Marehemu STEPHEN MUJUNI STEPHEN 

Leo tarehe 15 Machi 2013 ni miaka 13 tangu ututoke hapa duniani. Tulikupenda sana ila Mungu alikupenda zaidi kaka. Bado tunakumbuka Upendo wako, uchangamfu, ucheshi, uchapakazi, na kutoa msaada wako kwetu bila kuchoka.

Unakumbukwa na baba yako, dada zako, kaka yako, wajomba, jamaa na rafiki zako. Tunaamini kuwa kimwili hauko nasi ila kiroho tuko pamoja. Tutaendeleza yale uliyokuwa ukiyafanya wakati wa uhai wako. Bwana ametoa na Bwana ametwaa, jina la Bwana libarikiwe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Oh no!!! Maskini Stephen mtoto wa dk Stephen kumbe alishafariki dunia? how sad!!! Nilimuacha Bugene Sec nadhani akiwa form 2 1992. Mcheshi, mcheza mpira wa miguu mzuri yeye na rafiki yake somebody Kalelangambo...Nimesikitika sana...Mungu ampe baraka za milele na awape nguvu na uzima ninyi ndugu zake mliobaki.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...