Mkuu wa Jeshi la Polisi IJP Said Mwema akifafanua jambo mbele ya wajumbe wa kamati ya kudumu ya baraza la wawakilishi Zanzibar (hawapo pichani) wakati wa kikao cha pamoja kujadili mambo mbalimbali yahusuyo usalama.Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Baraza la Wawakilishi Hamza Hassan Juma na kushoto ni Kamishna wa Utawala na Raslimali watu Clodwig Mtweve kikao hicho kilifanyika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Dar es Salaam.
Mkuu wa Jeshi la Polisi IJP Said Mwema, mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Baraza la wawakilishi Zanzibar, Mhe. Hamza Hassan Juma, (Kulia) Kamishna wa Utawala na Raslimali watu Clodwig Mtweve na kamishina wa Polisi Zanzibar Mussa. A. Mussa wakipitia hati ya maboresho ya Jeshi la Polisi wakati kamati hiyo ilipotembelea makao makuu ya Jeshi la Polisi, Dar- es salaam.
Mkuu wa Jeshi la Polisi IJP Said Mwema akiagana na wajumbe wa kamati ya kudumu ya baraza la wawakilishi Zanzibar baada ya kumaliza kikao cha pamoja cha kujadili mambo mbalimbali yahusuyo usalama kikao hicho kilifanyika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Dar es Salaam. (Picha na Frank Geofray wa Jeshi la Polisi)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...