Taarifa iliyoifikia Globu ya Jamii hivi punde zinaeleza kuwa  yule dereva aliyemgonga askari polisi wa usalama barabarani WP 2493 CPL-Elikiza  Lokisa Nko na kutokomea, amekamatwa jana usiku masaa kadhaa baada ya kupoteza uhai wa askari huyo maeneo ya Bamaga mapema jana mchana.

Kwa Mujibu wa Mkuu wa Kikosi cha Polisi cha Usalama barabarani nchini, Kamanda Mohamed  Mpinga amesema leo kuwa gari lilohusika kwenye ajali hiyo aina ya Landlover Discovery rangi nyeusi limepatikana likiwa limefichwa maeneo ya Tabata dampo jijini Dar.

Kupatikana kwa gari hilo kumekuja baada ya Polisi kufuatilia na kujua mmiliki wa gari hilo kuwa ni kanisa la TAG chini ya Mchungaji Wambura, ambaye kwa ushirikiano alioutoa dereva aliyetambuliwa kama Jackson Stephen, alijulikana na hatimaye kupatikana

Kamanda Mpiga ametoa taarifa hiyo mbele ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete jioni hii nyumbani kwa Marehemu hukoUnunio kiasi cha kilomita 25 hivi Kaskazini mwa jiji la Dar. 
Rais Kikwete pamoja na uongozi wa juuu wa jesgi la polisi walifika kuhani msiba huo nyumbani kwa marehemu ambaye ameacha  Mume na watoto watatu. Mume wa marehemu pia ni askari polisi.

Pichani juu Rais Kikwete akimfariji mume wa marehemu na watoto wake pamoja na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Saidi Mwema.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Ankali nimekuona nunauza sura na kamela yako kwenye clip. Anko unauza sana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...