Kadinali Jorge Mario Bergoglio wa Argentina (pichani) ndie amechaguliwa kuwa Papa mpya wa Kanisa Katoliki Duniani kote.
Kadinali Bergoglio anakuwa mtu wa kwanza kutoka Amerika kusini kuchaguliwa kuwa Papa.
Mara tu baada ya kuchaguliwa alichagua jina la Papa Francis I.
Awali moshi mweupe ulishuhudiwa ukifuka kutoka bomba la kutolea moshi katika kanisa la Sistine Chapel na kufuatiwa na kengele kupigwa. Hii ilikuwa ni ishara kwa walimwengu kuwa makadinali ambao walianza mchakato wa kumchagua Papa mpya hatimae walikuwa wamefaulu katika kazi yao.
Kadinali Bergoglio anachukuwa nafasi iliyoachwa wazi na Papa Benedict XVI, ambaye alijiuzulu mwezi uliopita akisema hana nguvu na uwezo wa kuendelea kuliongoza Kanisa Katoliki.
Makadinali 115 walikuwa faraghani tangu siku ya Jumanne alasiri na wakaanza mchakato wao kwa kupiga kura mara nne kwa siku.
Ilikuwa inahitajika kuwa angalau Makadinali 77 yaani theluthi-mbili wangeliweza kumpigia kura mmoja wao ili aweze kutangazwa kuwa Papa mpya.
Na kabla ya mchakato huo kuanza kulikuwa hakuna dalili za kuonyesha nani angelichaguliwa.
Moshi mweupe
Maelfu ya watu kutoka sehemu mbali mbali duniani walikwa wamekusanyika katika ukumbi wa Kanisa la St Peter tangu siku ya Jumanne.
Muda mfupi kabla ya Kadinali Bergoglio kujitokeza , maelfu ya watu walionekana wakikimbia kuelekea ukumbi wa St Peters ili kuweza kumshuhudia Papa mpya akitangazwa .
Papa Francis I ni nani?
Alizaliwa Mjini Buenos Aires huko Argentina mwaka1936.
Papa Francis 1 ni mtu wa kwanza katika kipindi cha miaka elfu moja (1,000) kwa mtu kutoka nje ya bara la Ulaya kutawazwa kuwa papa wa Kanisa Katoliki.
Papa Francis 1 ni mwana wa Mtaliano aliyekuwa akifanya kazi katika shirika la gari Moshi kabla ya kuhamia nchini Argentina miaka ya zamani.
Kama kadinali wa Jimbo la Buenos Aires ,Kadinali Bergoglio amekuwa mkosoaji mkubwa wa serikali ya Argentina.
Hata hivyo Kadinali Bergoglio anapendwa sana na wafuasi wa kanisa hilo huko Argentina na hasa watu maskini.
adinali Jorge Bergoglio, mwenye umri wa mwaka 76, kwa karibu miaka yake yote kama Kasisi amehudumu nyumbani kwao Argentina.
Kadinali huyo wa Jimbo la Buenos Aires inasemekana aliibuka nambari mbili wakati Papa Benedict alipochaguliwa mwaka 2005
Anaaminika kuwa na ujuzi mkubwa ambao wengi wanasema utamsaidia sana katika uongozi wake.
Katika maisha yake ya huduma kwa Kanisa Katoliki huko Amerika Kusini ambapo Kanisa Katoliki lina waumini wengi zaidi duniani, Kadinali Bergoglio ameibuka kuwa mtu anayependa sana udhabiti wa kisiasa katika nchi zilizo katika bara la Amerika Kusini.
Bergoglio anasifiwa kwa kuleta mageuzi makubwa katika Kanisa la Argentina huku katika eneo hilo la Amerika Kusini Kanisa bado linashikilia itikadi za kale.
Chanzo:BBC Swahili.
tunaomba mwenye ujuzi atufahamishe asili na historia ya moshi mweusi na mweupe ktk Bible au kitabu chochote.
ReplyDeleteNi tukio ambalp wengi wanaliona likifanyika kama ishara ya kupatikana au kukosekana Papa mwengine lakin nini asili yake hasa.
BLACK SMOKE means BAD news no new pope. WHITE SMOKE means GOOD news there is a new pope. Isn't this a racist at its best? Untill now BLACK is regarded to be be BAD. And there were some people believed that this was the time for pope of africa origin!! It will never happen as BLACK IS NOT GOOD, IT IS THE SIGN OF BAD NEWS!!!!
ReplyDeleteWhat happened to those 2 African cardinals? Walisema kuwa wana chance? Naona wameenda kwa mzungu mwenzqao. Son of an italian immigrant :)
ReplyDeleteAmina, Mungu Baba mwana na Roho Mtakatifu amuongoze Papa Fransisko ktk kuongoza kanisa hili kubwa duniani linalopigwa na mawimbi ya shetani
ReplyDeleteIm very disappointed, i expected pope from africa..why not? Why not?
ReplyDeleteNo All Popes have been caucasian (White) Most have been Italian.
ReplyDeleteThere have been three African popes.
http://en.wikipedia.org/wiki/African_popes lists them:
Pope Victor I (189 to 199)
Pope Miltiades (310/311 to 314)
Pope Gelasius I (492 to 496)
Their actual race is not known, however, but at least Miltiades appears to have been a native of Africa.
The first black pope was Pope St. Victor I. He served from 186-197 A.D. and lived in North Africa. He was the 15th Pope. Victor I was the pope who changed the language of the church
ReplyDeletefrom Greek to Latin. He also was responsible for determining when Easter would be celebrated. And then there was Pope St. Militiades, who was pope from 311-314 A.D., when
Constantine the Great ruled the Roman Empire. Constantine was the first emperor of Rome to allow freedom of religion in that part of the world. In 324 A.D., Constantine adopted Christianity
as the official religion of the empire.
The third black pope was Pope Saint Gelasius I, who was the 49th Pope, serving as pope from 492 A.D. to 496 A.D. Believe it or not, Gelasius I established February 14 as Valentine’s Day,
in honor of St. Valentine, who reportedly burned at the stake because of his faith. Gelasius I was the last African pope. "
Selfishness ni tatizo sana kwetu hasa watz. ukishajifananisha na moshi lazima utajilinganisha kwa umri, ukabila pia udini. hebu semeni ni rangi gani mliona inafaa. au kwa nini unatumia taa kupata mwanga kama unauenzi weusi. mnashindwa kabisa kuwaza vitu vyenye maendeleo na kuleta maana. haya wewe unauliza why not from africa. inamaana wanaenda kuangalia ni bara gani kadrinal anatokea ili awe papa? wapendwa wanajamii haya ndio yanayotupeleka kufanya maamuzi mabovu kila siku. UVIVU WA KUFIKIRI NA KUTAKA SHORTCUTS
ReplyDeleteUsituletee ukabila wewe hujui kama kulikuwa na vote? Mbona hamchagui Rais muhindi hapo bongo? Kulikuwa na Cardinals 77 na mmoja tu ndiyo alikuwa anatakiwa sasa kama black haku pita una kuwa disappointed na nini next time nenda ukapige kula na wewe
ReplyDeleteHahahaha Wadau msikate tamaa kwa kusekana kwa Pope Mwafika kama mlivyoahidiwa safai hii.
ReplyDeleteLa muhimu endeleeni na Sala za Rozari kama Wakatoliki kamili, msienze mambo ya Uwana maombi na Upinzani Kanisani.
Si Lazima Pope awe mweusi bora Imani,
ReplyDeleteMchakato ulikuwa mgumu sana kama mnavyoona hata Ma Kadinali weupe wa nchi ingine wamekosa, ni kuwa wamependa apatikane Mu mwenye damu ya Italia.
Hivi mimi Mkonongo nikihamia Uingereza Ukonongo wangu utatoka?
Be patient time will came for the black Pope we need to pray hard.
ReplyDeleteIt does not matter whether it's black, blue or yellow. God cares most of our hearts than the races. After all before Gods eyes we are all his children.
ReplyDeleteNyagabona, G.P BIG UP SANA I LOVE YOUR COMMENT.
ReplyDeleteKUNA WATU SIO IMANI YAO BASI KELELE NYINGI WAO WANAWAHUSU NINI HUYU NI POPE WA 266 TARATIBU HIZOHIZO ZILIKUWA ZINATUMIKA YEYE KINAMKERA NINI? KAMA SIO IMANI YAKE ASEPE
Jamani umeme hapo bongo ukikatika mnapiga kelele kweusi tiiii, mbona msishangilie Tanesco wameleta giza meaning kweusi tiii, kama unauenzi weusi,mbona mnataka mwanga, meaning kweupe! hizi rangi zisilete poor me attitude. namjibu huyooo anayesema black ni bad news.Kama mnaeunzi weusi bibi harusi wote waanze kuvaa shela jeusi tuone.
ReplyDeleteMsiwe na wasiwasi wadau, iko siku inakuja Moshi mweupe utafuka kuashiria kupatikana kwa Papa Mweusi kutoka Africa, Mungu hana ubaguzi wa rangi ni hawa binadamu tu, mmesema na amewasikia subirini mtaona kwa macho yenu na mtabaki midomo wazi siku hiyo.
ReplyDeleteVile vile hana makuu huyu inasemekana. Kwenye siku ya kwanza kapanda basi na makadinali wenzake badala ya gari la kifahari la papa. Aidha hata akiwa kadinali huko Argentina inasemekana alikuwa akiishi katika fleti badala ya kasri la kikadinali; isitoshe alikuwa akijipikia mwenyewe. Sijui kama ataweza kuyaendeleza yote haya katika ukuu wake mpya na ni unyenyekevu wa kiasi gani atakaouleta katika wadhifa wake huu mpya.
ReplyDeletewakatoliki watatetea sana hii hoja ya moshi mweupe moshi mweusi lakini ukweli wabakia pale pale, ni suala kubwa sana ukilitafakari ikiwa linafanyika kwa kanisa kubwa kama hilo.
ReplyDeletemoshi ni moshi tu uwe mweusi ama mweupe yote ni mizuri kinachosikitisha ni iweje hawa watu wa mungu waseme moshi mweusi si mzuri kwa kuchaguliwa papa, wapi aliandikwa na nani alisema.
wanaotetea hii hoja na kusema ni sawa tu ni wale wote ambao wamekwisha badilishwa mawozo na hawa watu weupe yaani ni watumwa wasiojijua katika nafasi ya watu weupe. kwani ninauhakika kabisa hao watu weupe waliliweka makusudi ili suala ni kumuumiza tu kisaikolijia mtu mweusi. wametuwekea vitu vingi tu sio huo moshi tu ata hilo gauni la bibi halusi liwe jeupe kwani akivaa jeusi harusi haifani, kwani tukiita ikulu kama nyumba ya raisi haifai mpaka tuiite nyumba nyeupe,
eti mwingine anafananisha giza na mwanga kama weusi na weupe, ni vitu viwili tofauti na ndio maana vina majina tofauti. inabidi watu weusi na sisi tutafute protokoli zetu siku kila siku kufuata za kwao.
yaani katika kutafuta huyo papa hawakuona njie mbadala ata moja zaidi ya uo moshi mweusi na mweupe, come on.
duuu... Msikwazike sana, ndivyo maisha ya livo.. Mkatae mkubali papa ndio huyo wakwetu.!!!
ReplyDeleteLa muhimu muukubali Utezi huo na kamwe msifanye maandamano kupinga!
ReplyDeleteIf you are shallow you will discuss naive matters, but true religion is for the soul and not the colour. Look beyond. This is not politix.
ReplyDeleteClarification iliyotolewa na vatican - Jina lake ni
ReplyDeletePapa Francis na siyo Papa Francis I.
Ataitwa Papa Francis I huko mbeleni atakapochaguliwa papa mwingine na akachagua jina la Francis huyu Papa mpya ataitwa Francis II na wa sasa hivvi atakuwa Francis I.