirudi tena hapo!! Ebo? Hebu nendeni mkatukane nnchi za watu muone chamoto! Hatuna hata uzalendo?

    ReplyDelete
  11. Mtu anawapa taarifa msionewe kijinga mnaanza kumvamia eti sio lazima aende pale. Kwahiyo hamtaki tatizo litatuliwe mnakubali kukandamizwa na waasia!! Mm wabongo amkeni mtaonewa na kila mtu, badala ya kusolve matatizo nyie mwayakimbia. Ndo maana tutaendelea kuonewa na wageni ndani ya nchi yetu kama tuna attitude hiyo ya kukimbia kimbia. Kwanini uikimbie sehemu unayoipenda? Khe

    ReplyDelete
  12. Sio kila sehemu kila mtu anaenda ndugu yangu. Wale uliowakuta na wanakula starehe bila kulalamika wao sio watu? Sio watanzania? Ukiona hivyo usilalamike, ujue pameshaanza kupita uwezo wa kipato chako ama hadhi yako.

    Ni mambo tu ya kawaida. Hata bei ya bia makumbusho, break point, Rose garden, Meeda, sio sawa na Kempinski, Bahari beach, Mediteraneo, etc.

    Cha kufanya ili kumaintain starehe ni kuongeza juhudi ya kazi. Ikishindikana unaacha tu. Kuna starehe halafu kuna starehe yenye hadhi.

    Jipange tu ndugu yangu. Au kama parking fee ndio inasumbua ibuka na taxi tu. Swala si ni kustareheka!

    Au kwa mfano ulitarajia serikali ifanyeje kuhusu hili? Ikawaambie wasitoze parking fees?

    Tena kwa taarifa utakuwa umewasaidia serikali kupata mapato ambayo labda hawajui kwamba yanaingia hapo. Na hiyo itapelekea either parking fees kuongezeka ama bei ya msosi kuongezeka maradufu.

    Pole mkubwa. Watoto inabidi waelewe tu na mama umwambie kuwa maisha sasa yamekuwa ghali. mbadilishe kiwanja. Watazoea tu kama walivyozoea hapo mwanzo.

    ReplyDelete
  13. MIE JUZI IJUMAA TAREHE 22/03/2013 NILIKWENDA NA DOLA 22,000 KWA AJILI YAKUWALIPIA WAGENI WA OFISINI KWETU TOKA MAREKANI KWAKUA NILIKUA NA GARI YA OFISI NA MFUKONI SIKUA NA HATA BUKU YA KITANZANIA ZAIDI NILIKUA NA KAMA DOLA 50 HIVI KTK WALLET.BUT MBALI NA KUCHOMA MAFUTA YANGU KUWAPELEKEA MIHELA YOTE HIYO AMBAYO HUENDA NINGEIPELEKA HOTELI NYINGINE NILIZUILIWA GARI YANGU KUTOKA TAKRIBANI LISAA LIZIMA.HAWAKUJALI NIMEWAPELEKEA DOLA NGAPI KAMA BIASHARA BALI NILIKOMALIWA MPAKA NILIPE HILO BUKU AMBALO SIKUA NALO MPAKA NIKATAFUTA SEHEMU YENYE M-PESA NIKAPATA HIYO BUKU YAKUNINUSURU NA AIBU ILE....IN SHORT THEY DONT CARE ABOUT THE CUSTOMERS

    ReplyDelete
  14. Duh mbona kenya hata ukienda Mall (kama Sarit Center au Westgate) parking unalipia? sembuse hapo ni mgahawa high end?? Cha msingi nenda sehemu ambazo unaweza kumudu gharama bila kupata manyanyaso ya moyo.

    Parking fee kwa nchi kama Tanzania ambayo watu wanaiba mpaka power window+taa za magari ni muhimu sana. Nchi za Afrika magharibi hakuna utamaduni wa wizi wa namna hii na hivyo hata parking fee hakuna sehemu zote mfano Ghana+Nigeria.

    Ila Afrika mashariki udokozi umezidi, sijui huu utamaduni umetoka wapi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...