Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Said Mwema, wapili kutoka kushoto akikata utepe kuashiria kufunguliwa rasmi kwa Programu ya Mafunzo kazini kwa askari wote nchi nzima yaliyofanyika jijini Dar es salaam, akifuatiwa na Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es salaam DCP Suleiman Kova, Mkuu wa chuo cha Taaluma ya Polisi (DPA) ACP Ally Lugendo na kushoto ni Mkuu Kitengo cha wa Mafunzo SACP Alice Mapunda.
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Said Mwema akikagua program ya Mafunzo kazini kwa wakaguzi wa Polisi pamoja na askari, ukaguzi huo ulifanyika Makao makuu ya Polisi jiji Dar es salaam.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Said Mwema, akiwa na maofisa wa Polisi wakifuatilia kwa karibu uzinduzi wa program ya mafunzo kazini kwa kutumia mtandao, tukio hilo lilifanyika jijini Dar es salaam.
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Said Mwema akikagua Utekelezaji wa Programu ya mafunzo kazini kwa maofisa wa Polisi( kushoto ni Msemaji wa Jeshi la Polisi Advera Senso), ukaguzi huo ulifanyika Makao Makuu ya Jeshi Polisi ( picha na Frank Geofray- Jeshi la Polisi) .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hii ni habari njema. Pia wawe na Continuous Development Program.

    ReplyDelete
  2. Kuwe na gym kila wilaya au mji kwa askari kupunguza unene. Askari anatakiwa kuwa mkakamavu siyo legelege. Wale ambao wanatunza vitambi wawe wanasimamishwa kazi mpaka vikiisha ndiyo warudi kazini.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...