Jarida la katuni linaloandaliwa na mchoraji katuni, Nathan Mpangala, limeanza kurushwa leo, Alhamisi, likiwa na sura mpya kwa kusheheni katuni kibao ili kukidhi haja ya wapenzi wa katuni wa ndani na nje ya nchi.
Jarida hilo ambalo litakuwa likipatikanakwenye link; www.nathanmpangala.blogspot. com, linatambulikwa kwa jina la ‘Jarida la Katuni la Nathan’ au kwa kidhungu; ‘Nathan Cartoons Magazine’ linalenga kuongeza wigo wa matumizi ya katuni nchini kwani kwa miaka mingi, katuni zimekuwa zikitumika zaidi kwenye zaidi kuliko njia zingine.
Jarida hilo litakuwa likipambwa na katuni za kisiasa, uchumi, michezo na karakta maarufu zilizokuwa zikitoka magazetini siku za nyuma kama; Kijasti, Mzungu Mtaani, Daladala Laivu nk. Pia litakuwa na katuni mahsusi kwa ajili ya anga za kimataifa.
Mbali na katuni pia litakuwa na habari mbalimbali za mashindano ya katuni yanayoendelea ulimwenguni ili kuwawezesha wachoraji wa Kitanzania kushiriki.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...