Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni jana (Tar 12/03/2013) kwa kauli moja ilipitisha bajeti ya Tshs. 156,439,616,904 kwa ajili ya miradi ya maendeleo na matumizi ya kawaida wakati wa Kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika katika ofisi za Manispaa hiyo, Dar es Salaam.

Kati ya fedha hizo Tshs. 49,206,498,064 ni mapato ya ndani ya Manispaa, ambapo zaidi ya 50% ya bajeti imelenga kuhudumia miradi ya maendeleo zikiwemo barabara, maji, shule, hospitali, mikopo ya vijana na wanawake na masoko.

Meya wa Manispaa hiyo, Yusuph Mwenda alisema Manispaa yake imejipanga kuhakikisha inasimamia miradi hiyo ili ilete mabadiliko ya kuchumi katika Manispaa hiyo.

“Tumejizatiti kuisimamia vizuri miradi hii ili ilete tofauti katika Manispaa yetu ya Kinondoni.” Alisema.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda akizungumza wakati wa kikao cha Bajeti cha Manispaa hiyo kilichofanyika jana (Machi 12) katika ofisi za Manispaa hiyo, Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu wake, Songoro Mnyonge na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Mhandisi Mussa Natty.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Mhandisi Mussa Natty akizungumza wakati wa Kikao cha Bajeti cha Manispaa hiyo kilichofanyika katika ofisi za Manispaa hiyo, Dar es Salaam jana (Machi 12). Katikati ni Meya wa Manispaa hiyo, Yusuph Mwenda na Naibu wake, Songoro Mnyonge.
Sehemu ya Madiwani wa Manispaa ya Kinondoni wakifuatilia kwa makini wakati wa Kikao cha Bajeti cha Manispaa hiyo kilichofanyika katika ofisi za Manispaa hiyo, Dar es Salaam jana (Machi 12).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Manispaa ina budget ya mabillion? Kipato chao ni kodi tu au kuna miradi mingine ya kuingiza hizo pesa.

    ReplyDelete
  2. Anyways ngoja tuone kama hizo barabara na miradi mingine itatekelezeka! Mwaka uliopita kwa mfano daraja linalounganisha eneo la Kinzudi -Goba na Kinzudi Kwa Mtenga ambacho ni kiunganishi cha watu takribani elfu 80 kwenda kwenye shughuli zao za kiuchumi katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dsm lilichakachuliwa kwa maelezo rahisi tu eti zilisolve tatizo la wahanga wa mafuriko ya 2011Dec.

    ReplyDelete
  3. ingekua vizuri kama wangewaelezea wananchi ni miradi gani inayolengwa kukamilishwa kwenye hiyo bajeti,kwa mfano ni madaraja gani au ni barabara zipi waiweke wazi kusudi isipotimia waweze kuambiwa sababu ni nini kwa sababu hizo ni kodi zao.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...