Na Mroki Mroki-Father Kidevu Blog-Moshi
 
 Wanariadha kutoka Nchini Kenya wameendeleza Umwambawao katika mbio za Nyika za Kilimanjaro ‘Kilimanjaro Marathon 2013’ zilizofanyika leo mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.

Wakenya walidhihirisha umwamba katika Mbio za Kilometa 42 baada ya Mkimbiaji wao Kipsang Kipkemoi (pichani) kunyakua nafasi ya kwanza  katika mbio hizo za mwaka huu upande wa wanaume na Wanawake ilinyakuliwa na Mwana dada Edna Joseph aliyebeba Medali ya Dhahabu.

Nafasi ya pili hadi ya tano kwa wanaume ni Julius Kilimo, Dominick Kiagor, Onesmo Maithiya Loshile Moikari ambapo upande wa wanawake ni Eunice Muchiri, Frida Too, Rosaline David na Jane Kenyara.

Jumla ya wakimbiaji 65000 walishiriki mbio za Kilimanjaro Marathon 2013.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Wakenya wanaichukulia riadha kama ajira yao. Vijana wao wengine wametengeneza pesa kwenye huu mchezo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...