Tanzania itakuwa mwenyeji wa Siku
ya Kimataifa ya Miti (World Wood Day)
ambayo huadhimishwa tarehe 21 Machi kila mwaka. Waziri wa Maliasili na Utalii
Mhe Khamis Suedi Kagasheki atakuwa Mgeni Rasmi katika maadhimisho hayo ambayo
yatafanyika kwenye Viwanja vya Karimjee Dar es Salaam.
Siku ya Taifa ya
Miti huadhimishwa duniani kote kuhamasisha watu kuhusu manufaa ya miti katika
maisha ya kila siku ya binadamu ili waweze kuitunza na kuitumia kiuendelevu.
Kaulimbiu ya mwaka
huu ni: Mbinu za kitamaduni za kutumia miti ni nzuri (A cultural approach to achieve wood is good).
Tarehe 21 Machi
itakuwa ni siku ya kilele cha maadhimisho hayo ambayo yataadhimishwa kwa siku
nne mfululizo tangu tarehe 19 hadi 22 Machi kwa kufanya shughuli mbalimbali
zilizopangwa.
Baadhi ya shughuli
hizo ambazo zitaanza tarehe 19 Machi katika viwamja vya Karimjee ni:
·
Maonyesho ya bidhaa zitokanazo na miti;
·
Mashindano ya bidhaa zitokanazo
na miti, za hapa nchini na za kutoka nje;
·
Kutoa na kujadili mada kuhusu
Utamaduni wa Kupenda Miti;
·
Kupanda miti katika wilaya ya
Kisarawe;
·
Kutembelea VETA Chang’ombe;
·
Mashindano ya uchoraji kwa
watoto.
Maadhimisho haya
huratibiwa na Chama cha Kimataifa cha Utamaduni wa Miti (International Wood Culture Society) ambacho kiliasisiwa nchini
Marekani mwaka 2007 kwa nia ya kuwatia moyo watu wajenge utamaduni wa kupenda
miti.
Mwaka huu Tanzania
imechaguliwa kuwa mwenyeji wa siku Siku ya Kimataifa ya Miti kwa kuwa
imeonyesha juhudi za kuwashirikisha wananchi wake katika kuhifadhi na kupanda
miti.
Wananchi wanakaribishwa kuhudhuria mikutano na maonyesho yote
yaliyopangwa katika viwanja vya Karimjee maana hakutakuwa na kiingilio chochote.
[MWISHO]
George Matiko
MSEMAJI
WIZARA YA MALIASILI NA
UTALII
17 Machi 2013
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...