JAJI Mkuu wa Zanzibar, Jaji Omar Othman Makungu akiuzindua mtandao wa Jumuia ya Majaji,mahakimu na makadhi wa Zanzibar (ZAJOA) kushoto Rais wa ZAJOA, Jaji Abraham Mwampashi, uzinduzi huo ulikwenda sambamba na mkutano mkuu wa mwaka wa jumuia hiyo uliofanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Habari kikwajuni mjini Zanzibar leo.
JAJI Mkuu wa Zanzibar, Jaji Omar Othman Makungu akipata maelezo juu ya mtandao wa Jumuia ya Majaji,Mahakimu na Makadhi wa Zanzibar (ZAJOA) kutoka kwa mjumbe wa kamati tendaji ya jumuia hiyo, Mohamed Ali Shein muda mfupi baada ya jaji mkuu kuuzindia mtandao huo, kushoto Rais wa ZAJOA, Jaji Abrahman Mwampashi uzinduzi wa mtandao huo ulikwenda sambamba na Mkutano mkuu wa jumuia hiyo uliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Habari Kikwajuni mjini Zanzibar leo.
JAJI Mkuu wa Zanzibar, Jaji Omar Othman Makungu akiufungua mkutano Mkuu wa Jumuia ya Majaji, Mahakimu na Makadhi wa Zanzibar (ZAJOA),kushoto Rais wa Jumuia hiyo, Jaji Abraham Mwampashi na kulia Msaidizi Rais wa ZAJOA, Jaji Fatma Hamid Mahmoud mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa Wizara ya Habari Kikwajuni mjini Zanzibar leo.
WAJUMBE wa Jumuia ya Majaji,Mahakimu na Makadhi wa Zanzibar (ZAJOA) wakimsikiliza Jaji Mkuu wa Zanzibar, Jaji Omar Othman Makungu wakati akiufungua mkutano mkuu wa jumuia hiyo uliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Habari Kikwajuni mjini Zanzibar leo.(Picha na Haroub Hussein).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...