Kituo cha mafuta cha Oil Com kilichopo eneo Nane Nane mjini Morogoro kimekamatwa leo kwa wizi wa umeme baada ya kuharibu mita ya umeme kwa kuweka rezista kwa lengo la kupunguza upimaji wa mita ya umeme. Kituo hiki ni cha pili kukamtwa na kikosi cha ukaguzi toka makao makuu, ndani ya masaa mawili yaliyopita na kituo kingine ni cha Oil Com kilichopo eneo Kihonda
Mafundi wa Tanesco wakitoa waya zote za umeme zilizokuwa zinapeleka
umeme Oil Com baada ya kukamatwa kwa wizi wa umeme
Kituo cha mafuta cha Oil Com kilichopo katika eneo
Kihonda Mkoani Morogoro kimekamatwa kwa wizi wa umeme na kikosi cha ukaguzi
toka makao. Ni hujuma na ambazo kama zikiendelea ni hatari kwa uhai wa Shirika
hili la umma.
Meneja wa Kituo (kushoto) akipewa maelekezo baada ya kushuhudia mita ilivyohari biwa
Mita ya umeme iliyoharibiwa toka Kituo cha mafuta cha Oil Com kilichopo
eneo Nane Nane.
Mita iliyoharib iwa
kwa kuwekewa rezista kupunguza upimaji wa mita
Meneja wa kituo cha mafuta cha Oil Com kilichopo eneo Nane
Nane ambaye ndiye meneja wa kituo cha mafuta cha Oil Com kilichopo eneo la
Kihonda (kulia)akishuhudia mita ya umeme iliyoharibiwa
ikijaribiwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...